Wednesday, August 20, 2008

Nchi inayumba, Kikwete vaa sura ya Kagame

Shikamoo,

LEO nimeamua kuandika waraka huu kwako Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka inayokaribia mitatu sasa tangu ushinde na kuapishwa mwaka 2005 baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu.

Napenda kutumia fursa hii kukupa pole kwa kazi ngumu ya kuongoza kundi la watu wengi wenye njaa ya tumbo, njaa ya ubongo na njaa ya tiba bora.

Hakika njaa zinazowakabili Watanzania ni nyingi na hazina ukomo, hasa zikiainishwa kwa nafasi binafsi, kaya, kata, kijiji, miji, majiji na taifa kwa ujumla wake.

Ni mnafiki pekee anayeweza kukudanganya, au wewe mwenyewe kudanganyika (ingawa hili najua siyo rahisi kwako kwa kuwa umeyaishi maisha ya wengi wetu), kwamba mambo ni shwari kila mahala. Kwamba HAKUNA MATATA.

Nakumbuka vyema, na bahati nzuri bado ninaendelea kuirejea hotuba yako ya mara ya kwanza Bungeni Dodoma ambayo ilisheheni ahadi na namna nzuri ya kumpunguzia Mtanzania ufukara (unaojumuisha njaa zote alizonazo).

Kila Mtanzania aliyekusikia siku ile ukiwa umetulia na kuisoma vyema, atakubaliana nami kwamba hotuba ile ndiyo ilikuwa dira yenye mwanga wenye miali ya kuchoma na kuunguza kero nyingi za watu wako waliokuchagua, hata wale wasiokipenda chama chako – CCM, kwa kura za kishindo.

Ni hotuba ile iliyohuisha hatma ya maisha yao iliyokuwa imefikia mahali pa kuonyesha kukata tamaa, hata kama waliokutangulia walikuwa wakitamba kwa hadithi za kukua na kuimarika kwa uchumi mkuu, ilhali maisha ya watu yakiendelea kudhoofika.

Kadri miaka ilivyokuwa ikisonga, hasa ule mwaka wa kwanza, matumaini ya watu wako yaliendelea kukupa muda kwamba neema ya kweli yaja. Hakuna aliyeonekana kuwa na haraka ya hiyo neema iliyoonekana katika hotuba yako na hata dhamira yako iliyojionyesha kuchukizwa na umaskini wao.

Hata hivyo, ikiwa miaka mitatu inakaribia kukatika, asilimia kubwa ya matumaini waliyokuwa nayo watu wako wengi, kwamba wewe ndiye mkombozi aliyepo, inapungua kwa kasi ya kutisha, hata kama wasaidizi wako, hasa wale wanafiki na wanaojipendekeza watakueleza vinginevyo.

Uhakika ni kwamba hata wewe unalitambua hilo kupitia kwa watu wako wengine wa karibu, wale wanaoitwa –mawaziri wa jikoni wa rais-hasa wanafamilia uliowapa jukumu la kukusanya ‘maneno’ ya watu wako huku kwetu mitaani.

Kasi ya kupungua kwa asilimia kubwa ya matumaini ya watu wako yanajiegemeza katika matukio mabaya yaliyoikumba nchi yetu, yakiwa yanafanywa ama na wasaidizi wako, uliowachagua kwa imani kubwa, au wafanyabiashara wenye kuhusiana nao.

Hilo halina kificho na wala hakuna haja ya kukueleza vinginevyo, kwani hata wao wenyewe walitambua na sina uhakika kama walijutia kuhusika kwao na dhambi za kuongeza ufukara kwa Watanzania, lakini angalau waliamua kuachia ngazi kwenye madaraka uliyowapa na wengine kuikimbia nchi, wakijificha huko walikotanguliza ‘vijisenti’ walivyowaibia watu wako.

Ufisadi. Ufisadi. Ufisadi. Hii ni dhambi ambayo imekuwa ikilaaniwa na wapenda nchi yao, ikiwa inabeba na dhambi nyingine nyingi, ambazo zimekuwa, siyo kero tu, bali mzigo mzito wa gharama za maisha kwa watu wako.

Ni ufisadi huo ambao umeongeza bei ya umeme, bei ya vyakula, ada kwa watoto wetu, nauli kupanda na hakika umegusa kila sehemu ya maisha ya wananchi wa Tanzania, kiasi kwamba serikali nzima unayoiongoza ikaonekana inachusha kwa kila mtu, isipokuwa mafisadi wenyewe, wake zao, watoto wao na hata vimada wao.

Sasa leo wakati utakapokuwa ukilihutubia Bunge, mjini Dodoma, watu wako wenye kukata tamaa, wanataka uongee. Wanataka uzungumzie masuala yanayowakera kila uchao kwa sasa. Hawataki siasa ambazo tumezizoea zinazotolewa na viongozi wetu wanasiasa.

Wananchi wanataka kusikia namna unavyochukia ufisadi kwa dhati ya moyo wako. Wanataka kukusikia na kukuona ukikunja ndita kuwalaani na kutoa amri kuu ya kuwachukulia hatua kali mafisadi wote wanaofifisha juhudi binafsi ulizoanza kuzionyesha mwanzo wa uongozi wako.

Binafsi, msema kweli mpenzi wa Mungu, nikushangae kidogo kwa kushindwa hadi sasa kuwakemea wakuu wafuatao; Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kwa kushindwa hadi sasa kuwakamata watu walioandikwa katika ripoti uliyokabidhiwa majuzi juu ya uchunguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya je (EPA).

Kwamba kwanini hadi sasa hawajawaadabisha mafisadi wake wakati timu yao imekamilisha kazi? N’nachojua mimi ni kwamba wao kwa kazi zao wangekuwa wamewakamata watu hao kwanza na ndipo baadaye wakupe ripoti hiyo.

Polisi wanatakiwa kuwakamata wahalifu hao, baada ya Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Takukuru kuthibitisha kuwa walihusika na wizi huo, sasa wanasubiri nini au mpaka uwaeleze wawakamate watu hao? Wao wanafanya kazi gani, yaani kukupa ripoti basi? Wanasubiri nini? Au nao tuseme wako pamoja nao kama tulivyoshuhudia baadhi yao wakitetea wizi ambao bado unasumbua kupatikana kwa neema ya Tanzania?

Kama hawajawakamata tuseme hawajawatambua hadi sasa. Ikiwa ripoti hiyo imejaa maneno matupu kama ya ukasuku wa wanasisa, tafadhali achana nayo kabisa na usiisome kwani itakuondolea zaidi asilimia za imani kwa wananchi wako.

Idadi kubwa huku mitaani tunakopita na kuzungumza na wapiga kura wako, wengi wanaonekana kushangaa timu hiyo uliyoiunda, kwamba inasubiri nini.

Mbali na hilo, wananchi wanatarajia kuwa utazungumzia na kutoa msimamo juu ya ‘mgogoro’ wa Muungano, hatma ya maslahi kwa wafanyakazi na zaidi sana suala zima la neema kwa kila Mtanzania.

Rais Kikwete, vitabu vitakatifu, ambavyo naamini unavithamini na ndiyo mwongozo wako, kabla ya Katiba, vinasema kuwa ukiona maovu yanatendeka, basi yazuie hata kwa upanga ili yasiendelee, ukishindwa yakemee hata kwa ulimi na ukishindwa kabisa, basi onyesha kuchukizwa na kuchukua hatua, hata kwa kupitia wengine.

Hatua za namna hii, zimetumiwa zaidi na Rais wa Rwanda Paul Kagame na hatimaye sasa nchi hiyo iliyokuwa imegubikwa na vita, inapanda kwa kasi katika chati yake ya kuwaletea neema wananchi wake.

Utakapofaya hivyo, hakika utakuwa umemtendea haki Mungu Mkuu na waja wake Watanzania na thawabu zitarundikana katika fungu lako.

Nakutakia kila jema uwapo Dodoma na unapojiandaa kwa safari yako ya Marekani.

Wasalaam

Simon Martha Mkina
Simu: 0754 020880
Email: smkina@gmail.com
Blog; http://www.mkina.bloghspot.com/

Labels:

Tuesday, July 08, 2008

sss

video

Labels:

Tuesday, July 01, 2008

Tanzanian journalists in US trip speaks

Get to know what our colleagues, journalists who are touring Maine University and other international  newsrooms are saying about their work environments back home. Please visit:   wlbz2 television

Labels:

Monday, June 30, 2008

US Judge praises Tanzania


District Judge of Maine in United States, John Woodcock has said Tanzania is a real model in Africa concerning peace and development.

Judge Woodcock (pictured) expressed this when he was speaking to six Tanzanian Journalists who are visiting Maine University in Orono city mid this week.

"We know that Tanzania is almost the only country in Africa that has been experiencing smooth transition election and shifting of power, this is very nice," he said in one of district chambers.

The most respected judge in the US said African countries needs to pick a leaf from Tanzania should they want to have tangible development and peace.

He praised Tanzanians for keeping peace as their first priority in building their nation and asked them to keep it secure.

Speaking on corruption in The US, Judge Woodcock said for five consecutive years he had not received any case brought to him over corruption.

"For more than five years now, I have never come across any case on corruption, but this doesnt mean that there is no corruption in the US, it might be there in a small scale," he added.

 This is contrary to Tanzania judicial circles whereby corruption cases are the order of the day, including grand corruption based on government funds embezzlement.

Tanzanian journalists are in the US for ix weeks training course sponsored by USAID. Te trip will take them to New York and Washington where they will visit some international class newsrooms and organisations.    
    

Labels:

Sunday, June 29, 2008

In the USA


Hi my buddies,

Not see you long time men, you know what I was busy with my almost flopped trip as one of you were praying on my failure to come :)- No worry anyway.

Right now am giving Barack Obama a hand on his road to the White House next year.

To  be straight am in Maine State, at Maine University for my short course in International journalism. It is a nice state university with state-of-the- art equipments and well trained tutors (professors, mind you).

Our training is superb, based much in first hand experience with a minimum bookish-old- fashioned teaching.

As I arrived a little bit late, am catching up what my buddies, we are six Tanzanian journalists, were  taught in the class and outside.

We have visited some tv stations and print newsrooms around so far, expecting to travel again to Washington and New York where we will be visiting some international class newsrooms and meeting with UN big fishes, without going places to see what New Yorkers and Washingtoners enjoy their life. 

Also, depending on financial muscles, will do a little shopping, Gods will, for our extended families at home.  

I will keep you posted

Love you and remain blessed

Labels: ,

Monday, March 03, 2008

why aren't black Tanzanians running the economy?


THIS world is not fair at all, especially The African and Black World. Go every corner in their world you find that black natives are the ones who don’t benefit much from what our Creator has give them. This is contrary to the world govern by our fellow Whites.

In Japan, the Japanese run the economy, in Germany, the Germans hold and run the entire economy to own benefits. In America, the Americans, especially those with light skinned are the ones who chew freely the economy while the original natives- the Red Indians are segregated.

In India, the economy is for Indians and for the Indians themselves. They can give out some assistance to other countries, but there should be more Indians. Like they portraying in Tanzania.

All those nationals they are benefiting the diamonds, golds, oil, uranium, waters, lands and all sort of God-given natural resources.

In Africa, it’s very contrary to that. The economy, natural resources; golds, diamonds, lands, waters and the like are managed and benefiting light skinned comers.

Why aren't the Africans, Tanzanians to be precisely running the economy? This is the biggest challenge I faced the other day from an American friend who paid a visit to my office. He kept on asking questions. Why you people are so poor? Are you mean? Don’t you have committed leaderships?

He said, he would expect to see Tanzanians leading very nice life as they have all precious lands, weather, natural resources and the like.

Why are you so poor? I told him I don’t know just as President Jakaya Kikwete does. He don’t know either why are we so poor to the extent that people are not aware of their next meal when they get one.

In Tanzania, white people; includes Indians, Americans, Germans are made up about 4% of the population but controlled most of the economy. In Tanzania the populations nears 40 milion.

They control 25% of the land, 92% of the banking, all manufacturing, all tourism, 74 % of gold, diamond and Tanzanits reserves. Hivi sisi tumerogwa!

For leaving all those big percentage in hands of foreigners, no matter they have bought citizenships, black Tanzanias are going backwards, even though we occupy 90 % of the population."

We need economic consciousness and to mobilise one another's spirit. We need economic leadership for ownership and control and we must work at owning our own intellectual property. Tanzanians needed economic solidarity.

We need black economic solidarity so that we can support each other. Black people don't have solidarity like the white people do. Ni ubinafsi tu kwa kila mmoja. I wonder.

Wednesday, February 27, 2008

Kikwete soma haya. Nyerere anakuasa


Nilishituka katika usingizi na kujisikia mzito kupita kiasi na ghafla nikajikuta niko katika katika nyumba moja ya kawaida kabisa mahali ambako nikaaminishwa kwamba ndipo makazi halisi ya Baba wa Taifa.

Kwa kuwa kazi yangu ni kutafuta habari, nilihitaji sana maoni ya Baba wa Taifa, mtu ambaye anaujua kwa dhati uchungu wa Tanzania, watu wake na rasilimali zake na mara moja nikamkabili mzee huyo ambaye alikuwa anaonekana kuwa mwenye mawazo mengi na hudhuni iliyomfanya kuwa na uso uliochoka.

Nilisita kumuuliza kuhusu kilichokua kikinikera kwani alianza kulia aliponiona hali iliyonifanya nami nishindwe kujizuia kububujikwa na machozi.

Nilianza kulia naye alinikumbatia na kuniambia, “nalilia Tanzania yangu, najutia yaliyotokea. Sikujua kwamba niliyemuamini amefanya yale niliyoyapinga kwa nguvu zangu zote.”

Nilipata ujasiri na kutoa kijitabu changu cha kuchukua dondoo za habari ili nianze kunukuu maneno yake. Kwa bahati mbaya nilikuta kijitabu hicho kimejaa, hakina nafasi kubwa ya kuandika.

Nikaokota vipande vya karatasi jirani na tulipokuwa tumekaa na kuanza kuandika maneno hayo. Katika mazungumzo yetu nilijiona mpumbavu kwa kutokuwa na kaseti ndogo ya kurekodi, baada ya kuona mazungumzo yananoga.

Nilitaka kujua undani wa maneno yake, na kwa kweli hakuwa na mengi ya kuzungumza na mahojiano yalikuwa mafupi mno, kasi cha kunifanya nipate maneno machache kutoka kwake.

Baada ya kusema analilia Tanzania yake, Mwalimu alisema, “zimwi la ajabu lenye mapembe ya rushwa, kulindana na matumizi mabaya ya madaraka, limeimeza Tanzania yangu. Msikate tama, pambaneni. Mwambie Jakaya (Rais Jakaya Kikwete) aangalie.”

Baada ya maneno hayo nilipoteza ujasiri maana nilipoteza mwelekeo na sikuweza kuendelea na mahojiano yake kwa kina. Katika hali ya kawaida, mimi sio mtu wa kushindwa kufanya mahojiano na mtu yeyote, hasa nikipata nafasi lakini kwa Mwalimu nilikwama.

Kabla sijaondoka aliniomba nimsindikize akapumzike kwa kuwa alikuwa amechoka. Nilimshika mkono na kumepeleka hadi chumbani kwake, ambako kulikuwa na vitanda vitatu na kabla hajalala akasema, “Nilimzuia Jakaya mwaka 1995 nikijua mwenzetu amekomaa na ni msafi kumbe amekuja kuniaibisha kabisa.”

Hayo ni maneno machache na pengine kutokana na kuguswa nayo, ndiyo niliyoweza kuyanukuu nilipozinduka huku uso wangu ukiwa umetapakaa machozi.

Nimejiuliza na kuwauliza watu wa karibu nami kuhusiana na ndoto hiyo, lakini nimepata majibu mchanganyiko ndio sababu hasa nimeamua kuwapa nafasi Watanzania wa Mwalimu Nyerere nao wapate maneno hayo. Sio lazima wayaamini, lakini wapate ujumbe.

Mara baada ya Mwalimu kufariki, nilipata kuota ndoto ambayo alinieleza huku akitembea kwamba niwaambie ‘jamaa zangu’ kwamba hajapendezwa kabisa na kuuzwa ama kubinafsishwa kwa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), jambo ambalo nakumbuka aliwahi kuliweka wazi wakati wa uhai wake tulipokuwa mjini Arusha.

Siku hiyo ilikuwa ni ziara ndefu ya kuanzia Dar es Salaam, Iringa mjini na hatimaye vijijini na baadaye Arusha, safari ambayo nilibaini ukakamavu wa Mwalimu katika umri wa utu uzima na hiyo ilikuwa miezi michache kabla ya kwenda nchini Uingereza kwa matibabu, safari iliyokuwa ya moja kwa moja. Hakurejea tena akiwa hai. Alipoteza maisha yake akiwa huko baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya damu.

Lakini, hadi sasa sifahamu kinachonisukuma kuwa na hisia kali na Mwalimu Nyerere, kwani kabla hata ya kutangazwa kuugua kwake, nilipata kuwaeleza wakubwa wangu wa kazi wakati ule, Salva Rweyemamu, aliyekuwa Mhariri Mtendaji wangu ambaye tulikubaliana kuwa na subira kabla ya kuandika habari hiyo.

Ilikuwa ni gazeti moja litolewalo kwa wiki kwa lugha ya Kiingereza ndilo lililotusukuma kuanza kuandika habari za ugonjwa wa Mwalimu, kwani liliandika habari ikielezea kwamba Mwalimu amezidiwa na amesafirishwa kwenda nje ya nchi, jambo ambalo halikuwa sahihi wakati huo. Tukaandika ukweli kwamba anaumwa, lakini yupo nchini.

Tuliendelea kufuatilia habari zake hadi siku ambayo alikuwa akiondoka nchini kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi (Swiss Air), siku ambayo ni waandishi watatu tu ndio walikuwapo uwanja wa ndege, Absalom Kibanda, ambaye sasa ni Mhariri wa Tanzania Daima na mpiga picha Emmanuel Herman, ambaye amerejea tena Habari Corporation.

Siku hiyo nakumbuka, uwanjani hapo kulikuwa na kundi la waandishi wa habari waliofika kupokea wanamichezo waliofika Dar es Salaam kwa ndege ya Swiss Air iliyomchukua Mwalimu, lakini baada ya kuwapokea wanamichezo waliondoka bila kujua Baba wa Taifa anaondoka kwa mara ya mwisho kwenda Uingereza.

Nakumbuka baada ya makosa kadhaa ya kitaaluma kutokea, nilimwambia Kibanda kwamba Mwalimu hatorudi. Sikuwa na sababu zozote za kusema maneno hayo na hakuna aliyezingatia maneno hayo na ndio maana hata mpiga picha wetu Herman hakupiga picha za kutosha katika tukio hilo. Niliumia sana.

Nakumbuka hata waliomsindikiza hawakuwa watu wazito kwani alikuwapo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, John Chiligati na upande wa Polisi, alikuwapo aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam, Salum Mkwama, na pia ofisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Nje, ambaye alikuwa pale kusimamia itifaki.

Hata aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, alikutana na Mwalimu pale VIP akiwa katika safari zake na hakuwa katika orodha ya waliofika kumsindikiza Mwalimu na mkewe Maria, huku familia ikiwakilishwa na mabinti wawili ambao walionekana wakiipungia mkono ndege ikiwa angani.

Hisia hizo zinanipeleka siku ya kifo chake, nilipojikuta nikianguka mara baada ya kuona sura ya Baba wa Taifa pale nyumbani kwake Msasani na haikuishia hapo kwani nilitoka nyumbani kwenda kusindikiza mwili Uwanja wa Ndege kwenda Butiama, lakini nilijikita nikidandia ndege ya jeshi la Afrika Kusini kwenda Musoma na hatimaye Butiama.

Haikuwa jambo la kawaida, kwani sikuwa na chochote zaidi ya nguo nilizokuwa nimevaa hata niliponyeshewa na mvua tukiwa katika msafara wa mwili wa marehemu sikuwa na nguo za kubadili na huko nilimkuta muongoza kwaya, Ansbert Ngurumo, ambaye naye “alizamia” kufika Butiama; hakuwa ameaga ofisini. Tulivutwa na mzimu wa Nyerere.

Hata Benjamin Mkapa, akiwa Rais aliyekuwa madarakani, alisema mbele ya kaburi la Mwalimu kwamba watakaofanya mambo kinyume na wosia wa Baba wa Taifa, “jinamizi lake litawashukia,” na kwa hakika inaelekea sasa “jinamizi” linaelekea kumshukia yeye.

Hakuna ubishi kwamba mambo mengi ambayo Mwalimu aliyapinga kwa nguvu zake zote hadi anakata roho, Mkapa ameyakiuka ikiwa ni pamoja na sio tu kushindwa kabisa kupambana na rushwa, bali pia yeye binafsi kujihusisha na rushwa na ufisadi.

Mwalimu alipinga kabisa Ikulu kutumika kujinufaisha, lakini mara tu alipoaga dunia, Mkapa alianzisha kampuni akitumia rasilimali za umma, ikiwa ni pamoja na majengo, magari, wataalamu na hata kuamua kabisa bila aibu kushirikiana na waziri wake, Daniel Yona kufanya biashara wote wakiwa madarakani.

Pamoja na kufahamu wazi kwamba Baba wa Taifa alipinga kabisa kuuzwa kwa NBC, Mkapa alijenga uhusiano wenye utata mkubwa na wamiliki wa benki hiyo, uhusiano ambao ulimuwezesha kuendelea kujineemesha yeye na familia yake na kujitanua kwa kujipatia nyumba nyingine jirani na ile aliyokuwa akiishi pale Sea View, Dar es Salaam.

Ni Mkapa huyo huyo ambaye sasa tunaambiwa kwamba kwa baraka zake, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imefanya ‘madudu’ ya ajabu ambayo kwa hakika ndiyo yaliyofanya Baba wa Taifa, aniijie katika ndoto baada ya kubaini kwamba nimekuwa nikiumia sana kwa jinsi Tanzania yetu ilivyotumbukizwa katika “janga la kujitakia”.

Hakuna asiyefahamu kwamba Mkapa alitetewa kwa nguvu zote na Baba wa Taifa, wakati huo akionekana kama mtu pekee msafi katika kundi kubwa la wanasiasa walioomba kuwania urais mwaka 1995, mwalimu huko aliko sasa anajuta, lakini anamwambia Jakaya aangalie.

Mwalimu analia Jakaya angalia, Tanzania na Watanzania kwanza mambo mengine baadaye, tuko nyuma yako ukiamua.

Kuamua kwa Kikwete kutatokana na utashi wake binafsi na sio wa mashabiki wala watu waojikomba kwake.

Ni kuamua ndiko kutampa sifa na baraka tele kutoka kwa Mungu Mkuu baada ya kutovaa sura ya aibu kwa watu ambao wanamkwamisha kutekeleza azma yake.

Azma kubwa ya Kikwete ni maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini sasa anaonekana kushindwa na wengi tunaamini kuwa anaweza, isipokuwa anaangushwa na hao wapambe wanaomzunguka.

Wapambe wake ni wengi wakiwamo marafiki zake, wasaidizi wake wa karibu serikalini ambao kila jambo wao wanaona ni hewala, wakati ukweli ni kwamba Watanzania wanateketea na kutomuamini rais wao waliyemchangua kwa kura nyingi.

Ni vyema, sasa Kikwete akaamua kabla muda haujawa mwingi, akawatosa wote wanaomuangusha na kumfanya kukosa thawabu.

Nakumbuka Simba wa Vita, Waziri Mkuu mstaafu, Rashidi Mfaume Kawawa aliwahi kukieleza kikao kimoja cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, kwamba ni vyema mtu anayetoboa jahazi akatoswa mapema, kwani kulelewa na kushangilia huku akiendelea na hujuma zake, mwisho wake ni abiria wote, pamoja na nahodha kuzama na kupoteza maisha.

Kikwete, wakati wa kuwatosa wote wanaokuangusha ni sasa na usijali urafiki, uswahiba au undugu na watu wa aina hiyo na hapo utakuwa umeokoka na kulitendea haki taifa la Watanzania.

Labels:

Lowassa sasa aanza kutapatapa


Unamkumbuka mtu huyu aliyekuwa anafukuza wenzake hata kwenye mikutano ya hadhara? Akifokea viongozi wa wilaya mbele ya wakwe, wake, watoto na ndugu zao! Sasa naye ameamua kuachia ngazi, hataki tena uwaziri mkuu wa Taznania. Ameamua kwenda kuchunga ng'ombe kwao Monduli.


Namtakia mapumziko mema, ikiwa wenye nchi hawatakasirika na kumkamata kwa kumhoji na hatimaye sheria kuamua nini kifanyike kwake na kwa wengine wenye tabia kama yake ambao walishirikiana kuruhusu kampuni ya kitapeli, kampuni hewa kuliingia taifa kwenye mkenge wa mwaka.


Pamoja na kumshauri, siku tatu baada ya kuwa ameachia ngazi kwamba asizungumze lolote kwa vyombo cvya habari, sasa anaonekana kukadi, a ameazna kuwaita waandishi na kuwaomba eti wamsafishe. Jamani Lowassa acha utazid kuchafuta.


Anasema eti ohh... mbona Mwinyi alijiuzulu na baadaye akawa rais. kwamba naye anaweza kujariu bahati yake.


Haya nisimkatishe tamaa tusubiri wakati ndiyo utakuwa mwamuzi murua.




Labels:

Sunday, August 26, 2007

Uchumi unakua na Lowassa wetu

NImemsikia Waziri Mkuu Edo Lowassa akisema kuwa uchumi unakua kwa kasi.
Wengi wamezungumzia kauli hiyo ya mtendaji mkuu wa shughuli za serikali Bungeni mjini Dodoma aliyoitoa wakati akiahirisha Bunge la wale wakubwa wanaojiita wawakilishi wa wananchi, ilhali ukweli unaonekana kuwa kidogo katika hilo.
Edo alisema wachumi wanathibitisha kuwa uchumi unakua na kwamba wanaokejeli kauli yake ni watu wasiokuwa na utambuzi wa namna uchumi ulivyo.
Nami kama walivyo Watanzania wengi, sina ugomvi na kalu hiyo, ingawa napata shaka mno kulinganisha ukuaji huo na hali halisi yauchumi wa mwananchi mmoja mmoja.Hata aee namna gani, Lowassa hawezi kueleweka kwa wananchi wa kawaida ambao bado wanakula mara moja kwa siku, tena ikiwa ni kipande cha muhogo na kusukumia kwa maji, mabayo siyo safi wala salama.
Hali hiyo inaonyesha ugumu wa maisha ulivyo sasa, kuliko hata kipindi kirefu kilichopita ukiondoa tu kile kipindi cha nyuma ambacho watu walilazimishwa kula dona la Yanga. Nilikuwepo wakati huo na nilishuhudia namna marehemu baba yetu alivyokuwa akitudamsha kuwahi nafasi katika foleni kweye maduka ya ushirika ili tupate kilo mbili tatu na kipande cha sababu.
Ni vyema, Lowassa na wanene wenzie wakaona nana njema ya kueleza wananchi ukuaji wa uchumi ambao unaendana na hali zao za maisha, vinginevyo wananchi hawataelewa ana maana gani anapowaambia ukuaji wa uchumi ilhali maisha yao yanakuwa magumu kila uchao.

Tuesday, July 31, 2007

Wakitushindwa, tuwabane watupe elimu ya neema

WAPO viongozi wa kada mbalimbali; mawaziri, manaibu wao, makatibu wakuu. Wapo pia wabunge na wawakilishi na wakuu wa taasisi kadhaa za serikali.

Nimewaona wakurugenzi wa idara muhimu za serikali, nimewagusa wakusanya kodi wa nchi hii ambao wanatajwa kutumia ‘akili’ nyingi kuikumbatia ‘neema’.

Nao waandishi wa habari, madaktari, wauguzi, wataalamu wa maeneo kadhaa ya kusimamia rasilimali za nchi hii, ambazo kimsingi zinapaswa kuwafaidisha wananchi wote bila kujali rangi, kabila, uwezo wa kifedha wala wa kiakili na zaidi maeneo wanakotoka au wanakoishi, lakini zinaishia mifukoni na kwenye matumbo ya hao wachache na wale wanaowategemea.

Idadi kubwa ya Watanzania ambao nimewataja na hata ambao hawajaguswa hapa, ni wepesi kutumia ‘akili’ zao kujineemesha binafsi badala ya kuangalia umma mpana wa Watanzania, unaohitaji zaidi kujituma kwao, uaminifu wao na uzalendo wao katika ujenzi wa nchi hii kwa faida ya taifa.

Hata hivyo, hakuna anayeonekana kufanya hivyo, kila mtu alipo anajitahidi kuchukua anachojidanganya kuwa ni mali yake binafsi au eti ni bahati yake kwa kuwa tu ana nafasi ya kuomba, kutoa rushwa na kufanya ufisadi mwingine unaohujumu uchumi na rasilimali za Tanzania.

Inashangaza watu hao waliopewa dhamana na taifa, au kukabidhiwa na ndugu zao au marafiki zao wenye ukuu katika maeneo kadhaa wakitumbua kila chembe ya neema ya Watanzania wote na kujidai kuwa ni kundi lisilohusika na kilio cha umasikini unaobeba magonjwa, ujinga na madhila mengine makubwa ya Watanzania wengi.

Eti wao ni watu wanaojiona kuwa na dunia yao ndani ya ardhi ya Tanzania. Hawana chembe ya utu kwamba mali wanazohujumu moja kwa moja au kwa kushirikiana na wale tunaowatambua kuwa ni wachimbaji na wachukuaji wa rasilimali zetu kwa manufaa yao.

Hao wachukuaji wa rasilimali zetu, kwa kutuona siye ‘hamnazo’ wanatudanganya kwa pipi na peremende na wakati mwingine wakituletea shanga, ili wake zetu wavae au tutengenezee viatu na mapambo, huku wakifaidi neema isiyooza tuliyoshushiwa na Mungu kwa ustawi wetu, lakini sasa ni kinyume chake.


Tunawakumbatia, tena wakati mwingine kwa kukenua hadi magego kuonekana kwa kicheko, pale shule za watoto wetu zinapopewa eti msaada wa kujengewa matundu ya vyoo, kuchimbiwa visima na hata kununuliwa mipira miwili - mitatu eti kutoa mwanya kwa vijana wetu kujiburudisha. Tumekwisha.

Wanaochekelea namna wanavyowanyonya Watanzania wenzao kwa kuruhusu rushwa kutembea, dawa za kulevya kusambaa na kutumiwa na vijana wetu, na kuona tukiibiwa rasilimali zetu huku wao wakisimamia, kamwe hawatadumu na furaha waliyonayo sasa kwa kuwa historia, itawahukumu hata kama wamekufa.

Hivi inawezekana namna gani Mtanzania tunayemfahamu kwa miaka mingi akiwa mtumishi wa serikali, akilipwa mshahara tunaoutambua akawa na mahekalu, magari ya kifahari, akisomesha watoto wake nje ya nchi kwa gharama za kupaa na zaidi akifanya manunuzi bidhaa za matumizi ya familia yake nje ya nchi?

Inawezekana vipi kiongozi ambaye tunayefahamu mshahara wake akamiliki nyumba ya milioni 200, wakati mshahara wake ni sh. 900,000 kwa mwezi. Huyu hata kama atadai amekopa pesa benki hawezi kuwa na hekalu lenye thamani ya namna hiyo. Atakuwa ametuibia tu.

Mtanzania wa aina gani atakubali kuwa mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la serikali linalojinadi kuwahudumia wagonjwa wa ukimwi au kupigania ubora wa elimu akiwa na majumba na biashara kubwa Ulaya na Marekani kwamba mshahara au posho zake zinamuwezesha kuwa na mali nyingi kiasi hicho? Hakuna, lazima atakuwa ametumia migongo ya wanaotaabika kwa ugonjwa au ujinga kujineemesha.

Haiingii akilini, hata kwa kijana aliyemaliza darasa la saba akaamini kuwa mkusanya kodi akawa na meli na huku akitumia ndege ya kukodi kumsafirisha mkewe na watoto kusalimia wazazi wake mikoani, kwamba ni ujira wake ndiyo unaomtosha kufanya kufuru ya namna hiyo. Huu ni unyang’anyi wa silaha zaidi ya SMG.

Majizi na mahujumu ya uchumi yanatofauti gani na majambazi au majangili ambayo kila uchao tunayatangazia vita, huku tukiyasahau manyambizi yanayohujumu na kudumisha madhara kwa vizazi na vizazi?

Katika Tanzania ya leo, kila mmoja anapopata nafasi ya kuhudumia jamii kwa kusimia shughuli kwa niaba yetu sote, anaona amepewa upenyo wa kujineemesha kwa rushwa na kuhujumu uchumi kwa kadri ya uwezo wake wote. Tabia hii ya dhambi ya kutisha sijui imetoka wapi, nani kaileta na amejificha wapi miaka yote hii bila kutiwa nguvuni?

Hivi usalama wa taifa unaofanyika sasa ni kuhakikisha tu wakubwa wanaishi raha mstarehe bila hofu? Au majukumu yao siku hizi yametofautishwa na kulinda mambo kama hayo.

Jukumu la kunusanusa hao wanaoharibu taswira ya mbeleni ya nchi hii ambayo, bila kushtuka sasa itakuwa na kiza kitupu kwa watoto wetu wa sasa na hata wale wajao, limetolewa mikononi mwao?

Hao wanaohujumu uchumi wetu, wanapaswa kujulikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili, ili kwamba Tanzania yenye neema iwezekane kwa wote na siyo hao wanaobahatika kupata dhamana za kusimamia huduma na rasilimali zetu sote.

Kama tunadhani wanaojitajirisha wana akili za ziada za kutafuta neema, basi usalama wa taifa uwakusanye na kuwalazimisha kuelimisha jamii pana namna akili walizonazo zinavyofanya kazi kwa kila mmoja ili Watanzania wote waishi kama wao.

Inawezekana kuwa na Tanzania yenye ustawi kwa wengi ikiwa kila wenye dhamana watajitoa na kuweka uzalendo mbele na kuacha ubinafsi, tabia na mwenendo wa maisha ya chura wenye taswira ya; yangu…yangu…

Saturday, July 07, 2007

Enzi za Uhai wa Amina Chifupa


Hii ndiyo sura ya Mbunge wa Viti Maalum (Vijana) CCM, Amina Chifupa. Picha hii ilipigwa muda mchache baada ya kuukwaa uwakilishi wa vijana.

Labels:

Friday, June 22, 2007

Ni mpambano wa Bajeti na wananchi, washindi wabunge


Jamani,

NIMESHANGAA sana leo, eti wabunge wetu, ambao kazi yao kubwa ni kupitisha au kutishia kutopitishwa kwa geresha, hatimeye wamepitisha kwa kauli moja Bajeti ya Serikali ya mwaka 2007-2008.

Kimsingi, bajeti hii iliongoza kwa kupingwa na wananchi na wengi wakiamini wabunge, bila kujali U-CCM wao au hata vyama vingine, wangekuwa pamoja na wapiga kura wao. Lakini wapi, mambo yanayosomwa na waheshimiwa sana mawaziri, ndiyo kinachopita, bila kujali nini na wapi nani anapinga nini.

Imeshapita hivyo, basi tuendelee kuwa pamoja wananchi kwa kuumia na machungu ya bajeti hiyo itakayoanza kuuma Julai Mosi.

Haijalishi wewe una gari, unatumia barabara, unatumia mafuta ya taa au hata maji kufika ofisini kwako na kurejea nyumbani, lakima umekamuliwa kiasi ambacho huwezi kupumua. Tuombe Mungu Mkuu atatunusuru.

Wabunge waliotarajiwa na wananchi, wameshindwa kufanya lolote kuondoa angalau senti kadhaa kwenye bajeti, achana na shilingi.

Nawaapia kwa jina lolote, isipokuwa la Mungu Mkuu, kwamba usiku huu Waziri Mkuu, Mawaziri, wabunge wote, na hata waandisi waliokuwa wakiandika kuonyesha namna bajeti itakavyoua mtazamo wa serikali wa kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na maisha bora, watakavyokuwa wakitafuna vyuku, kunywa mibia na mvinyo, kusheherekea kupita kwa bajeti hiyo.

Hata wewe msomaji unakaribishwa ukiwa Dodoma, kusogea eneo la tukio na angalau kufaidi harufu ya vyakula vinono.

Ninasema vita vya bajeti na wananchi, washindi wamekuwa wabunge.
Pichani anaonekana Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society, John Ulanga akimuuliza swali Waziri Zakhia Meghji. Huenda angekutana naye jana angemuuliza; Waziri hiv kweli bajeti hii itanasua umasikini kwa watu wetu? Jibu analo?

Labels:

Saturday, June 16, 2007

NAOMBENI KURA NDUGU ZANGU

Aslaam Aleykhum,
Mambo,
Nimeamua kutumia salamu zote hizo kwa wanablogu wenzangu ili niwe pamoja nao, najua jumuwata ina wanachama wa kila imani na wengi hupenda kupata salamu inayowagusa, inawezekana wapo hawataguswa na mojawapo ya hizo, lakini nawahakikishia kuwa tupo pamoja na tutaendelea hivyo.
Ninajitokeza kwa mara ya kwanza kuomba kupewa ridhaa ya kuongoza jumuia yetu kwa nafasi ya uenyekiti.
Ninafanya hivyo kwa kuwa nimepata taarifa za ruhusa kuanza kampeni. Ninafanya hivyo kwa moyo mkunjufu kuwaomba ridhaa zenu ili tuhsirikiane kukuza jumuia yetu ambayo ni changa, lakini yenye mwelekeo wa kuwa kubwa na kukomaa kwa muda mfupi endapo itakuwa na viongozi makini, wenye kushirikisha wanachama wote.
Ninazo sifa za kuongoza. NAOMBENI KURA ZENU.
Aksanteni

Labels:

Thursday, May 31, 2007

Maisha magumu ya ukimbizi


Jamani,

Nimeipata picha hii kutoka kwa rafiki yangu mmoja ambaye anadai lazima kila mtu apinge, kwa nguvu zake zote, kuwepo kwa vita na machafuko katika nchi za Afrika.

Anasema vita ni vibaya mno, havina macho na huua na kuvuruga familia na pia kusababisha kuwepo kwa wakimbizi kama anavyoonekana mama huyu akiwa na mtoto wake wakionekana kuhisi njaa baada ya kupakiwa katika gari la kile chombo kinachoitwa UNHCR ili kurejeshwa kwao.

Mama huyu na mtoto wake walisombwa na mkumbo wa kuikimbia nchi yao ya Burundi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na sasa anarejeshwa nyumbani ambako anaonekana hana hakika endapo amani inayoelezwa kuwepo ipo.

Tukemee vita na machafuko yote popote pale ili kuepusha adha na mhangaiko mingine inayoweza kuepukika.

Tutumie blogu zetu kutangaza na kuhimiza amani na upendo huku tukimtaka kila mmoja kuchangia nguvu na mawazo yake katika kukuza maendeleo.

Labels:

Tuesday, May 29, 2007

Joto linapozidi Dar!


Dar es Salaam pamoja na zile zinazoelezwa kuwa raha zake, bado kuna tatizo moja kubwa; joto. Hali hii imechangiwa mno na mgawo wa kisirisiri wa umeme unaoendeshwa na shirila linalojidai kuwa la wananchi la kusambaa umeme la Tanesco.

Ona sasa matajiri wameamua kuwanunulia wanyama wao wapendwa vijifeni vya kuwapoza na adha hiyo.

Jamani Tanesco, acheni kutukandamiza kwa kutunyima umeme, ilihali mabwaya yote yamejaa, mwingine ukiwa unazalishwa na dada yake Richmond na huku ule unaoongezwa kwa malipo makubwa na mjomba wao IPTL ukiwa umejaa tele pia. Haya...

Labels:

Ukimwi na wanablogu


jamani wenzangu,

Nimejitokeza kuomba ridhaa ya wanablogu wote na wasiokuwa wanachama, kupata ridhaa ya kuwa mwenyekiti, lakini nimekumbuka kitu kimoja kikubwa, kwamba nasi tuko katika mapambano makubwa ya kuutoomeza ugonjwa wa ukimwi. Nimekuwa nikieleza na kushauri namna ya kuuepuka ugonjwa huo kupitia machapisho na hata katika ukurasa wangu huu wa blogu.

Kwa mara nyingine tena, naomba wanablogu wote tuwe mstari wa mbele kupinga kuwepo kwa ukimwi na tukiweza kuwasaidia walioathirika na kuathiriwa na ugonjwa huo unaoweza kumpata yeyoye bila kujali midevu yake, umri wake, uwezo wake wa fedha wala akili na busara.

Tuko pamoja kuutokomeza

Labels:

Ninagombea uenyekiti

Jamani wenzangu katika mawasilinao ya kisasa yasiyohitaji ukiritimba wa wale viongozi wa habari wanaojiita waharirir, nimerejea.
Kupotea kwangu kwa muda katika ulimwengu wa blogu kuna sababu kubwa. nayo ni kuwepo maeneo ya porini kwa muda mrefu. Huko hakuna umeme, hivyo kuninyima muda na fursa inayoambatana na haki yangu ya kuandika na kusoma mambo mengi ya mtandaoni ikiwemo blogu.
Nimekasirika mno kutambua wananchi wengi, hasa wa vijijini wanakosa uwezo na nafasi ya kuchangia fikra zao kwa uhuru mkubwa na hatimaye kusikika kutokana na kuosekana kwa nguvu ya nishati inayozalisha umeme, licha ya nchi yetu kuwa na madevu yenye mvi kwa kuwa na umri wa miaka 46.
Nikiwa mwenyekiti, kwa maana ya kuongoza kwa msaada mkubwa wa wanachama wote na wasiokuwa wanchama wa blogu Tanzania, tutahakikisha maeneo mengi yanakuwa na umeme kwa kuoiga kelele kibao kwa serikali ili kuharakishwa kwa usambazaji wa umeme vijijini.
Tushirikiane ili tuwe pamoja katika kushika maendeleo ya kweli na siyo yale yanayosikika masikioni yakitangazwa kwa mbwembwe na wakubwa wetu.
Tutafika kwa kuweka mbele maslahi ya taifa na blogu

Labels:

Friday, January 19, 2007

Wakubwa wakitafakari jamani


Nimeona niwaeleze ukweli kuhusu namna viongozi wenu wanavyowapigania ili muwe na maisha bora, hapa msidhani eti wamelala. Wakubwa hawalali, bali hapa wanatafakari kwa kina namna ya kuwaondoa wananchi wetu katika lindi la umasikini. Tusiwahukumu jamani viongozi wetu. Hapa wanaonekana wakitafakari aliyokuwa akiyazungumza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Januari 12, 2007 wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi jinsi serikali na viongozi unaowaona na wengine wasiokuwepo namna wanavyopambana usiku kucha, hawalali wakihangaikia matumbo ya wananchi wa Tanzania.

Labels:

Monday, December 11, 2006

Simon Mkina aombwa kuingia jengo hili


Leo nimepata mgeni katika ubongo wangu. Sikumtarajia kabisa muda huu kuwasili, tena katika kipindi hiki ambacho hata machungu ya wengine aliowatembelea wakaudhika, bado hayajawatoka.
Sikuwa nimelala, bali mchana kweupe, nikiwa natafakari namna ya kupata habari nzuri za kuuza gazeti langu jipya la serikali. Sikumkaribisha, bali alijikaribisha mwenyewe katika kichwa changu. Sijui anatafuta nini!
Laki siyo vibaya nikiwaeleza mgeni hyo kwamba anaitwa Mawazo. Alipokuja alinieleza anaomba kuishi katika kichwa changu kwa muda mfupi na kunieleza nia ya ugeni wake; eti anataka nikagombee ubunge ili iweze kuingia katika jengo linaloonekana nyuma ya kichwa hapa katika picha hii niliyopigwa na Mroki Mroki wakati nikiwa Dodoma kuandika habari za waheshimiwa sana wabunge wetu.
Sijajua iwapo niendelee kumkaribisha au kumtimua, maana naona kama amewahi sana na muda huu siyo muafaka, asije akanikosanisha na wakubwa wangu, kaka zangu na jamaa zangu wengine ambao wako madarakani kabisa au wapambe wao.
Nipeni mawazo yenu jamani, nimfanye nini mgeni huyu au nimtimue kwa sasa.

Wednesday, December 06, 2006

Tanesco haooooo! wameumbuka!


Tanesco, kwa wasiojua ni shirika la kuzalisha, kusambaza na kuuza umeme kwa Watanzania.
Ni shirika ambalo linabeba nembo nzuri yenye kuonyesha twiga, mnyama mrefu, mpole na mwenye ufahamu wa maadui zake kwa kasi zaidi. Lakini, Tanesco wenyewe wanaonekana kutowajali zaidi wateja wao, hivyo sielewi kwao mteja ni nani; mfalme au pagazi tu wa kule Comoro.
Yaani utashangaa kuona namna wanavyohudumia wateja wao. Ni viibaya mno hata kama unawapelekea pesa, na ikiwa unakwenda na tatizo la kuomba kuunganishiwa nishati hiyo ya kuzalisha mwanga, ndiyo utakoma. Ngoja niwaache kwanza kwa sasa, ingawa jambo kubwa linaloudhi ni namna wanavyohangaika kuongeza gharama za umeme wa wananchi wa kwananchi.
Eti walikuwa wakipigania kuongeza bei ili wananchi wa Kikwete na Mungu waumie zaidi, yaani wakamuliwe zaidi vijisenti wanavyovipata kwa taabu, tena katika mazingira haya yasiyokuwa na umeme.
Katika 'move' yao hiyo, Kikwete akaona ohhoooo... wananchi wake wataumia mno, na kauli mbiu yake ya 'maziwa na asali' kwa kila Mtanzania itafifia. Ameapiga stop kwamba hakuna kupandisha bei ya umeme wala nini. Kula Tano Kikwete wetu...wembe ni ule ule kwa maji, dawa na tiba, usafiri na hata bia na katika zile hoteli kubwa zinazojipangua madaraja kwamba ni za nyota tano.
Tanesco haooooooooooooooooooooooooooooo, wameumbuka.

Thursday, November 30, 2006

Nani kasema milima haikutani


Kuna kudanganyana kwingine hakufai kabisa. Mtu anatambua kuwa ni vibaya kutangaza uongo, lakini anaendelea nao miaka nenda rudi na kuwarithisha watoto na ndugu zake wengine, na wao wanasambaza kila mahali, hata katika machapisho.

Miongoni mwa uongo mkubwa ni kwamba milima haikutani! Nani kasema. Jamani mbona kuna milima inayoporomoka ikiwa jirani na kukutana au inaposombwa na maji, kama yale yaliyotokea wakati wa tsunami! Nani hajui kuwa kulikuwepo milima iliyokutana?

Tukiacha hiyo, ipo milima inayokutana mara kwa mara na mara nyingine zaidi ya mara nne au tano kwa siku. Kama unabisha njoo nikupeleke Namibia kwa masharti ya kunilipia gharama za usafiri na pesa za kujikimu.

Huko nitakuonyesha milima inayokuwepo asubuhi na mchana inapotea. Hiyo inawezekana kabisa ikatoka eneo kama Manzese kwa Mfuga Mbwa na kukutana tena eneo la Magomeni Mapipa. Siyo utani na wala sitanii. Soma kuhusu dunes na utaelewa nasema nini.

Hebu ona picha ya milima hiyo inayoweza kuhama na kukutana. Niliipiga nilipokuwa Namibia, jirani na mji wa Swakopmund.

Thursday, November 23, 2006

Nipo nimejaa tele kama Lowassa


Nilikuwa Bungeni Dodoma wakati mkuu wangu wa kazi Edward Lowassa alipoanza kughani mashairi akimjibu mshairi mmoja aliyekuwa akieleza kwamba wako wapi watu waadilifu na wachapakazi wenye uzalendo mkubwa baada ya Nyerere.

Lowassa alisema; Tupo Tumejaa Tele.

Mshairi alitoa changamoto na Lowassa akajibu kwa changamoto, sasa changamoto ni kwa wananchi kuibua changamoto zenye kuiongoza nchi katika changamoto kuu za kuwaondolea wananchi wetu changamoto ya umasikini iliyogubikwa na changamoto ya changamoto chanya na hasi.

Nawaachia nyie wasomaji wa Kona Yangu huku picha yangu, nikiwa na Rais wa Msumbiji Comarade Amilio Guebuza nikiwa nimejaa tele...tele...tele kama tetele-mwitu.

Wednesday, November 22, 2006

Simon on the move

Jamani mashabiki wangu natumai hamjambo.
Sikuonekana hapa kwa kipindi cha miezi miwili kutokana na kutingwa na majukumu ya utalii, niliamua kuondoa upofu wa kujua nchi yetu. Niliamua kuzunguka vijiji na mitaa yote ya Tanzania.
safari hii haikufadhiliwa na yeyote, bali iligharimiwa na mifuko yangu binafsi. Niliamua kukata mazoea kwamba watalii ni wazungu pekee wanapotoka kwao.
Uhakika ni kwamba nimefurahi sana kuondoa tongotongo kuhusu maisha ya Watanzania wenzangu wanaoishi vijijini ambako, kwa ukweli wa Biblia, wanaishi chini ya mstari wa umasikini.
Nikiwa huko nimevumbua mashamba, nyika na mapori kama walivyofanya waliokuwa wakiitwa wavumbuzi wa mwanzo, kina carl Peters na Dk. Livinstone. Yapo mengi nitakayoeleza siku chache zijazo.
Baada ya kurejea Bongo, nikaanza safari tena ya jiji la dar es Salaam kutoka majengo ya gazeti la Uhuru hadi kuweka makazi katika gazeti la daily News. Nitawaeleza baadaye mission yangu hapo.
Nisiwachoshe sana, maana jioni imeingia na hakuna umeme, sitaki kuingia nyumbani kwangu nikishika kuta ili kuepuka kujigonga katika meza na samani zingine chache nilizobahatika kununua.
baadaye basi.

On the move

Thursday, September 21, 2006

Wasomi wetu na uwakili wa shetani

NINAWAHESHIMU sana wasomi makini wanaotumia bongo na uelewa wao kuchangia maendeleo ya taifa na wananchi wake, lakini ninawadharau na kuwaponda wasomi wasiotumia bongo zao kuleta mabadiliko yenye faida.

Nchi nyingi makini, zenye kuwajali wananchi wake zinawatumia sana wasomi katika kubuni, kuandaa na kutekeleza mipango yenye mwelekeo wa kusaidia upunguzwaji wa hali duni za maisha.

Katika nchi hizo, wasomi mara nyingi wanakuwa wasemaji na watangazaji wa mipango iliyochanganuliwa na wasomi tayari kwa utekelezaji.

Hata hivyo, zipo nchi zenye wasomi wanaopenda kutumia fursa walizojiwezesha wenyewe ama kuwezeshwa na jamii ama serikali kupata elimu kutumia bongo na uelewa wao kukandamiza hao waliowatuma, siyo kufuta ujinga tu, bali kupanua na kukomaza uelewa.

Kundi la wasomi hawa ni wale ninaowadharau kwani wao wanatumia mwanya wa kuwa na vyeti (sema karatasi ukitaka) kutoka vyuoni kurubuni, kutapeli, kudumaza na hata kuua wenzao na taifa kwa manufaa binafsi.

Wengi wa wasomi wa aina hiyo ndiyo wale waliojazana katika ofisi wakiwa wasaidizi wa Rais, Waziri Mkuu na viongozi wengine wa juu wa serikali na hata Chama.

Ni watu ambao wanaaminiwa mno na viongozi wetu kwa kuchambua na kuchaganua mambo, lakini kumbe ndiyo hao hao wanachagia kuharibu maendeleo yaliyopo au yaliyokusudiwa.

Mipango mingi ya maendeleo ya Tanzania ambayo inaonekana kushindwa ilibuniwa na kuadikwa na wasomi tunaowaamini, lakini kumbe nia na madhumuni yao makubwa hayakuwa kuwakomboa Watanzania, bali kuona kujinufaisha wao.

Miradi mikubwa ambayo imegharimu kiasi kikubwa cha fedha zetu, tunaiona ikilegalega na kusababisha matatizo makubwa ya kiuchumi na kijamii. Wakitafutwa walioibuni na kuisimamia ni wasomi tulionao.

Inawezekana kabisa wasomi wakajitetea kwamba wanasiasa ndiyo wanaokwamisha mafanikio ya michanganuo ya miradi wanaoibuni au kuisimamia, lakini ukweli ni kwamba wanaosababisha ongezeko la ugumu wa maisha ni wasomo tunaowategemea kusaidia jamii kwa ujuvi wao.

Katika kundi hili nilalolitaja la wasomi, waandishi wa habari nao wamo, kwani wanaonekana kushindwa kutumia mwanya walionao kuielimsha jamii na kubaki kushabikia habari zisizokuwa na kichwa wala miguu, eti wakitaka kuuza magazeti yao na kuburudisha basi!

Mara kadhaa Kona Yangu imenusanusa kuhusu namna baadhi ya viongozi wetu wanavyodanganywa na wasomi wetu kwa kuandikiwa michanganuo mirefuuu na yenye michoro ya kisomi ambayo baadhi ya viongozi wetu, kama walivyo wananchi wengi hapendi kusoma.

Ushahidi wa hili uko wazi, tunawaona wawakilishi wetu karibu kila ngazi wakishikwa na kigugumizi kubeba makabrasha yao ili kujisomea kwa ajili ya kujadili mada. Wao wanachofanya ni kuyaacha katika anwani zao ‘yakiozeana’ ama kuyapeleka nyumbani ambako ‘hutupwa’ kwenye kabati ya vitabu. Nani ajisumbue kusoma bwana!

Watanzania ni mashahidi kuhusu namna baadhi ya wasomi wetu wanavyotumia fursa walizopata kutapeli na kufanya ubadhirifu wanapokabidhiwa ofisi za umma, hawana uchungu na maendeleo ya umma wanaoutumikia, bali wanajali zaidi matumbo yao na yale wanayosaidia kuyajaza asubuhi, mchana na usiku.

Hivi ni lini wasomi wetu wote watakuwa chachu ya kuleta maendeleo na kuibua chagamoto zenye mwelekeo wa kujenga na kukuza uchumi endelevu ili kila Mtanzania aonje neema ya kuwa na rasilimali kibao? Bado tuna kazi kubwa ya kujenga utaifa kwanza.

Sina haja ya kutaja miradi ambayo wasomi wetu tunaowaamini wametungiza ‘mkenge’ wanapokwenda kusaini mikataba na kupokea ‘teni pasenti’, huku wakijua dhambi yao hiyo ni kuwaweka wananchi rehani. Hawa hawatufai kabisa.

Nina imani kwamba wasomi wa sampuli hiyo, wasiokuwa na utaifa hawawezi kamwe kutumika ‘kuiba’ ujuzi kutoka nchi nyingine na kuuleta Tanzania kwa manufaa ya umma.

Ipo habari ya kweli kuhusu wasomi wa nchi za Asia; hasa China na India ambao wamekuwa wakiitumika sana kuiba ujuzi kutoka nchi nyingine na kuutumia kwa manufaa ya umma. Hivi ndivyo hata wasomi wetu wanavyopaswa kuwa. Hivi sisi tunashindwa nini. Hapa Kona Yangu haiwafundishi wizi, bali inatoa chagamoto kwa wasomi kujifunza mengi kutoka ndani na nje kwa neema ya watu wetu.

Wasomi wetu wanaotumia mwanya wa ujuvi wao kutuibia ama kuhujumu uchumi hawana tofauti na mawakili wa shetani ambao muda wote wanafikiri kuwanyonya damu wana wa Adamu.

Thursday, September 07, 2006

Kutodhibiti fedha hizi, kauli ya Kikwete itakuwa ndoto

MIONGONI mwa falsafa ambazo zinanigusa mno nafsi yangu ni msimamo wa Rais Jakaya Kikwete kuhusu suala zima la ukuaji wa uchumi.

Rais Kikwete amekuwa akisisitiza kuwa ukuaji wa uchumi unaoelezwa kwa wananchi na ama wataalamu wa uchumi au viongozi wa siasa, kwamba uchumi umekua huku hali za wananchi zikiwa duni haiwezi kuwasaidia.

Kiongozi huyo wa nchi ambaye nyota yake ya kukubalika inazidi kung’ara kwa rika zote na kwa watu wa kada mbalimbali, ana maana kuwa takwimu zilizoko katika karatasi zikionyesha kukua kwa uchumi ni ‘hesabu’ ambazo hazieleweki kamwe kwa mwenye njaa.

Idadi kubwa ya Watanzania ni watu masikini ambao hawawezi hata kuhimili idadi ya kawaida ya mlo wao kwa siku moja.

Ukweli ni kwamba Watanzania wengi hawana njia za kuwahakikishia wanapata chakula cha kutosha na chenye ukamili wake kwa ajili ya mahitaji ya mwili. Mwili huhitaji vyakula vya kujenga, kulinda na ‘kuunakshi’ ili uvutie.

Kutokuwepo kwa ‘msosi’ wao wa uhakika kunasababishwa na mambo mengi, makubwa yakiwa ni rushwa, kutotendewa haki, ubadhirifu wa baadhi ya watendaji wa umma na hujuma za kila aina zinazofanywa ili kuwanufaisha wachache katika jamii.

Juhudi za Rais Kikwete kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anafaidi keki ya rasilimali zetu na uhuru uliopatikana kwa ‘mbinde’ zinaonekana na dhamira yake iko wazi.

Ni dhamira hiyo inayowapa moyo zaidi wa kuwepo kwa neema kwa kila mmoja wetu, ingawa bado ipo kazi ambayo inahitaji pia ushirikishwaji wa wananchi wenyewe katika kuupiga vita umasikini, ambao ulionekana kuwa chanda na pete miaka mingi iliyopita baada ya 1986.

Hata hivyo, upo mwanya ambao hakuna anauyeuzungumzia kuwa ni kikwazo katika kuwakomboa Watanzania na ‘njaa’ inayowakabili.

Njaa ninayoizungumzia hapa ni pamoja ukosefu wa makazi bora, kuzungukwa na magonjwa kibao ya kuambukiza na zaidi sana njaa ya tumbo, ambayo kimsingi ndiyo ufunguo unaozungumzwa na Rais Kikwete.

Mwanya huo ni kuwepo kwa ‘njia nyeupe’ kwa baadhi ya wafanyabiashara kupeleka fedha za kigeni nje ya mipaka ya nchi yetu bila kuulizwa na yeyote.

Hivi sasa kila mfanyabiashara wa fedha; awe Mtanzania wa kuzaliwa, kuomba au hata kudanganya, anao uwezo wa kusafirisha kiasi chochote cha fedha bila kupitia Benki Kuu au katika taasisi zinazoshughulika na masuala ya uchumi.

Haihitaji kuwa na karatasi kutoka chuo chochote kutambua kuwepo hilo na kuthibitishwa na jinsi dola ya Marekani, paundi ya Uingereza inavyopanda kila uchao dhidi ya fedha yetu, ambayo baadhi ya watu wasiokuwa na utaifa wanaziita za madafu. Sina uhakika wanayaangua wapi hayo madafu!

Kuondoka kwa kiasi kikubwa cha fedha ndiko kunasababisha mfumuko wa bei kwa kiasi kikubwa huku wahusika wakifaidi na ‘walalahoi’ ambao ndiyo wanunuzi wakubwa wakikamuliwa hadi tone la mwisho.

Hivi sasa dola moja ya Marekani ni sawa na sh. 1,335 na kwamba kesho au Jumamosi kiasi hicho kitakuwa kimeongezeka kwa asilimia 10 au zaidi. Inatisha sana hali hii.

Nguvu ya soko la dunia mara zote imekuwa ikipimwa kwa kuzingatia fedha ya Marekani, hivyo shilingi yetu zinapokuwa nyingi zaidi kwa dola moja, uchumi wetu unashuka kwa njia moja hata kama itaelezwa kinyume chake.

Zipo nchi ambapo kupata dola moja ya Marekani lazima muhusika atembee kweli kweli kutoka Benki Kuu hadi taasisi zinazohusika, ambako atapatiwa karatasi lukuki kumuhalalisha kuwa anapaswa kupata na kutumia fedha hizo.

Lakini hapa kwetu kila kitu ni bwerere…na ruksa. Ukitaka dola za Marekani nenda tu mtaa wowote, hata kama ni dampo kule Tabata, utapata tu. Hakuna haja ya kuuliza benki ziko wapi. Kwa nini ujisumbue bwana! Ya nini! Ndivyo tulivyo.

Inaweza kabisa kuelezwa kwamba KONA YANGU inahitaji kuwepo kwa urasimu uliokuwepo miaka mingi iliyopita. Hapana hiyo siyo nia yangu.

Lakini ieleweke kuwa bila udhibiti wa fedha hizo za kigeni tutakuwa tukitwanga maji kwenye kinu, na kwamba kauli za viongozi wetu zinaweza kuwa zile zile zilizozoeleka masikioni mwetu.

Hakuna maendeleo bila udhibiti wa mambo kadha wa kadha ikiwemo rushwa na dhambi nyingine, ambazo nimekuwa nikizipigia kelele kila ninapopata nafasi ndogo katika ukurasa huu kueleza.

Ni vyema sasa serikali yetu ikabuni mbinu za kudhibiti usafirishwaji wa fedha za kigeni zinazopatikana hapa nchini, ili kulinda nguvu ya shilingi yetu, hivyo kuimarisha uchumi ambao utatuhakikishia maisha bora kwa kila Mtanzania.

Inawezekana.

Wednesday, September 06, 2006

Salamu kibao kutoka Namibia

KAMA nakumbuka vyema, sijawahi kuishi katika mazingira yenye baridi kali tangu kuzaliwa kwangu, lakini hiyo haina maana kwamba siwezi kuishi mazingira ya namna hiyo. Naweza.

Hilo nimelithibitisha karibuni baada ya kuishi katika miji mitatu yenye baridi kali nchini Namibia ambako nilidumu kwa miezi miwili na ushei.

Niliishi Windhoek, mji mkuu wa nchi hiyo na baadaye kwenda kutoa tongotongo kwenye mji wa kitalii, kama wanavyoita wao wa Swakopmund.

Kana kwamba haitoshi, uroho wa macho yangu tena ukashawishika kupata shibe ya mji mwingine wa Walvis Bay, ambao ni maarufu sana kwa uvuvi na usindikaji wa samaki.

Katika miji hiyo sikwenda kutalii tu kama ambavyo wengi wanaweza kudhani, bali nilikwenda ‘kupiga’ kitabu kutoka upande mwingine wa bara letu.

Huko bwana kuna baridi siyo mchezo. Muda wote ilikuwa ni mimi na makoti, kofia na soksi za vidole vya mkononi. Hakukuwa na ubishi wa kuvaa vifaa hivyo. Ilikuwa ni lazima ili kwenda na usawa wa huko, viginevyo ningeweza kurejeshwa mapema kwa ubishi.

Miezi miwili kumbe mingi. Nilizoea mno kuwa na watu wa huko. Nikajifunza baadhi ya tabia zao njema na nilizoziona mbaya zikusumbuka nazo.

Nikajifunza maneno mawili matatu; kubwa na la awali likiwa ni Eewa- hili ni neno lenye maana karibu sawa na Safi. Ni neno ambalo hutolewa baada ya mwenyeji kutoa salamu.

Nilipokuwa nikisema –eewaa, wenyeji wote, bila kujali kama ni Waherero, Wanama au Wadamara, waliniona kuwa ni mwenzao, pamoja na kwamba sikuwa nikienelea lolote baada ya hapo.

Mbali na kujifunza neno hilo, nimejifunza tabia nyingi nzuri kutoka kwa Wanamibia ambazo nimeamua kuzitoa kwa wasomaji wangu ikiwa ni salamu nilizobeba kutoka maeneo hayo.

Salamu zingine ni usafi. Napenda kuwashirikisha wasomaji wangu kwa salamu hii ili iwe chachu ya kuhimizana kujali mazingira ya usafi kuanzia mwili, majmbani kwetu, barabarani na hata katika vyombo vya usafiri tunavyotumia.

Jamaa wa huko bwana ni wasafi. Wamefundwa kuwa wasafi. Ukiwa katika miji ya Namibia, mijini na vijijini huwezi kuona karatasi ikizagaa hovyo.

Huwezi kukuta ‘jitu’ likikojoa hovyo. Hakuna anayeonekaa akitema mate hovyo na hakuna anayeonekana akitupa taka hata kama ni ndogo kiasi gani.

Pamoja na kwamba kuna sheria kali za mtu anayepatikana akitupa taka, lakini kitu kikubwa ambacho nimejifunza ni kwamba watu wa huko wamefundwa kuchukia uchafu. Kufundwa huko kunaanzia utotoni nyumbani, baadaye shuleni na kuendelea hivyo.

Hapa kwetu hali ni tofauti kabisa, ipo ‘mibaba’ inayoamua tu kutupa taka hovyo majumbani kwao. Inatupa vichungi vya sigara mezani, sakafuni chumbani na hata kwenye vyombo vya usafiri. Haina haibu!

Kana kwamba hiyo haitoshi, kukojoa hadharani ni jambo ambalo linaonekana kuwa tabia miongoni mwetu. Mtu anaamua kujisaidia haja ndogo bila kujali kwamba anachafua mazingira. Zaidi ya hapo anaweza kuamua kuweka ile kubwa kabisa bila aibu.

Unashindwa kuelewa inakuwaje mtu na akili zake anafanya vitendo vya namna hivyo ambavyo hata baadhi ya hayawani hawawezi kuvifanya? Je ni nani wa kulaumiwa katika hili.

Iwapo Wanamibia wanaweza kuwa wasafi na wenye kujali mazingira yao, nini kinashindikana kwa Watanzania kuwa wasafi kuanzia makwao na hata barabarani? Iweje mtu ashindwe kutupa taka panapohusika? Tujirekebishe jamani.

Nimewalaumu sana watu kwa kushindwa kuwa wasafi, lakini pia uongozi wa jiji la Dar es Salaam nao naulaumu kwa kushindwa kuweka vifaa vya kutosha vya kutupia taka au kuwa na vyoo vya umma maeneo mengi yanayopitiwa na watu. Hii inaweza kuwa sababu nyingine inayofanya uchafu kuzagaa kila mahali.

Salamu nyingine nzuri ambayo nimeipokea huko ni unywaji wetu wa pombe, au bia kama ambavyo baadhi ya watu hupenda kuiita. Idadi kubwa ya watu wa Namibia, hasa wafanyakazi hupenda kunywa bia zao kuanzia saa 11 jioni.

Pamoja na kwamba wapo ‘wanaokamata’ kinywaji chao tangu mapema, lakini ni wachache ikilinganishwa na wengi wenye ustaarabu.

Zaidi ya hapo, siku za kazi wanywaji wanakuwa wachache mno, huku idadi kubwa ikijitokeza kila Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kunywa bia kama ‘samaki’.

Kila Ijumaa baa zote zinajaa, huku sauti za juu zikitawala kutoka kila sehemu inayouza kimiminika chenye rangi ya dhahabu ambacho kinaonekana kufurahiwa na zaidi ya asilimia 80 ya Wanamibia kama ilivyo kwa Watanzania.

Watanzania wanachoweza kujifunza kutokana na salamu hii ni kuachana na ulevi wa muda wote, hasa wakati wa kazi na muda ambao wanapaswa kuwa nyumbani na familia zao wakisaidia ulezi wa watoto.

Idadi kubwa ya Watanzania, hasa wa mijini hivi sasa wanapenda mno ‘kusalimia’ baa kila wanapotoka kazini kwa kisngizio cha kusubiri msongamano wa magari barabarani kupugua. Hii siyo tabia nzuri hata kidogo.

Ni vyema tukajifunza kunywa kinywaji chenye kileo kila Ijumaa, Jumamosi na siku zingine kujiweka tayari kwa kazi za ujenzi wa taifa siku inayofuata.

Nimeona vyema kuanza na salamu hizi huku zingine zikiendelea kuchapishwa katika safu hii kama nilivyozipokea kutoka Namibia.

Tuko pamoja sasa.

Wednesday, June 07, 2006

Unafiki, kujichekesha hakuwezi kuleta neema TZ

Nani ataweza kuwavusha wana wa Tanzania hadi kufika nchi ya Kaanani?

Hilo ni swali ambalo limekuwa likisikika kutoka kwa wananchi ambao wana uchungu mkubwa na ustawi wa maisha yao na ya wengine.

Siyo juzi, siyo mwaka jana, wala mwaka huu, swali limekuwa likiendelea kuulizwa na idadi kubwa ya Watanzania na kukosa jibu lenye mwelekeo sahihi.

Wapo waliosema jibu sahihi ni kupatikana kwa kiongozi mzuri, anayependwa na wananchi, anayechapa kazi vyema, anayejituma, mwenye uchungu na maendeleo ya nchi na watu wake.

Kimsingi swali hilo liliulizwa wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere, likaulizwa wakati wa Alhaj Ali Hassan Mwinyi, likahojiwa wakati wa uongozi wa Benjamin Mkapa na sasa linaendelea kuulizwa wakati huu wa uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Wote wanaohoji hivyo wanategemea mazingira ya wakati husika, huku wakijenga matumaini kila uongozi unapokaribia kufika mwisho kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

Ni matumaini hayo yamekuwa yakitoa nafasi ya subira na kujenga ukuta mgumu wenye mtazamo chanya kwa kila uongozi mpya unapoingia madarakani.

Ni uvumilivu huo huo umekuwa sura ya Watanzania kiasi cha kupewa sifa ya subira na majirani zetu au wageni wanaopata fursa ya kutembelea ardhi ya nchi yetu au kusoma historia na habari zake.

Kuingia madarakani kwa Rais Kikwete kulidhihirisha imani kubwa ya wananchi kwake, huku idadi kubwa ya watu, bila kujali itikadi ya siasa na hali ya maisha, wakimpa ushirikiano katika kuendeleza Tanzania.

Imani ya Watanzania kwa Rais Kikwete inajikita katika msingi wa maisha yake ya shule na uongozi ndani ya Chama na serikali tangu akiwa kijana.

Baada ya kumpa kura Rais Kikwete, idadi kubwa ya Watanzania waliompa kura na wale walioamua kuwapa wagombea wengine kwa maana ya kukuza demokrasia, wameendelea kumuunga mkono katika utekelezaji wa kazi zake.

Wengi wanaamini kwamba kiongozi aliyekuwa akisubiriwa Tanzania sasa amepatikana na hali hiyo imekuwa wazi kila anapopata fursa ya kuonekana kwao; iwe moja kwa moja au kupitia vyombo vya habari.

Hata hivyo, pamoja na kuwepo mazingira mazuri sasa ya uchumi unaokua, bado imani pekee haitoshi ikiwa wananchi hao hao watabweteka na kukaa bila kujituma katika kufanya kazi zao kwa lengo la kuimarisha uchumi wa familia na nchi kwa jumla.

Kumsifia tu Rais Kikwete kwa kila analofanya bila kujituma kufanya kazi hakusaidii jitihada zake za kuona kwamba kila Mtanzania, angalau anawekewa mazingira mazuri ya kumfanya aweze kula milo miwili au mitatu kwa siku.

Wito huo wa kujituma hauwaangukii tu wananchi wa kawaida, bali ni mnyororo unaotakiwa pia kuwafunga viongozi wanaomsaidia rais kuhakikisha malengo ya kuinusuru Tanzania na umasikini yanafikiwa.

Viongozi hao, kuanzia ngazi za chini, wanapaswa kuvua ngozi ya unafiki na kujichekesha kila wanapomuona Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Sheni na Waziri Mkuu Edward Lowassa na kuwatumikia wananchi kwani lengo la kuwepo kwao ni kusaidiana nao kuondoa kero au kzimaliza kabisa.

Kiongozi yeyote mnafiki hujitanabaisha kwa matendo yake na wananchi wanamjua hata kama atajichekesha na kuosha mikono yake mbele ya viongozi wakuu wa nchi.

Hali ya namna hiyo ilijitokeza mno wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka jana ambapo wananchi walionyesha kuanza kuwachoka viongozi wa namna hiyo kwa kuwaumbua mbele ya Rais Kikwete baada ya kuwazomea kila waliposimama kuomba kura.

Vyovyote iwavyo, Kona Yangu inaamini kwamba zomeazomea ya namna hiyo ilidhihirisha jinsi wananchi wanavyochukia unafiki, uroho na uchafu mwingine unaofanywa na viongozi; wawe madarakani au wamestaafu.

Viongozi wanafiki, hata kama wamejificha wamo katika kada mbalimbali za uongozi ikiwemo wasaidizi wa karibu wa viongozi wetu.

Viongozi hao wanapaswa kujirekebisha sasa na kutoa mchango wao kwa viongozi wanaowachagua kushika nafasi mbalimbali ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu ambalo kwa sasa bado liko nyuma.

Ikiwa kiongozi anayejijua atauvua unafiki wake na kutumika ipasavyo kwa wananchi, hakika ni kwamba maendeleo yanayotarajiwa yatafikiwa na atakuwa amemsaidia mno Rais Kikwete badala ya kuwa mchekaji na mpiga kofi kwa kila kinachoelezwa na viongozi wa juu wa serikali au Chama.

Dalili za kiongozi mnafiki ziko wazi; kubwa ikiwa ni kutotimiza anachoahidi, kutoamini anachokizungumza, dharau, kuwa msiri kwa vitu vya wazi na kuogopa kuelezwa ukweli.

Viongozi wa namna hiyo wamo kila mahali hata katika serikali za kichungaji, kipapa na hata kifalme na walikuwepo wakati wa utawala wa Yesu.

Ni wakati muafaka sasa kiongozi wa namna hiyo kujiondoa ikiwa atashindwa kujishuku na kujirekebisha mwenyewe.

Endapo atashindwa kujirekebisha mwenyewe na kusoma alama za nyakati ni vyema akaondolewa kuliko kuendelea kumlea na kuhalalisha maendeleo duni huku akiwachelewesha kufaidi neema na matunda ya Uhuru wa Tanzania.

Friday, May 12, 2006

Wachezji wavuje jasho, wafaidi viongozi!!!

KAWAIDA ni kwamba Watanzania kama walivyo waanchi kutoka mataifa mengine ni wapenzi wakubwa wa michezo mbalimbali, huku kila mmoja akiwa mpenzi wa mchezo anapenda.

Miaka mingi, hata kabla ya kuingia kwa wakoloni, Tanganyika (wakati huo kabla ya kuungana na Zanzibar) ilikuwa na michezo yake lukuki. Kimsingi, watu walijumuika katika michezo hiyo na kuifurahia.

Miongoni mwa michezo hiyo ni pamoja na bao, mpira wa miguu, mchezo wa ng’ombe na aina nyingine ya michezo ambayo ilikuwepo wakati huo.

Katika kuhakikisha kwamba michezo hiyo inaendelea na kuwepo kwa heshima, zilitengenezwa taratibu za kufuata ili kumpata mshndi halali na pengine utaratibu wa kutolewa kwa zawadi kwa washindi na kuwapa moyo wanaoshindwa ili baadaye wawe washindani wa kweli na hata kupata ushindi.

Ni katika kuwepo kwa taratibu hizo, jamii ilikubaliana kuwepo kwa viongozi ambao wanasimamia taratibu na kanuni za michezo hiyo ili iwe endelevu zaidi.

Kimsingi, zamani michezo ilikuwa na lengo moja tu; kwamba ni sehemu ya burudani ya kuliwaza akili na kujenga mwili na mara nyingi ilifanyika wakati wa jioni, hasa baada ya kazi na baada ya mavuno.

Hata hivyo, hali sasa imebadilika mno na michezo siyo tu kwamba ni burudani na kuupa mwili mazoezi, bali ni eneo muhimu mno la kukuza ajira, hasa kwa vijana wetu.

Kama ilivyokuwa zamani, michezo hiyo inaendeshwa kwa taratibu na kanuni mbalimbali ambazo zinaifanya kuwa endelevu zaidi na kwamba michezo mingi, hata iliyokuwepo zamani imeboreshwa kwa maana ya kuweka ‘usasa’ zaidi katika kuiendesha.

Miongoni mwa usasa huo ni pamoja na kuwepo kwa taratibu za kiofisi zaidi katika kuisimamia michezo hiyo. Mpira wa miguu una chama chake kinachosimamia taratibu za kupatikana kwa mshindi. Mpira wa meza unazo taratibu zake na mpira wa kikapu unazo taratibu na kanuni zake. Uhakika ni kwamba kila mchezo sasa uliopo unazo taratibu zake za kiofisi katika kuongoza na kusimamia taratibu.

Nia na lengo la kuanzisha taratibu za kiofisi kusimamia michezo hiyo ni kuhakikisha kwamba taratibu na shughuli za michezo husika zinasimamia na kufuatwa na wahusika bila kuwepo kwa uvunjaji wa sheria na kanuni zilizopo.

Hata hivyo, inavyoonekana sasa watu wanaopewa kusimamia taratibu na kanuni za michezo wamegeuka kuwa wanyonyaji wakubwa wa wahusika wakuu ambao ni wachezaji wenyewe.

Ndiyo. Ni wanyonyaji wakubwa wa wachezaji kwa kuwa wamejenga wigo mpana wa ubinafsi ambao unawahakikishia wao mapat makubwa ambayo yanatumika kujaza matumbo yao na kuwaneemesha waaowategemea.

Hao ninaowazungumzia hapa ni viongozi wa juu na wasimamizi wa timu ambao, bila aibu wanadiriki hata kuua vipaji vya vijana wetu ili wao na watoto wao wafaidi jasho la watu wengine wanaoingia uwanjani kuumia.

Vijana wetu wanaumia sana uwanjani wanapokuwa wakicheza, lakini wanafaidi kidogo mno jasho lao, huku wanaojiita mameneja wa timu, viongozi wa timu, makomandoo, marafiki wa kila aina wakifaidi peke yao.

Mbali na hao viongozi na wa timu, vyama vya michezo navyo badala ya kuwepo kutetea maslahi ya wachezaji na timu zao, vimegeuka kuwa wanyonyaji wakubwa wa nguvu za vijana wanaoingia uwanjani kuumiza misuli yao.

Monday, May 01, 2006

Hivi nani mfanyakazi bora

Jamani, nimekuwa nikiwaza na kuwazua; Ni nani mfanyakazi bora katika ofisi zetu Tanzania?
Nauliza hivi kwa kuwa kila ifikapo tarehe kama ya leo kila mwaka, ofisi huwa zinahaha kutangaza wafanyakazi bora. Sijui wanatumia vigezo vipi.
Muda wote wachapakazi ndo wanakosa nafasi hizo na wanaopata ni wale wanaopendwa na wanaowateua; iwe manajimenti, ofisa mtendaji mkuu na wote wanaofanana na hao.
Sasa mimi nasema hakuna cha mfanyakazi bora wala nini. Wote n i watumishi tu na mtindo huo wa kuwepo wafanyakazi bora unadumaza utendaji wa kazi wa watu wengine na ndiyo maana nchi zetu haziendelei.
Nimemaliza

Tuesday, April 25, 2006

Fimbo ya kila mtu kwa Nche Nkampa

Kumbe hatukuwa tukijua kwamba asiyekuwepo na lake halipo.
Sasa nimeamini.
Jamani hebu tufike mahali tuone kwamba mambo sasa yako hadharani baada ya kuwa yamefichwa kwa muda mrefu sana.
Nimeamini kuwa Watanzania tu waoga mno wa kueleza ukweli na waoga wa wakubwa, hasa wanapokuwa madarakani.
Ni kwamba wengi wetu hatuwezi kueleza kuwa mfalme yuko uchi hata kama hana hata chupi ya kufunika tupu zake zote.
Iweje leo ndio kunaibuka kila kitu kinachoelezwa kuwa kibaya cha Mzee Mkapa wakati hayuko madarakani.
Weweee acha tu! Kila mtu sasa eti anamuona Mkapa kama mtu aliyekuwa akisaidia mnoi kukuza umasikini wa Mtanzania.
Jamani hivi tulikuwa wapi wakati yeye akiwa madarakani. Je tulikuwa tukumuogopa kwamba nidikteta au namna gani.
Iweje leo hayupo kwenye kiti kikuu na kwenye nyumba yenye vinono inayovuja maziwa na asali ndiyo kuibuke tuhuma kibao dhidi yake. jamani tulikuwa wapi.
Leo ndiyo kila mtu anaibuka kuwa almasi zetu zote zilikuwa zikipelekwanje na hazikutusaidia kabisa wananchi wa kawaida.
Kwa hali hiyo naanza kuogopa sifa tunazowapa viongozi wetu wanapokuwa madarakani...huenda nyingi ni za mgongo wa chuipa.
Tubadilike sasa, kila awe mkweli kwa nafsi yake, kama kiongozi amekosea na yuko uchi tumweleze na tuache kujipendekeza wala kuwa wanafiki.
Tungekuwa wema kabisa, hata kama ingegharimu damu yetu, kama kila mmoja angekuwa anamnyooshea kidole Nche Mkapa kwa yake yanayodaiwa kuwa mabaya yake badala ya kusubiri atoke madarakani ndiyo kila mtu ashike kiboko kumchapa.
Muda ndiye mwamuzi bora.
Tusubiri...labda tutaujua ukweli

Tuesday, April 11, 2006

Nilikuwepo Azimio la Dom

Jamani,
Yaani bila aibu mnaonekana kunitenga. Ni kwei sikuwepo kwa muda, lakini isiwe sababu ya kunitosa kiasi hicho.
Kwanza naomba mkumbuke kwamba niliunga mkono azimio la Dodoma kwa nguvu zote na miongoni mwa washiriki nilikuwepo.
Tatizo ni kwamba picha haikuweza kupata taswira yangu kutokana na kwamba sikuonekana kiwiliwili hapo kweye mkutano huo uliojaa Coca na Fanta.
Jamani nilikuwepo tele, nafsi yangu ilijaa tele hapo. Mbona wengine wanakuwepo kinafsi na mnawakubali, iweje mimi mnione kuwa ni dhalili kwa hili.
Nakubaliana nanyi jamani mia kwa mia.
Tuko pamoja na leo nawatakia maulid njema. Nitakuwa Movenpick nikifurahia sikukuu hiyo mahsuss kwetu waungwana.
Tuko pamoja

Monday, April 10, 2006

Fursa zijulikane sasa kwa wote


HAKIKA ni kwamba Watanzania wengi bado wanaogelea katika dimbwi la ufukara, huku matatizo makubwa yenye msingi wa umasikini yakiendelea kuwakabili kila kukicha.

Sababu za maisha ya Watanzania kung’ang’aniwa na ufukara ni nyingi na kila moja inaweza kuelezwa na kufafanuliwa kwa mapana na marefu yake.

Ni kutokana na ufukara wa wananchi wetu, maisha yao yamekuwa ya kubahatisha mno, kuanzia kutokuwepo kwa uhakika wa tumbo kujazwa chakula na uhakika wa mwili kutoshambuliwa na magonjwa, au hata tiba ya uhakika wanapokuwa wameugua.

Katika vita dhidi ya ujinga, kwa kiasi fulani, ushindi unaonekana kuwa upande wetu kutokana na kuwepo kwa silaha na dhamira madhubuti kuamua ushindi.

Awamu zote tatu za uongozi wa nchi yetu, kuanzia kwa Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa zimejitahidi mno kuwaondolea ufukara na umasikini wananchi; kila awamu kwa nafasi ya mafanikio ambayo inaonekana.

Wakati akiwa madarakani, Mwalimu Nyerere (sasa marehemu) alifanikisha mno kujenga umoja wa kitaifa, ambapo aliimarisha uhusiano wa wananchi bila kujali kabila wala maeneo wanakotoka. Imani ya Mwalimu Nyerere ilikuwa kwamba hakuna maendeleo na wala hakuna ushindi dhidi ya umasikini endapo hakuna umoja. Kwa hilo alifanikiwa.

Uongozi wa Mzee Mwinyi ulifungua milango ya kuwepo kwa demokrasia, mfumo ambao leo unaendelea kujenga misingi ya maendeleo makubwa ya kiuchumi yanayoonekana sasa. Mzee Mwinyi aliamini kwamba bila kukua kwa demokrasia, hata kama uchumi utakua, bado utakuwa na shaka ya kudumu kutokana na kutokuwepo kwa uhuru wa kisiasa. Na pia Mzee Mwinyi aliiondoa serikali katika mifumo wa biashara na kujikita zaidi katika kushughulikia kero za wananchi wake.

Mzee Mkapa alikuja kuimarisha zaidi uchumi kwa maana ya kujenga utamaduni wa wananchi kulipa kodi zaidi ili iwe rahisi kuimarisha na hata kuwa na miundombinu imara. Kiongozi huyo anaamini kwamba kuwepo kwa miundombinu imara ni kuchonga barabara ya kufikia mafanikio ya kiuchumi kwa haraka zaidi.

Uongozi wa sasa chini ya Rais Jakaya Kikwete (JK), ingawa bado ni mchanga katika kuwatumikia wananchi, ishara zinaonyesha kwamba imetanua mno ‘mbawa’ zake kuyashughulikia na hatimaye kutoa ufumbuzi wa sehemu ya ufukara na umasikini kwa Watanzania.

Rais Kikwete katika kuhakikisha kwamba analitumikia vyema taifa, kwa maana ya kushirikiana na wananchi kupunguza umasikini, amekuwa na imani kwamba Tanzania yenye neema inawezekana.

Imani hiyo ya Rais Kikwete ndiyo msimamo wa Watanzania wote. Kila mmoja anaamini kuwa Tanzania yenye neema inawezekana kabisa bila kusubiri mjomba ama shangazi kutoka ughaibuni.

Kama walivyo wananchi, Kona Yangu inaamini kwamba neema hiyo kwa kila mmoja wetu inawezekana kabisa, isipokuwa wananchi wanatakiwa kuelezwa na kuzifahamu fursa zilizopo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache mno zilizopewa fursa na Mwenyezi Mungu ambazo zinaweza kutatua ufukara wao, ikiwa watatambua kuwepo kwake, huku wakipewa msukumo na viongozi wanaokuwa madarakani kwa wakati husika.

Inawezekana kabisa kwamba sasa wakati husika kwa Watanzania kuzitambua fursa hizo umefika, na kinachopaswa kufanywa na viongozi ni kuziweka wazi.

Fursa hizo ni nyingi, lakini endapo hazitatambulishwa kwa wananchi, wasiwasi wa Kona Yangu ni kwamba zitaendelea kuwanufaisha wachache, huku wananchi wengi wakiendelea kuteseka.

Ieleweke kwamba kumekuwepo na mipango mingi ya kuwapigania Watanzania ili waondokane na umasikini, lakini bado haijaweza kutoa msukumo wa dhati wa kuondoa ufukara kwa Watanzania.

Kama zilivyo sababu za kuwepo kwa ufukara huo, sababu za kushindwa kwa mipango na mikakati ya kuwaepusha wananchi na umasikini, zimejikita mno katika dhana ya ubinafsi wa wananchi wachache wanaobahatika kuwa waongozaji. Hawa badala ya kuwaonyesha wenzao wengi njia za kuondokana na umasikini, wao wanajionyesha wenyewe na wake na watoto wao.

Ndiyo maana basi, wapo Watanzania wachahe wenye utajiri wa kutisha, huku wenzao wakiendelea kusumbuliwa na mlo wa siku moja na hata kushindwa kutibu watoto wao kwa magonjwa yanayotibika; msingi wa shida zote hizo ni umasikini.

Hakika ni kwamba hao wenye utajiri mkubwa ndio wenye kutambua na kuielewa mikakati ya kupambana na umasikini na kutumia fursa hizo wenyewe bila kuwaeleza wengine.

Ni vyema basi, serikali ya sasa ikaweka msukumo mkubwa katika kuwapatia wananchi elimu ya namna ya kutumia fursa zilizopo za mikakati na mipango kamambe ya kupambana na ufukara (sema umasikini ukitaka).

Ikiwa hilo litafanyika, maisha ya kila Mtanzania yataweza kabisa kuwa bora na kuifanya neema kusambaa kwa kila mmoja.

Siku 100 za Kikwete Ikulu

MIAKA mingi iliyopita, watendaji wa serikali katika nafasi mbalimbali walionekana kujisahau mno katika suala zima la kuwatumikia wananchi.
Watendaji hao walichojua ni kwenda ofisini kusaini vitabu kwamba wamefika na kutokomea kwenda kwenye shughuli zao zingine kinyume na utaratibu ambao unawataka kufanya kazi kwa saa nane.
Mazoea haya siyo kwamba yalikuwa maeneo ya vijijini pekee, bali yalishamiri mno maeneo ya mijini na kuwa sehemu ya maisha ya wafanyakazi, hasa wa serikali.
Wapo baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakionekana ofisini wakati wa kupokea ujira wao wa mwezi au madai mengine na siyo vinginevyo.
Tabia hii ilichangia mno kudumaza ukuaji wa uchumi na kujenga ustawi wa jamii bora, kwani kila eneo la kupata huduma halikuwa na watendaji kwa muda muafaka.
Zaidi ya hapo, wafanyakazi wengi wa serikali walijenga tabia ya kuwa waongo wanapotoa taarifa zao za maendeleo kwa viongozi wanaotokea kutembelea maeneo yao.
Uongo huo ulizidi mno walipokuwa wakitoa taarifa hizo kwa wananchi. Kutoa taarifa za uongo kulisababishwa na tabia yao ya kuwa wazembe wa kazi.
Hata hivyo, hali hiyo sasa inaonekana kupotea kwa kasi ya kutisha. Kwa muda wa siku 100 tu za Rais Jakaya Kikwete madarakani, sasa hali imebadilika mno.
Kila mfanyakazi wa serikali katika eneo lake anajitahidi kuwahi kazini, kufanya kazi kwa kujituma na kutoa huduma kwa wananchi wahitaji.
Ule utaratibu wa kuwaona wananchi kuwa ni dhalili wanapofika katika ofisi za serikali kuhitaji huduma, sasa umepotea kama umande jua linapochomoza.
Ama hakika wananchi wengi, ukiondoa wenye vyeo na fedha, walionekana kutokuwa na haki ya kupata huduma kutoka kwa watendaji wa serikali.
Sasa hali inabadilika, watendaji wa serikali, hasa wale wanaotoa huduma za moja kwa moja kwa wananchi wanaonekana kujali kazi zao na wanaachana na mazoea.
Hali hiyo imewezekana kutokana na ukweli kwamba serikali ya sasa haitaki kudanganywa na kwamba haina mchezo kwa watendaji wabovu wala wababaishaji ambao hawatimizi wajibu wao kwa wananchi.
Sasa ni kwamba kila mtumishi wa serikali anakuwa msimamizi wa mwezake na kuwa waongo wanajirekebisha, kwani walioko madarakani hawataki kudanganywa na hawako radhi kuona wanaongopewa kutokana na ufuatiliaji wa karibu.
Kiongozi yeyote ambaye anafanya kazi na karatasi ofisini tu, ni rahisi mno kuongopewa na watendaji wa chini yake kwani wanakuwa na uhakika kwamba hakuna ‘follow-up’.Utendaji wa sasa wa Rais Kikwete ndiyo unaotoa msukumo wa kila mmoja mkubwa kwa mdogo katika ofisi kusikia mwangwi wa sauti ya Rais Kikwete kila anapotoroka eneo lake la kazi.
Ni mwangwi huo unaomwambia kila anayetoroka kazini kurejea na kuwatumikia wananchi kwa neema ya Tanzania na watu wake ambao bado wana safari ndefu ya ushindi dhidi ya ufukara.
Hongera Rais Kikwete kwa utendaji wako unaoonekana wazi kwamba umejengeka katika dhamira ya kuwatumikia wananchi, hasa wale wenye hali duni.
Kila Mtanzania anakutegemea na kukuombea kwa Mungu Mkuu ili upate siha njema na uwezo maradufu wa kupigania haki, maendeleo na kudumisha amani na utulivu wa Tanzania.
Inawezekana.

Thursday, April 06, 2006

Nilitekwa tena na magaidi

Wapenzi waungwana wangu,
Kwanza niwaombe samahani sana kutokana na kukosa mawasiliano nawe na hivyo kuwanyima mlichokuwa mkikipenda katika gazeti langu tando.
Ni kweli nimepokea malalamiko mengi kutoka kwenu; wapo walioniandikia barua pepe, wapo waliopiga simu na wapo, walioweza, kunifuata ofisini kueleza masikitiko yangu.
Jamani wapenzi, kilichokea ni kwamba nilitekwa kwa muda wa miezi minne na miezi miwili baadaye nliamua kupoumzika ili kutibu machungu ya suluba za kutekwa huko.
Aliyeniteka naweza kabisa kumuita gaidi, ingawa alikuwa na uungwana kidogo wa kunipa ktu kidogo kwa ajili ya neema ya watoto na mke wangu huko nyumbani.
Ninachoweza kueleza ni kwamba, mimi na nyinyo wote tumsamehe tu kwani hakujua alitendalo kwa uhakika.
Sasa najiagiza kwamba, nitakuwa nikiandika kila mara ili tuendelee kupata mawasiliano na kubadilishana mawazo kuhusu nchi yetu na dunia kwa jumla.
Nasema; Yaliyopita si ndwele tungange yajayo.
Pamoja na hayo, nachukua nafasi hii kuwapongeza waandishi wapya wa gazeti tando ambao wameamua kujitosa na kuwa katika familia kubwa na inayoendelea kukua kwa kasi. Jamani nasema karibuni sana.
Nawatakia kile jema na tuwe pamoja sasa na hata milele
Nawapenda

Tuesday, October 11, 2005

Wagombea wangu masikini!

Uchaguzi wa mwaka huu Tanzania kweli umejaa mambo magumu.
Sasa wagombea wameanza kudhihirisha kwamba kampeni siyo lelemama, zinahitaji muda na fedha.
Wengi wameishiwa na wanalia machozi ya damu kwamba wanaonewa na serikali kwa kunyimwa ruzuku za kuendesha kampeni.
Mgombea wa PPT- Maendeleo, mwanamama pekee Anna Senkoro amesema hana kitu hivi sasa na anawaomba wananchi na mashabikiw ake kumchangia petroli awezew kuzunguka angalau maeneo machache ya kuombea kura.
Naye Profesa Shayo akasema uchaguzi huu hauwezi kuwa wa haki maana CCM inazo fedha nyingi za kampeni, lakini wao hawana kitu.
Profesa akasema kwamba anachofanya sasa ni kuzunguka kwenye mabaa anakopendelea kunywa kinywaji chake na anaowakuta hapo ndipo anamwaga sera zake, hataki mchezo na zaidi ya hapo anatumia gari lake analoendesha mwenyewe kuzunguka mitaa ya Dar es Salaa tu na kutangaza sera zake kuwaomba wananchi ridhaa. Huyu hataki mchezo kabisa.
Jamani tusubiri tuone, najua kwa kuw amazingira ya namna hii ya kulalamika yameanza, lazima kuna utayari wa kukataa matokeo kwamba hayatakuwa halali.
Tusubiri tuone

Mrema ashinda tuzo ya usanii!

Nimecheka..nikacheka na nikafurahi kweli kweli.
Bwana kutokana na kucheka huko, na pia kuungwa mkono na jamaa wengine niliokutana nao wakisoma gazeti, nimeamua kumtunukia Mrema shahada na tuzo ya juu ya usanii bora nchini.
Huyo bwana anayewania kuingia Ikulu, majuzi aliniacha hoi. Aliamua kuwapa ukweli wapiga kura wake jamani. Huyu ndiye mtu anayesema ukweli tupu na wengi bado wanamuamini na kumpenda.
Mrema aliamua kubakiza dakika 15 anazopaswa kumaliza hotuba yake kwa wananchi kunadi sera zake ili ashiriki na wapiga kura wake kucheza muziki wa Bongo Fleva.
Mgombea huyo ambaye ni rafiki yangu alisema ni bora abakize muda huo mfupi li aweze kucheza muziki huo wa Bushoke uitwao Mume bwege kwani hawawezi kupata tena muda wa kucheza naye atakapokuwa Ikulu pale Magogoni.
Mrema akawaambia wananchi kwamba wanaobahatika kucheza naye sasa ndiyo wamebahatika na wasiobahatika itakuwa bahati mbaya.
Akashuka jukwaani na kuanza kusakata muziki huo wa kisasa unaopendwa zaidi na vijana.
Mrema bwana...weee acha tu. Akacheza, akakata mauno, akanyonga mabeba na pia kusonta vidole kama wanavyofanya vijana wa kisasa.
Kitu kimoja tu alisaahau, kushusha suruali yake hadi jirani na magoti na kuonyesha chupi yake kama wanavyofanya vijana na kuita mtindo huo kuwa ni kata..nini sijui ( ahh wanajua wao).
Mrema akacheza na kuwaeleza akiingia Ikulu hahana muda tena na zaidi ya hapo wapo walinzi kibao ambao hawatawaruhusu wananchi kucheza naye.
Ehheee bwana eee..akacheza hadi dakika 15 zikaisha na baada ya hapoia akwaaga akaondoka zake akiwa amelowa jasho, kibaragashia chote kililowa mwanangu.
Duuuu Mrema kweli kiboko

Wednesday, September 21, 2005

Nimechanganyikiwa

Nimewasikia. Nimewaona na wengine nimewagusa. Hawa ni wanasiasa wanaojipitisha hivi sasa kwangu na kwa waajiri wao wengine wa mijini na vijijini. Eti sasa ndiyo ninawaona kwamba wananithamini sana na kunipenda. Eti wananiona mali kwa sasa.
Nawashangaa, hawa walikuwa wapi zamani kuwa na tabia njema namna hii ya kunijali na kuniona mimi wa maana. Hivi nina kitu gani sasa hivi zaidi ya zamani. Au jamani nimeota dhahabu kichwani bila kujua, au nina tananite kwapani au nimeficha almasi kwenye unyayo wangu bila kujua.
Naomba waungwana mnieleze niwasikileze watu hawa au niwakimbie. Kama nina madini ambayo wao wanayaona niwasubiri wayatoe tugawane au nikimbie na nibaki nayo hata kama hayanisaidii sana.
Nazungumzia Kura yangu. Nipeni jibu.

Tuesday, August 30, 2005

Maprofesa wauza baa waja juu

Kumbe KONA YANGU imewagusa na kuwapandisha presha baadhi ya maprofesa hao wa kilimo na ufugaji wanaouza bia na ‘mikonyagi’, mmoja kaniandikia akiniita mtu mwenye wivu, kizabinazabina, niliyeshindwa maisha na kwamba niache kuwafuata katika maisha yao.
Anadai kwamba kilimo kimeterekezwa na kila mmoja, tangu viongozi wa vyama na hata walioko serikali, kwamba wanachojua wao ni kuwaeleza wananchi kwmaba kilimo bado ni uti wa mgongo, ilihali ni kinyume cha hivyo.
Bila kujitaja jina anaendelea kufoka, nadhani hata alikuwa akitokwa na povu wakati akitoa yaliyo moyoni mwake, kwamba wao kama wataalamu wameshindwa kupewa umuhimu, hata ushauri wao haufanyiwi kazi.
Anadai kwamba-katika hali ya namna hiyo, wao wafanyeje, kama siyo kutafuta njia mbadala ya kufanya shughuli zingine ambazo wanadhani zinawaingizia kipato kikubwa zaidi, akimaanisha hata kuuza bia.
Sina ugomvi na msomi huyo (sina uhakika kama ni daktari au profesa), hata kama angesema maneno yote ya kejeli, matusi na dharau anayodhani inanifaa kutokana na kuandika nilichoandika. Hakiwezi kufutika na nina furaha kwamba ujumbe umemfikia yeye na wengine wote, siyo wa fani ya kilimo na ufugaji pekee, bali wote wenye dhamana ya kuwa viongozi wetu katika mapambano ya umasikini, lakini wakienenda kinyume na matarajio ya Watanzania.
Hapa nazungumzia wote wanaoterekeza utoaji wa taaluma zao kwa wengine (kama madaktari wa mifugo, uuguzi, waandishi na hata wapishi) na kuwa ‘wanenguaji’ majukwaani. Twaache wanenguaji wawe wanenguaji na wengine kama wanahitaji kufanya hivyo, wafanye kujifurahisha huku wakiendelea na taaluma zao kwa manufaa ya wananchi.
Hivi kama profesa anauza bia hadi usiku wa manane, ni muda gani anaandaa somo la siku inayofuata, ikiwa atakuwa na kipindi ? Hata kama itaelezwa kwamba ana uzoefu wa kutosha, kwamba anaweza kufundisha bila kuhitaji maandalizi kutokana na uzoefu, hivi kweli huyu anaweza kuwa makini ! Sidhani.
Ikiwa hiyo ndiyo tabia yake, je anapata wapi muda wa kusoma na kutafiti mada ama dhana mpya za kisasa katika kuboresha ufundishaji wake na kutoa elimu yenye mazingira ya kisasa ambayo ndiyo inahitajika mno zaidi ya aliyosoma yeye enzi zile za mwaka 47?
Ninachojua ni kwamba msomi mwenye utaifa anapaswa kuwa chachu ya kugundua dhana mpya na kuwapa elimu mpya aliyopata kwa watu wanaomzunguka kwa faida ya wote.
Inashangaza kusikia profesa akitukana, huku akitoa sababu za kijinga kwamba serikali imeterekeza kilimo. Hata kama ni hivyo, ni wapi serikali inamzuia yeye kwa kutumia ujuzi wake kuwa na mashamba ya mfano na kufuga kisasa na kuuza mazao yake kokote anakopenda!
Mbona hivi sasa yapo mazingira mazuri tu ya kumwezesha yeyote kuuza mazao yake anapopenda hata ikiwa nje ya nchi.
Uhakika ni kwamba kama huyo profesa (sijui…) ameweza kufungua eneo la kisasa la starehe anashindwa nini kuwekeza katika sekta inayomgusa moja kwa moja ya kilimo ambako kuna faida kubwa na kuachana na kelele -pengine za walevi- na kujifunza matusi kutoka kwao hata kutukana wengine!
Inaeleweka kwamba wasomi ni watu wanaopima na kuchambua hoja na kuzijibu kwa nguvu zenye kusukumwa na kutanabaishwa kwa hoja husika, lakini kamwe siyo kurejesha matusi kama alivyofanya msomi huyo kwangu.
Inawezekana pia siyo msomi, bali ni mhuni tu wa kawaida ambaye ubongo wake umechanganywa na ‘mipombe’ anayokunywa hadi usiku wa manane, hata kushindwa kupata muda wa kupambanua lipi jema na lipi la manufaa na kuambulia ‘mitusi’ isiyokuwa na faida kwake.
Huyu ameshindwa kabisa kutambua kwamba KONA YANGU imekuwepo ikielimisha, kukosoa, kuonya na hata kupongeza pale inapoonekana kunafaa kuzungumziwa kwa manufaa ya wananchi.
Wakati umefika sasa kwa wasomi wetu kuwa na utaifa zaidi na kuwa tayari kujifunza zaidi na ikiwezekana kuwa wenye kupigiwa mfano katika shughuli wanazofanya, hasa zinazohusiana moja kwa moja na taaluma walizosomea.
Kila heri wasomi wetu.

Tuesday, August 23, 2005

Maprofesa SUA na baa za mifano!

Niko Morogoro sasa. Ninafanya kazi zangu za kujipatia riziki, si mwajua jamani maisha popote. Morogoro ni mji unaokua kwa kasi kubwa na karibuni utakuwa na idadi kubwa ya watu kutokana na kuwa na vijishughuli vingi hapa.
Katika pita pita zangu, nimekutana na mabaa mazuri ajabu hapa. Ama hakika ni baa za mfano. Zimepangwa vyema, zina vinywaji vya kila aina na wahusdumu wake siyo hapa, wamiliki au mameneja wao wanajua kweli kuchagua. Nawapongeza.
Nilichugundua ni kwamba baa zote hizo zinamilikiwa na maprofesa na madaktari, wataalamu waliobobea katika kilimo na mifigo. Ni wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).
Hawa wataalamu kwa kweli nawapa sifa kwa kujua namna ya kuendesha biashara za baa na jinsi wanavyoweza kuwakamata wateja kama 'wanalia' vile. Wanawapata kirahisi kweli.
Hawa mabwana (sina uhakika kama mabibi nao wamo), sina ugomvi nao katika kuanzisha mabaa haya mazuri, lakini kinachonisikitisha zaidi ni kwamba mbona wanashindwa kuwa na mashamba ama bustani za mifano kama wanavyofanya katika mabaa.
Mbona hawana mifugo ya mfano ili wakulima waweze kuiga kutoka kwao na wao waweze kufaidi elimu yao.
Ina maana hawa mabwana wao elimu yao ni ya kufundisha tu darasani, nje ya hapo hawana kitu...ni kuuza bia tu - Basi.
Ngoja nikomee hapo kwanza, nawahi hapo baa kuna kinywaji changu nilikiacha ghafla kuja kuandika hii.
Baadaye

Vyombo vya habari viwe na utaifa zaidi sasa

BAADAYE mwaka huu, Watanzania watakuwa wakiamua nani anawafaa kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano katika nafasi mbalimbali za uongozi ambazo ama ziko wazi au zitakuwa wazi siku chache zijazo.
Nafasi ninazozungumza hapa ni za aina tatu ambazo ni Urais, Ubunge na Udiwani. Hawa wote kwa jumla yao ni viongozi ambao wanapaswa kushirikiana na Watanzania wengine kuhakikisha kwamba maadui wa maendeleo na neema ya nchi wanapigwa vita kwa hali, mali na ikiwezekana damu.
Ieleweke kwamba nafasi za ubunge zitakuwa wazi rasmi kuanzia kesho baada ya gazeti la serikali kutangaza hivyo, huku nafasi za udiwani zikiwa tayari wazi baada ya mabaraa kuvunjwa na kwa upande wa nafasi ya Urais hadi baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu, Mwezi Novemba.
Viongozi tunaowatafuta kwa nafasi zote ni wale tu wenye kuonekana dhahiri, kwa kwamba wana lengo la kushirikiana na wananchi wenzao kutokomeza rushwa, magonjwa, ufisadi na ujinga.
Hawa tunawataka kuwa wenye ukweli katika mioyo yao na matendo yao, kiasi kwamba wakiomba kura kwamba tuwachague, ituridhishe kwamba wanayonena ni kweli na wala siyo unafiki ambao, kwa wengi, umekuwa ndiyo ahadi za wanasiasa.
Pamoja na kwamba wakati wa kampeni, mengi ya kuvutia, kunenepesha ngoma za masikio na mboni za macho yatajitokeza, bado wananchi wanayo karata yao ya kuwakataa wote wenye kutaka nafasi ya uongozi kwa kuwa tu wanataka sifa za kuitwa waheshimiwa au kupata mafao ni kiinua mgongo kinachotota mafuta.
Katika kipindi hiki cha sasa hadi kufikia siku ya kupiga kura, vyombo vingi vya habari vimeibuka kwa wingi na kwa kasi ya kutisha, vingi vikiwa ni sehemu ya kuanza mikakati ya kampeni kwa wagombea wao.
Ni jambo jema mno kuwa na vyombo vingi vya habari ambavyo vinajua vimeanzishwa kwa sababu gani yenye mwelekeo wa kutoa mchango kwa maendeleo ya nchi yetu na wala siyo vinginevyo.
Sisemi kwamba kuna dhambi katika kuwepo kwa wingi wa vyombo vya habri katika kipindi hiki, kwani ninaamini kabisa ndicho kipindi ambacho Watanzania wengi zaidi wanapaswa kupata habari zaidi kuliko kipindi kingine chochote.
Vyombo vya habari, hasa magazeti yanabeba jukumu kubwa la kuwaelimisha wananchi juu ya kuwa na uamuzi sahihi, kwanza kwa kuwaweka wazi wagombea wenyewe, nia na malengo yao kuomba nafasi wanazozitaka.
Ikiwa vyombo vya habri hivyo vitasimama katika ukweli na kutangaza yale tu yenye kuhuisha maendeleo yetu, amani na muungano wetu, historia kamwe haitaweza kuwahukumu waandishi husika na hata wamiliki wa vyombo vyenyewe.
Lakini, itakapotokea vinginevyo, kwa maana ya waandishi kutofuata maadili yao yanayobebwa na dira ya ukweli, uwazi, haki na kulinda haki ya binadamu katika kuandika habari zao, basi historia kamwe haitawaacha wao na wamiliki wa vyombo hivyo hivi hivi hata kama itapita miaka mingi ijayo. Lazima hukumu itatolewa hata wakiwa makaburini.
Nina hakika kwamba yapo baadhi ya magazeti yaliyoanzishwa sasa ama kuibuka katika kipindi hiki, yatatumia mwanya uliopo kuandika uongo, chuki, uzushi, fitina na kila aina ya uchafu unaoonekana kufaa kwao kwa malengo yanayojulikana zaidi kwa waandishi wenyewe na wamiliki wa vyombo hivyo.
Ni katika kufanya hivyo, wamiliki na waandishi watakuwa wakipata fedha za ziada- kwa kuuza magazeti ya- ambazo wanadhani zitawanufaisha kwa kujiwekea akiba, kujenga nyumba au kufanya mambo ya hovyo yenye kuwapa sifa za muda mfupi huku wakiacha madhara makubwa kwa jamii.
Uandishi wa namna hii unapaswa kupigwa vita, siyo na serikali pekee, bali hata wananchi ambao ndio wanunuzi, kwani kuendelea kuulea matokeo yake ni majuto ambayo hayatakuwa rahisi kuyafuta katika kipindi kifupi.
Nguvu ya vyombo vya habari inaeleweka na madhara yake yanaonekana, siyo kwa nchi jirani pekee, hata hapa nchini nguvu hiyo inaonekana hata kama wapo wasiyoiona na kudhani vyombo vya habari vipo vipo tu kwa ajili ya biashara – full stop. Havina lolote linaloweza ‘kupindua’ mtazamo wa wananchi.
Ninaeleza hivi kwa kuwa tayari dalili zipo zenye mwelekeo wa kuchomoza ‘ujenzi’ wa chuki unaoundwa na vyombo hivyo, bila kujali maslahi ya taifa kana kwamba wanaoandika hawahusiki na maendeleo wala amani ya Tanzania.
Vyombo vya habari na hasa magazeti yameanza kutukana, kukejeli na hata kudhalilisha na kuchochea chuki miongoni mwa wananchi iwe katika medani za kidini, kisiasa au kushambulia wenye kuonekana wana nia ya kutaka kuomba ridhaa ya wananchi katika kupata nafasi.
Habari za jumla jumla kwamba kundi Fulani halimtaki mgombea Fulani kwa sababu A-Be-Che zenye kutukana zinapaswa kuepukwa kabisa na vyombo hivyo, hata kama habari yenyewe itampa utajiri mwandishi au mmiliki wa chombo husika. Watambue kwamba; Utajiri siyo kila kitu duniani.
Itamfaidisha nini mwandishi au mwenye chombo cha habari kumiliki majumba makubwa ya kifahari, wanawake wazuri wote Dar es Salaam, magari aghali, tiba aitakayo, ikiwa amani itakuwa imevurugika au kuzungukwa na idadi kubwa ya masikini wenye njaa ya kutisha?
Mfano halisi wa mchango wa vyombo vya habari katika kuvunja amani na kuvuruga maendeleo unaonekana katika nchi ya Rwanda, ambapo waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari walilazimisha kuwepo kwa chuki zilizosababisha ndugu wa jamii mbili- Watutsi na Wahutu kuanza kuchinjana bila woga.
Vyombo hivyo, kama inavyoanza kujitokeza sasa, vilianza kuandika mambo ya hovyo ya uongo, fitina na majungu kuhusu mgombea mmoja mmoja na baadaye kuendelea na kundi kubwa linalomhusu na hatimaye kuleta chuki ya jamii nzima.
Yaliyotokea Rwanda sasa ni historia yenye uchungu usippaswa kurejewa na jamii yoyote ya biandamu. Watu wanaofikia milioni moja walichinjwa na kunyongwa katika kipindi cha siku mia moja tu; kisa-vyombo vya habari vimechochea.
Hatupendi haya yatokee hapa kwetu wala eneo jingine lolote duniani. Na Watanzania wasidhani kwamba ilitokea Rwanda hapa haiwezi kutokea kwa kuwa tu amani iliyopo imezoeleka. Thubutu!
Inapaswa kila mmoja kwa mahali alipo, wakiwemo waandishi, wamiliki wa vyombo vya habari na vyombo vyote vya usalama, kutokuwa na woga wa kuwakemea wenzao wenye mwelekeo wa kutanguliza tamaa ya matumbo yao ya utajiri kupitia kuandika habari za uongo na chuki.
Kinachopaswa kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari ni kutanguliza utaifa kwanza kila wanapotaka kutangaza ama kuchapisha habari, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Fedha za damu, kamwe hazimuachii furaha ya milele mwandishi au mmiliki wa chombo cha habari.
Inawezekana. Utaifa kwanza.

Thursday, August 04, 2005

Wenye presha watakufa leo

Jamani, napenda kuwaeleza kwamba waliokuwa wabunge wakidai kwamba wana hati miliki ya maeneo yao, leo watakufa kwa presha baada ya majina yao kushindwa kurejeshwa na kamati za kuwachuja. Hawa ni wale walioko katika chama tawala.
Inawezekana kabisa wengi wao wakakosa kuamini macho na masikio yao watakapokuwa wamepigwa chini na kulaumu ung'ang'anizi wao kwenye viti vya Bunge.
Sitaki kueleza mengi, tusubiri hadi hiyo kesho nitakapokuwa fiti kuwaletea habari za vifo vya waliokuwa waheshimiwa kwa miaka mitano au zaidi.

Mikono ya waandishi sijae damu

BAADAYE mwaka huu, Watanzania watakuwa wakiamua nani anawafaa kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano katika nafasi mbalimbali za uongozi ambazo ama ziko wazi au zitakuwa wazi siku chache zijazo.
Nafasi ninazozungumza hapa ni za aina tatu ambazo ni Urais, Ubunge na Udiwani. Hawa wote kwa jumla yao ni viongozi ambao wanapaswa kushirikiana na Watanzania wengine kuhakikisha kwamba maadui wa maendeleo na neema ya nchi wanapigwa vita kwa hali, mali na ikiwezekana damu.
Ieleweke kwamba nafasi za ubunge zitakuwa wazi rasmi kuanzia kesho baada ya gazeti la serikali kutangaza hivyo, huku nafasi za udiwani zikiwa tayari wazi baada ya mabaraa kuvunjwa na kwa upande wa nafasi ya Urais hadi baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu, Mwezi Novemba.
Viongozi tunaowatafuta kwa nafasi zote ni wale tu wenye kuonekana dhahiri, kwa kwamba wana lengo la kushirikiana na wananchi wenzao kutokomeza rushwa, magonjwa, ufisadi na ujinga.
Hawa tunawataka kuwa wenye ukweli katika mioyo yao na matendo yao, kiasi kwamba wakiomba kura kwamba tuwachague, ituridhishe kwamba wanayonena ni kweli na wala siyo unafiki ambao, kwa wengi, umekuwa ndiyo ahadi za wanasiasa.
Pamoja na kwamba wakati wa kampeni, mengi ya kuvutia, kunenepesha ngoma za masikio na mboni za macho yatajitokeza, bado wananchi wanayo karata yao ya kuwakataa wote wenye kutaka nafasi ya uongozi kwa kuwa tu wanataka sifa za kuitwa waheshimiwa au kupata mafao ni kiinua mgongo kinachotota mafuta.
Katika kipindi hiki cha sasa hadi kufikia siku ya kupiga kura, vyombo vingi vya habari vimeibuka kwa wingi na kwa kasi ya kutisha, vingi vikiwa ni sehemu ya kuanza mikakati ya kampeni kwa wagombea wao.
Ni jambo jema mno kuwa na vyombo vingi vya habari ambavyo vinajua vimeanzishwa kwa sababu gani yenye mwelekeo wa kutoa mchango kwa maendeleo ya nchi yetu na wala siyo vinginevyo.
Sisemi kwamba kuna dhambi katika kuwepo kwa wingi wa vyombo vya habri katika kipindi hiki, kwani ninaamini kabisa ndicho kipindi ambacho Watanzania wengi zaidi wanapaswa kupata habari zaidi kuliko kipindi kingine chochote.
Vyombo vya habari, hasa magazeti yanabeba jukumu kubwa la kuwaelimisha wananchi juu ya kuwa na uamuzi sahihi, kwanza kwa kuwaweka wazi wagombea wenyewe, nia na malengo yao kuomba nafasi wanazozitaka.
Ikiwa vyombo vya habri hivyo vitasimama katika ukweli na kutangaza yale tu yenye kuhuisha maendeleo yetu, amani na muungano wetu, historia kamwe haitaweza kuwahukumu waandishi husika na hata wamiliki wa vyombo vyenyewe.
Lakini, itakapotokea vinginevyo, kwa maana ya waandishi kutofuata maadili yao yanayobebwa na dira ya ukweli, uwazi, haki na kulinda haki ya binadamu katika kuandika habari zao, basi historia kamwe haitawaacha wao na wamiliki wa vyombo hivyo hivi hivi hata kama itapita miaka mingi ijayo. Lazima hukumu itatolewa hata wakiwa makaburini.
Nina hakika kwamba yapo baadhi ya magazeti yaliyoanzishwa sasa ama kuibuka katika kipindi hiki, yatatumia mwanya uliopo kuandika uongo, chuki, uzushi, fitina na kila aina ya uchafu unaoonekana kufaa kwao kwa malengo yanayojulikana zaidi kwa waandishi wenyewe na wamiliki wa vyombo hivyo.
Ni katika kufanya hivyo, wamiliki na waandishi watakuwa wakipata fedha za ziada- kwa kuuza magazeti ya- ambazo wanadhani zitawanufaisha kwa kujiwekea akiba, kujenga nyumba au kufanya mambo ya hovyo yenye kuwapa sifa za muda mfupi huku wakiacha madhara makubwa kwa jamii.
Uandishi wa namna hii unapaswa kupigwa vita, siyo na serikali pekee, bali hata wananchi ambao ndio wanunuzi, kwani kuendelea kuulea matokeo yake ni majuto ambayo hayatakuwa rahisi kuyafuta katika kipindi kifupi.
Nguvu ya vyombo vya habari inaeleweka na madhara yake yanaonekana, siyo kwa nchi jirani pekee, hata hapa nchini nguvu hiyo inaonekana hata kama wapo wasiyoiona na kudhani vyombo vya habari vipo vipo tu kwa ajili ya biashara – full stop. Havina lolote linaloweza ‘kupindua’ mtazamo wa wananchi.
Ninaeleza hivi kwa kuwa tayari dalili zipo zenye mwelekeo wa kuchomoza ‘ujenzi’ wa chuki unaoundwa na vyombo hivyo, bila kujali maslahi ya taifa kana kwamba wanaoandika hawahusiki na maendeleo wala amani ya Tanzania.
Vyombo vya habari na hasa magazeti yameanza kutukana, kukejeli na hata kudhalilisha na kuchochea chuki miongoni mwa wananchi iwe katika medani za kidini, kisiasa au kushambulia wenye kuonekana wana nia ya kutaka kuomba ridhaa ya wananchi katika kupata nafasi.
Habari za jumla jumla kwamba kundi Fulani halimtaki mgombea Fulani kwa sababu A-Be-Che zenye kutukana zinapaswa kuepukwa kabisa na vyombo hivyo, hata kama habari yenyewe itampa utajiri mwandishi au mmiliki wa chombo husika. Watambue kwamba; Utajiri siyo kila kitu duniani.
Itamfaidisha nini mwandishi au mwenye chombo cha habari kumiliki majumba makubwa ya kifahari, wanawake wazuri wote Dar es Salaam, magari aghali, tiba aitakayo, ikiwa amani itakuwa imevurugika au kuzungukwa na idadi kubwa ya masikini wenye njaa ya kutisha?
Mfano halisi wa mchango wa vyombo vya habari katika kuvunja amani na kuvuruga maendeleo unaonekana katika nchi ya Rwanda, ambapo waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari walilazimisha kuwepo kwa chuki zilizosababisha ndugu wa jamii mbili- Watutsi na Wahutu kuanza kuchinjana bila woga.
Vyombo hivyo, kama inavyoanza kujitokeza sasa, vilianza kuandika mambo ya hovyo ya uongo, fitina na majungu kuhusu mgombea mmoja mmoja na baadaye kuendelea na kundi kubwa linalomhusu na hatimaye kuleta chuki ya jamii nzima.
Yaliyotokea Rwanda sasa ni historia yenye uchungu usippaswa kurejewa na jamii yoyote ya biandamu. Watu wanaofikia milioni moja walichinjwa na kunyongwa katika kipindi cha siku mia moja tu; kisa-vyombo vya habari vimechochea.
Hatupendi haya yatokee hapa kwetu wala eneo jingine lolote duniani. Na Watanzania wasidhani kwamba ilitokea Rwanda hapa haiwezi kutokea kwa kuwa tu amani iliyopo imezoeleka. Thubutu!
Inapaswa kila mmoja kwa mahali alipo, wakiwemo waandishi, wamiliki wa vyombo vya habari na vyombo vyote vya usalama, kutokuwa na woga wa kuwakemea wenzao wenye mwelekeo wa kutanguliza tamaa ya matumbo yao ya utajiri kupitia kuandika habari za uongo na chuki.
Kinachopaswa kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari ni kutanguliza utaifa kwanza kila wanapotaka kutangaza ama kuchapisha habari, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Fedha za damu, kamwe hazimuachii furaha ya milele mwandishi au mmiliki wa chombo cha habari.
Inawezekana. Utaifa kwanza.

Saturday, July 16, 2005

Viongozi wote wezi!

Huyu bwana ni rafiki yangu, ndiyo ameingia kutoka Marekani huko kwao. Amekuwa akiwasiliana nami akieleza sababu za kuja kutembelea nchi yetu. Kwamba anafanya utafiti fulani ambao amenieleza. Kwa leo siusemi.
Anadai kwamba alikuja na mtazamo kwamba Tanzania ni masikini mno, kiasi kwamba watu wake wanashindwa hata kula milo mitatu au zaidi kwa siku moja. Hasa akizingatia kuwa idadi kubwa ya watu wetu wanaweza tu kupata kiasi kisichozidi dola moja kwa siku (sawa na sh. 1,000). Kiasi hiki kinamshangaza mno.
Jamaa huyo, ananieleza hata kwamba alikuwa akisita hata kuomba kuishi nami kwenye kijumba cha mbavu za mbwa mambacho alikuwa akikijenga katika akili yake kabla ya kutua Dar es Salaam.
Ananieleza kuwa mtazamo wake kwamba Tanzania ni masikini aliufuta baada ya kutua na kuanza safari ya kuelekea huko mabonde kwinama ninakoficha mwili wangu wakati wa usiku na vyombo vyangu na miili ya wale ninaoishi nao, bila kusahau wadudu tegemezi kama mende, panga na...hapana viroboto hakuna...weweeee!.
Siku mbili tatu za kumtembea huko alikokuwa akienda, hakuwa akiamini jinsi anavyokutana uso kwa uso na magari makubwa ya kifahari ambayo hakusita kunieleza hata kwao ni machache mno kutokana na kuuzwa bei ghali. Du...namweleza mbona hapa hayo ni mambo madogo, asione mie sina basi akadhani tuko sawa...hapana bwana.
Kweli ameona mengi na amenieleza mengi kuhusu mtaamo wake, lakini kubwa na hitimisho lake ni kwamba wote wenye magari ya kifahari na kuishi maisha ya utaua hapa duniani ni wezi, hasa kwa nchi kama Tanzania inayotangazwa kila kukicha kwamba inatembeza bakuli kwao ili kupatiwa msaada.
Anapopata kiasi cha mshahara wa waziri na waziri mkuu, ndiyo anachanganyikiwa kabisa na kusisitiza, hakuna mwenye usafi miongoni mwao, kwamba eti wote wezi wanaibia umma, ndiyo maana hakuna maendeleo, iweje wawe na magari mengi ya kifahari, moja lake, jingine la mtoto wa kwanza wa kiume, mtoto wa kwanza wa kike, mama na baba na pia jingine moja au mawili kwa nyumba ndogo.
Haya amesema, wengine mchangie.
Tutafika! Au ndo bakuli litatembezwa kila kukicha kwa wakubwa na kuwasujudia kana kwamba bola wao sisi tusingekuwepo duniani.

Tuesday, July 12, 2005

Mrema anafaa kuwa mcheza sinema

Nimecheka weee, mpaka mbavu zangu zinauma.
Huwezi kuamini kwamba nimeona sinema ya vichekesho ambayo naweza kabisa kuipa nafasi ya kwanza kwa kunichekesha vyema mwaka huu.
Kitu kilichozoeleka ni kwamba sinema nyingi za namna hiyo tunaziona kutoka kwa waigizaji wa nje, lakini huyo wa safari hii ni Mtanzania mwenzetu. Sielewi kwanini anakaa akipigizana kelele na serikali badala ya kuingia kwenye usanii na akala mahela yake kiulaiiini, kwani hawaoni wasanii wa sasa wa Bongo, wimbo mmoja tu (wao wanaita single) ananunua gari na hata nyumba.
Huyu msanii siyo mwingine, bali ni Augustino Lyatonga Mrema, mzee wa Kiraracha kule Moshi aisee.
Basi bwana, yeye jana wakati ameshachukua fomu kutoka kwa wakubwa wa usimamizi wa uchaguzi, akapanda baiskeli akiwa na mgombea mwenza wake, mwanamama kutoka Zanzibar. Wakazungushwa mji mzima wa Dar es Salaam wakiwa na wafuasi wao huku bendera za chama chao cha TLP zikitawala.
Ilikuwa ni burudani ya aina yake kwa kweli. hakuna aliyenuna baada ya kumuona Mrema akiwa juu ya baiskeli ya miguu mitatu akiwapungia wananchi kwa ishara ya kuwaambia kwamba anaingia kwenye kinyang'anyiro hivyo anaomba kura zao aweze kula tu kama wenzake wanavyofanya. Hakuna tofauti kamwe miongoni mwa hawa wenzetu.
Naomba kumpa ushauri wa bure, ikiwa atashindwa (jamba ambalo ninalo uhakika), basi aanze uigizaji katika vituo vya trelevisheni vya hapa kwetu na hata nje, kwani hata kama hajui malugha ya wengine anaweza kabisa kuwa mchekeshaji wa ishara tu kama Roward Atkinson (Mr. Bean). Akifanya hivyo hatakuwa mwenzetu tena, atakuwa ni bilionea mkubwa.
Kila heri Mzee mzima Mrema.

Monday, July 11, 2005

Fomu za Urais leo

Wanaotaka kuwaongoza Watanzania leo wanaanza kuchukua fomu.
Najua wanachofanya ni sinema tu, wanachukua fomu kuhalalisha ulaji tu, hakuna mwenye uchungu wa kuwatetea Watanzania. Hizo fomu zinahalalisha ulaji wao ambao utawekewa uzito na kura za wananchi hao hao wanaodanganywa kwa peremende na kilo ya sukari na sembe.
Haya, kwa kuwa ni utaratibu uliopo, basi acha wachukue na siku ikifika watangazwe wameshinda ili waendelee kula na kula na kulaaaaaaa.

Kumbe nanyi mwajua kama mimi!

Nimeona majibu ya ndugu zangu kuhusu msimamo niliouandika katika blog hii na mengine kukumbana nayo katika mail account yangu. Yote ni mazuri na yanaonyesha jinsi watu wanavyotofautiana kuhusu vitendo vya Marekani (pamoja na Uingereza na washirika wao) na Irak na mataifa mengine.
Wapo wanaodai kuwa Bush anaonea na wengine wakieleza kuwa anastahili na huo ndiyo mshahara wa dhambi anazofanya dhidi ya watu wengine.
Lakini, wapo pia wanaoeleza kusikitishwa kwao na 'uonevu' wa Bush kwa nchi zingine na kwamba wanananchi wake na hata wale wa Blair, wakishambuliwa hakuna mbaya. Ni haki yao.
Kila mmoja ana mtazamo wake. Kwangu mimi nilitaka kuibua hoja ambayo imekuwa ikikinzani kila kukicha na kutoka kwa kila mmoja.
Bado mjadala uko wazi, lakini msimamo wangu ni kwamba Bush anakosea na Wanaopiga wananchi wake wanakosea.
Hivyo, MOJA NI MOJA.
Tuko pamoja.

Friday, July 08, 2005

al-Qaeda wahuni, hamna akili

Hivi shetani wa miguu mingapi amewaingilia katika vichwa vyenu. Mbona mnakuwa wajinga namna hii nyie al-Qaeda?
Iweje mnaua tu watu hata wasiowahusu wala kuwawekea kauzibe matakwa yenu. Na sina uhakika mnataka nini, je ni haki fulani au hamu ya kuona damu ya binadamu ikimwagika kama kuku wa msaada.
Mnashindwa nini kumfuata Blair mwenyewe au Bush na kuwatwanga risasi, badala ya kuendelea kuua hata ndugu zenu wenye imani moja na mnaotoka nao eneo moja. Mnawaonea jamani na mnajiongezea dhambi tu bure. Wafuateni wahusika, mnashindwa nini.? Au nyie ni waoga?
Nipeni jibu. Mmefanya nini sasa kuua watu kibao pale Londoni, kwani hamjui Blair anaishi wapi, kama mtasema kwamba hakuwepo, basi mngempandia huko huko alikokuwa, kwenye mkutano wa matajiri.
Acheni woga jamani, si mnaweza!

Thursday, July 07, 2005

Wananchi kaeni mkao wa kula

Wananchi wangu, mlioko ndani ya Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi yetu nzuri inayovuja maziwa na asali, lakini vimiminika hivyo vitamu vikifaidisha wachache kutokana na uroho wao na ubinafsi.
Inaeleweka kwamba wabunge wetu, kila mmoja wao amevuta zaidi ya sh. milioni 30 ikiwa ni kiinua mgongo chake.
Ili angalau na wewe mwananchi ufaidi kiasi kidogo cha fedha hizo, basi usikubali kabisa kuziacha zote zikiishia mifukoni kwa waheshimiwa hao, kaa tayari kuzitafuna ingawa kidogo, kwani kipindi cha kuanza kutumika kwa fedha hizo kwako ndiyo kimewadia.
Nani asiyejua kuwa wabunge wamekuwa wakitenga sehemu ya fedha hizo kununua kura yako? Usikubali kabisa sasa kupewa upande wa khanga, sukari robo kilo na chumvi. Zamani imepita.
Akija kwa rushwa, basi nawe kamata...na chagua mtu unayeona anafaa kuongoza na kuleta maendeleo.
Ukweli unabaki pale pale kwamba wabunge wengi wanatumia rushwa kupata nafasi hizo, wao wameibatiza ruswa hiyo kwa jina la takrima kwa maana ya ukarimu wa Waafrika, lakini ukweli ni kwamba ni rushwa tu hiyo.
Rushwa ni mbaya sana, lakini kama imehalalishwa na wenyewe unafanya nini, kula na anza mbele.
Nawatakia wananchi wangu rushwa njema.

Rushwa tunaitetea, haitaisha

WATANZANIA ni watu wa ajabu. Ni watu wasioeleweka. Ni binadamu ambao hawawezi kusema wanachokiamini na badala yake husema wasichokiamini.
Haihitaji shahada ya juu ya elimu ya utambuzi wa tabia za watu kuweza kung'amua hilo pindi unapopata nafasi ya kuongea nao; iwe viongozi wa vyama vya siasa, watendaji wakuu wa serikali, wafanyabiashara na watu wengine wa kada mbalimbali.
Ni kutokana na hali hiyo, maovu mengi katika jamii yetu yameshindwa kutokomeza kwa kuwa unafiki umejaa katika fikra za watu bila kujali vyeo, umri na hata jinsia zao. Kila mmoja anajitahidi kumpiku mwenzake kwa rushwa na aina nyingine ya wizi unaofanana na huo.
Idadi kubwa ya Watanzania watasikika wakipiga vita rushwa, tena wengine wakisimama hata kwenye masinagogi, kwenye mikutano ya hadhara au wakizungumza na waandishi wa habari. Wanapozungumza hayo, mate yanawatoka kama mvua za rasharasha wakitoa maneno makali ya kukemea uonvu huo.
Kumbe ukweli ni kwamba wote hao ni waongo, wanachoamini sicho wanachokieleza mbele ya umati mkubwa wa watu.
Wengi wanashabikia rushwa kwa njia moja au nyingine. Ushahidi wa haya ninayoelaza upo wa kutosha na kwamba ni mtazamo ambao una mwangwi wa Watanznaia wachache waaminifu.
Hao wenye kupayuka wakilaani rushwa na uchafu mwingine unaodumaza haki, usawa na maendeleo, ndiyo wenye kuibuka na maneno yasiyofaa kama- kila mtu hula mezani kwake, chukua chako mapema na mengine yanayotia kichefuchefu.
Bila aibu, msemo wa -'kila mtu anakula mezani kwake'- hauna maana nyingine bali ni kuchochea rushwa. Inaeleweka kwamba kila mfanyakazi hulipwa ujira wake kulingana na makubaliano na mwajiri wake, sasa msemo huo unatoka wapi na una haja gani ya kushabikiwa?
Idadi kubwa ya watu wenye nafasi ya kuwatumikia wananchi katika ofisi za serikali, mashirika, vyama vya siasa, vyama visivyokuwa vya serikali na hata katika sekta binafsi, mawazo yao yamejaa namna ya kula rushwa.
Na msukumo wa mawazo hayo unachochewa na jamii inayowazunguka watumishi hao. Jamii pana hivi sasa imekuwa ya hovyo, ikishabikia wezi, wala rushwa na majangili.
Vijana wanapopata kazi na kuwa waaminifu kazini kwao, jamii huanza kuwajaza ujinga kwamba wanatakiwa kula rushwa ili waendelee na kuwa na maisha mazuri yanayoonekana mema.
Jamii imekuwa ikipiga saluti kwa wezi ambao wanaonekana wakiishi katika nyumba mithili ya mahekalu au wakiendesha magari ya kifahari wanayoyapata kwa rushwa ama uongo mwingine wanaoubatiza kuwa mtakatifu.
Kwa kuwa sasa rushwa ndiyo mtindo katika maeneo mengi, asiyekula rushwa anaonekana mshamba na anayekula 'chakula' hicho anaonekana mtakatifu na mtu mwenye akili.
Enzi zilizokuwa zikiongozwa na Hayati Mwalimu Nyerere waliokuwa wasafi, kwa maana ya kutokula rushwa ndiyo walikuwa wenye sifa kubwa machoni pa jamii na walionekana kufaa kuwatumikia wananchi. Kipindi hicho rushwa iliogopwa na haikutamanika kama ilivyo kinyume chake leo.
Hao waliokuwa watumishi waaminifu wakati huo, leo jamii inawacheka kwamba hawakuwa na akili, kwamba walikuwa wajinga kwa kushindwa kujijenga kwa kutumia nafasi zao.
Katika hali ya sasa, anayehongwa na kujenga nyumba ama kuwa na magari ya kifahari, ndiye anashabikiwa na kila mtu, akionekana ana nguvu za ziada za akili ya kutafuta pesa na anayejua kuzitumia.
Sasa mtu anaposifiwa kwa rushwa, ni lini atathubutu kuacha mchezo huo mchafu? Mla rushwa ni kama mtoto mdogo, akisifiwa, basi ataona fahari kurejea yale anayoyafanya kwa kusifiwa.
Lakini, anapokemewa hawezi kuendelea kutenda ambayo yanawachukiza wazazi wake, walezi au hata jamii inayomzunguka. Mla rushwa naye anapokemewa na jamii inayomzunguka bila kusubiri polisi ama nguvu za serikali pekee, lazima ataona aibu.
Jamii inaweza kumkemea mla rushwa, kwa kuacha kumshabikia kwa ukwasi alionao, huku yenyewe ikiendedelea kulala njaa ama kukumbwa na magonjwa yanayoweza. Jamii inasahau kwamba umasikini uliopo unachangiwa pia na tabia chafu za kula rushwa na kutokuwajibika kwa watumishi.
Kitu cha ajabu zaidi ni kwamba, baada ya kuwa mla rushwa anashabikiwa na jamii, ni jamii hiyo hiyo inayozunguka huko na huku ikilalama kutapakaa kwa rushwa kana kwamba haiwajui wala rushwa.
Kuwashabikia wala rushwa kwa mlango wa mbele na kuwalaani kwa mlango wa nyuma, ndiyo kunawafanya wahusika kuvimba vichwa na kuona kwamba rushwa ni haali yao na wanapaswa kuendelea nayo hadi wanapostaafu ama kukamatwa na vyombo vya serikali.
Ni vyema basi, jamii ikaacha kushabikia wala rushwa, kwa maana ya kuacha kutoa rushwa ili iwe njia rahisi ya kutokomeza wizi huo na tabia za kishetani zinazofanywa na baadhi ya watu.
Inawezekana kabisa kutokomeza rushwa kwa kushirikiana na jukumu hilo lisiachwe mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa pekee na polisi.

Tuesday, July 05, 2005

Bunge sasa ni mlo tuuuu, mwananchi wa nini?

Nimeamini, kwamba ni kweli.
Huwezi kuamini kwamba sasa wabunge wanajiandaa kumwaga manyanga ya nafasi zao walizozitumikia kwa miaka mitano tu.
Wanabwaga manyanga, wakikenua na kutufanya tuone hata maggo yao tusiyahitaji. Kwanza ni machafu, kwa kuwa wengi wao hawana utamaduni wa kusafisha meno yao. Yamejaa mabaki ya nyama choma na hata bia nadhani!
Tangu jana, wanajazana kwenye madirisha ya kulipana kiinua mgongo chao. Kila mmoja anaondoka na milioni 30.
Du! Ni fedha nyingi mno, ambazo wanazipata bila ya kufanya kazi, nani kasema wana kazi kule, mbona tunawaona wakiwa wamesinzia tu na wengine kuonekana baa tangu asubuhi.
Kweli ubunge raha, yaani hata kabla ya Bunge kuvunja, tayari wao wamekunja milioni 30, Watanzania wengine wanaostaafu hufariki hata kabla ya kuona senti za mafao yao wanayoweza kuyasumbukia hata kwa miaka sita baada ya kuondoka kazini.
Kwa hali hiyo washindwe kunenepa kweli, basi labda wawe wagonjwa, lakini kama ni wazima kunenepa ni lazima na ndiyo maana wanapambana na magonjwa ya unene, mafuta mengi na maisha mazurikama yanavyoweza kutafsiriwa kwa Watanzania yaani kula minyama, kunywa mipombe kibao na kula kula kusikokuwa na mpangilio.
Jamani nani atakataa ubunge kama hali yenyewe ndiyo hiyo.
Wanaokataa ujue wamechuma mno, wamekaa mno na wamekula sana fedha zetu za walipa kodi wanaokufa kwa magonjwa yanaweza kutibika, kufa kwa njaa na wengine kufa kutokana na ujinga unaoendelea kutawala miaka nenda miaka rudi.
rafiki yangu, mlokole baada ya kusikia kwamba wabunge wanafaidi, anaeleza kuwa anaona kwamba wanafanya wizi na nia yae ya kwenda jimboni ameiacha akisema hataki kupata dhambi ya wizi.
Kweli wabunge wanafaidi, ingawa wanapaswa kuona haya na kurudisha sh. milioni 24, wachukue nne tu. Hapo nitawaelewa.
Iweje wao wapate fedha za kutosha kabisa kujenga shule, hospitali na kununua dawa ambazo zitasaidia idadi kubwa ya Watanzania masikini?
Mie simo, lakini nimeona bora niseme haya ili, labda watakaoona watajipanga upya na wabunge wajao watakataa kuwaibia wenzao kiasi kikubwa cha fedha zao.
Nimemaliza.

Monday, July 04, 2005

Wauza akili TZ sasa walipwe vyema

Waziri wa Fedha Basil Pesambili Mramba alisoma bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha wa 2005/2006 mbele ya Wabunge na Watanzania kwa ujumla na kupokea maoni tofauti. Wapo walioipongeza na wengine kuiponda.
Ni matarajio ya Watanzania kwamba bajeti hiyo itakuwa na ahueni kubwa kwa wananchi moja kwa moja, badala ya kuonekana kupendeza zaidi katika makabrasha.
Nasema hivyo kwa kuwa taarifa zinaonyesha kwamba licha ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la makusanyo ya kodi na ushuru wa serikali, hali za wananchi wengi zimeendelea kuwa mbaya.
Hali hiyo, ilitokana na ukweli kwamba baadhi ya sekta zilikuwa na kipaumbele zaidi ya nyingine na kwa hivyo, kushindwa kuonekana wazi kwa uzuri wa makusanyo hayo makubwa yanayopatikana kila mwezi.
Hali hiyo imeweza kuthibitishwa na Mramba mwenyewe na Katibu Mkuu wa Hazina, Peniel Lyimo kwamba katika bajeti iliyopita baadhi ya maeneo yalipewa kipaumbele zaidi na mengine kusuasua katika upatikanaji wa fedha zilizokuwa zikihitajika.
Sipendi kueleza kwamba nailaumu Wizara ya Fedha au serikali kwa aina ya ‘ubaguzi’ wa aina hiyo, pengine huenda umesaidia mno kuimarisha sekta hizo ambazo ni miundombinu-hasa barabara na madaraja, elimu, maji (ingawa bado juhudi zinahitajika mno), ukimwi na utawala bora.
Hakuna siri kwamba Tanzania sasa ni nchi ya kupigiwa mfano katika sekta hizo kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uongozi wa Rais Benjamin William Mkapa.
Naungana na Lyimo kwamba huenda haikuwa sahihi kuwepo kwa ubaguzi wa aina hiyo, kwa kuwa mikakati ya kutokomeza umasikini haichagui sekta, isipokuwa inatakiwa kuwepo kwa usawa katika vita hivyo kwa kila sekta.
Watanzania wana imani kwamba bajeti ya mwaka ujao wa fedha ambayo itakuwa sh. Bilioni 4.2, itakuwa imefungua milango kwa nuru ya mkakati dhahiri wa kuutokomeza umasikini nchini.
Tunaelezwa kuwa katika fedha hizo, zaidi ya sh. Bilioni 1.5 zitaelekezwa moja kwa moja katika mikakati hiyo ya kuwaondolea wananchi umasikini mkubwa ambao unawakabili kila kukicha licha ya kujituma na hata kujishughulisha katika kazi zao za kila siku.
Ninasema wanashindwa kuondoa umasikini licha ya kujituma katika shughuli zao kutokana na sababu mbalimbali ambazo zikipatiwa ufumbuzi, kwa kusaidiwa kwa kiwango kikubwa na nguvu ya serikali, umasikini unaweza kabisa kuwakimbia wananchi kila unapowaona.
Pamoja na ahueni inayotarajiwa kutokana na bajeti hiyo, haina maana kwamba kila mwananchi, hata asiyefanya kazi atafaidika na bajeti hiyo, bali ni kwamba serikali itajenga mazingira mazuri zaidi ya kufanyika kwa shughuli kwa uwazi, bila kubughudhiwa na hata kuonewa na baadhi ya watendaji wa taasisi, kama vile za halmashauri za miji na wilaya.
Inawezekana kabisa, kama inavyoelezwa katika taarifa za awali za bajeti hiyo, kwamba fedha nyingi zitaongezwa katika sekta zilizopewa kipaumbele awali na sekta zingine kupewa uhakika wa kupata fedha kwa shughuli hizo hizo za kuutokomeza umasikini.
Katika kuhakikisha kwamba hakuna urasimu katika mapambano hayo dhidi ya umasikini, bajeti hiyo inaelekeza kwamba baadhi ya fedha ambazo zimetengwa zitawafikia wananchi wengi moja kwa moja katika maeneo ya vijijini waliko.
Ni kwa njia hiyo, ni imani kwamba wahusika - wananchi wengi wataona namna fedha hizo zinavyotumika baada ya kuwa wameamua watoe kipaumbele kwa sekta gani katika matumizi ya fedha hizo, iwe katika mikopo, elimu, afya na hata miundombinu.
Pamoja na kupongeza ongezeko la bajeti hiyo na kuwepo kwa mikakati ya wazi ya kupambana na umasikini, ninashawishika kueleza kwamba ni vyema sasa kada za watu ambao wanauza akili zifikiriwe zaidi kuongezwa mishahara na marupurupu mengine.
Ieleweke kuwa kada zinazouza akili ndizo zenye nguzo na mihimili ya kuhakikisha kwamba ushindi unapatikana dhidi ya adui umasikini ambaye ameendelea kuwepo katika nchi yetu licha ya juhudi za kupambana naye ambazo ni warsha, semina, makongamanona mikutano kuzingatiwa sana.
Kada hizo zenye kuuza akili zinaongozwa na walimu. Hawa ndiyo dira sahihi yenye kuonyesha iwapo ushindi utapatikana kwa haraka zaidi au utakuwa wa kusuasua.
Ni walimu (waliofunzwa vyema vyuoni) ambao wanauza akili zao kuwezesha watoto kuwa na silaha zenye sumu za kumtokomeza adui mkubwa umasikini. Ikiwa jamii itakamata vyema silaha hiyo, ushindi dhidi ya umasikini ni dhahiri kabisa katika kipindi kifupi kijacho.
Katika mapambano na adui huyo, ni vyema walimu wakawezeshwa kwa kiasi kikubwa katika bajeti hiyo ijayo, ambapo watakuwa na uhakika wa kupata mishahara minono na marupurupu ya kuvutia.
Watakapopata malipo yanayowavutia, biashara zao za maandazi ama pipi, ukwaju au maji baridi na barafu zitakoma na kwamba watakuwa ‘wakijichimbia’ kusoma ili waweze kuwafundisha vyema vijana wetu ambao ndiyo hasa wenye mwelekeo wa kubeba silaha hizo kwa ajili ya neema na mustakabali wa nchi hii.
Mbali na walimu hao wa sekondari na elimu ya msingi, pia walimu wa vyuo vya elimu ya juu wakiwemo wale wa vyuo vikuu wataachana na ufugaji wa ‘kitimoto’, kuku na hata bata na kupoteza muda wao mwingi wakiwaza namna ya kuwatibu wanyama hao na jinsi ya kuwafanya wawe na uzito unaotosha kuwaletea faida kubwa. Watatumia muda wao kuandaa namna ya kutoa elimu yenye kubeba changamoto ya kuutokomeza umasikini.
Ikiwa walimu hao watawezeshwa kwa kiasi kikubwa, ushindi dhidi ya umasikini unaweza kuwa rahisi mno na kwamba mikakati inayopangwa itakuwa ya vitendo zaidi na kuachana na nadharia zinazopatikana kwenye makongamano na warsha zinazohalalisha zaidi kutumika kwa kiasi kikubwa cha fedha hizo hizo za kuutokomeza umasikini.
Ni matarajio ya KONA YANGU kwamba Mramba na timu yake hawatasahau kada ya watu wanaouza akili, wakiwemo waandishi wa habari makini, madaktari na watendaji wengine kwa neema ya nchi hii.
Inawezekana kuwawezesha. Tutende.

Jamani nilitekwa!

Nimepokea mengi kutoka kwa wasomaji wangu. Wanaojua namba yangu na aina nyingine ya mawasiliano, walinipata na kunilaumu kwa kupotea kwangu.
Jamani, napenda kuwaeleza kwamba nilitekwa. Ingawa haikuandikwa, lakini nilitekwa na maharamia wenye uchu wa maisha ya wengine.
Huwezi kuamini kwamba hata waandishi wetu, hawakung'amua kutekwa kwangu. Sijui hawa wanafanya kazi gani.
Walioniteka waliniachia kwa sharti la kutowataja, kwani kinyume cha hivyo watarejea na safari hii wakiwa wakali kidogo.
Walioniteka walifanya hivyo, eti wakitaka kuninyamazisha, nami nawaeleza kwamba sitakaa kimya, nitasema tu hadi niingie kaburini.
Sasa nanipanga upya, nikitoka imetoka hiyo.
Tuko pamoja.

Wednesday, May 18, 2005

Dini yangu mpya, nani ana kifua kujiunga?

Kila binadamu mwenye akili timamu ana taratibu zake za kuomba msaada kutoka kwenye nguvu anazoamini kuwa zinamsaidia kwa njia fulani katika kutatua matatizo yake moja kwa moja ama kupitia njia zingine.
Nimekuwa nikifikiri mara nyingi, namna ninavyoweza kuanzisha dini yangu ambayo itakuwa na kazi moja tu. Kazi yenyewe ni kazi kweli kweli inayohitaji wafuasi kuwa waungwana kweli na wenye moyo.
Ninataka wafuasi ambao watakuwa na kifua cha kuhimili sala zangu na taratibu za dini yangu ambayo, sijaamua masharti yawe namna gani kwa watakaohitaji kunifuata kama mchungaji wao na msimamizi mkuu katika maisha yao.
Uhakika ni kwamba nitapata tu wafuasi. Kwani hao wanaoanzisha na kupata wafuasi wana nini na mimi nishindwe ninakosa kitu gani. Nitaweza tu bwana. Najua matatizo ya watu wetu, najua wanataka nini, najua wanakosa nini na nini cha kufanya waishi maisha bora zaidi.
Awali nimesema nahitaji wafuasi wenye moyo kweli, kwa kuwa watatakiwa kujitoa kwa kila hali na kukubali kuyakabili maisha magumu ya awali kwa kuwa huenda wakakataliwa na jamii kubwa, na hata kutengwa.
Wenye kifua cha ‘zege’ na watakaovumilia hadi mwisho ndio watakaookoka na hatimaye kuiona nuru yenye neema kuu kwa ajili ya uhai wao na uhai wa watakaowafuata baadaye, miaka mingi itakayofuata.
Mhimili wa mafundisho yangu utakuwa katika sala kuu ambayo ndiyo sheria kuu: amri kuu kwa dini na lazima kwa wote waielewe, kuifahamu na si kuikariri huku wakiitekeleza kwa vitendo.
Sitakubali kuwa na wafuasi wanafiki ambao wanadhani kucheka tu, kukenua meno yao na kunifuata ndiyo nitaamini kuwa ni waumini wa kweli wa dini nitakayoianzisha ambayo itakuwa na sala kuu.
Kwa kuwa najua kuwa wafuasi wengi watakuwa wametenda dhambi nyingi, nitakubali kuanza na sala ya toba ambayo anayeitamka anatakiwa aonekane anasema kutoka moyoni, huku nafsi yake ikimtambulisha kweli anayozungumza ni yanayopita juu ya ulimi wake.
Mzee tumechukua rushwa kiasi cha kutosha, tukajenga mahekalu, tukanunua magari ya kifahari, tukalipia ada kubwa watoto wetu katika shule za Ulaya na Marekani na kidogo tukatunza katika hazina za nchi hizo.
Sasa tumegundua kuwa kuiba, kutajirika zaidi kwa njia za rushwa hakusaidii kuongeza maisha, zaidi ya kuonekana mwenye mwili ulionona na mashavu yaliyojaa nyama. Kumbe yote hiyo ni ubatili mtupu, hukumu yetu ni kifo na kwamba siku zetu zimehesabiwa. Hatuwezi hata kuishi miaka 200, tukaona mbingu mpya na watu wapya.
Ni kwa rushwa hizo hizo, tumepata magonjwa ya ajabu mno, magonjwa yasiyotibika na sasa, raha zilizokuwa zimetuzunguka – zinayeyuka kwa haraka mno, hata waliokuwa wakitushabikia na kutuita wafalme au wajanja hawatuoni tena, wanatukimbia.
Tumetoa misaada mingi kwa wagonjwa na wenye shida kwa fedha zinazonuka, fedha ambazo tulizipokea kwa mikono yetu iliyojaa damu. Fedha ambazo nao walizipokea bila kujua tumezitoa wapi.
Wapo pia waliobweteka hata kufanya kazi kwa kuwa walikuwa na uhakika wa kupata fedha hizo nyingi, kwamba tuliwatelekeza wake na na watoto wetu na hata mama na baba zetu.
Tumekuwa tukitoa mimba na kuua viumbe visivyokuwa na hatia kwa tamaa ya fedha na hata malipo mengine ambayo ni haramu na yenye uzito sawa wa dhambi kama kuua.
Pia tumekuwa tukitetea wanaotoa mimba na kuwaona kwamba wanatekeleza ahadi za uhuru wao kamili na uchaguzi. Kwamba wanaotoa mimba wana uamuzi wa kufanya wanavyopenda, kwani waliamua kuwapata wao na wanaamua kuwatoa watoto kwa matakwa yao.
Kwamba tuliamua kuwaacha watoto wajiendee kama vifaranga pasipokuwa na usimamizi na kusema kuwa wanao nao wana uhuru wa kuamua mambo yao bila kuingiliwa wala kukanywa kila wanapokwenda hovyo.
Tumedanganya idadi kubwa ya watu na kutumia vibaya madaraka yetu kwa manufaa yetu wenyewe, wake zetu na shangazi zetu na kuueleza umma kwamba hiyo ndiyo siasa ambayo inatakiwa katika mazingira ya nchi zetu masikini kama hizi.
Kwamba tumetumia madaraka, fedha na nguvu zetu za kijeshi kuwavamia wengine na kuhadaa ulimwengu kwamba tunatenda haki kwa kuwa viongozi wa nchi hizo ni wakorofi na kuwa hawafuati ustaarabu wetu.
Kwamba tumevuruga dunia kwa picha mbaya za ngono na matusi yasiyotamkika kwa watu wastaarabu na kuita tabia hiyo kuwa ni uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza na kuonyesha chochote bila kuingiliwa na yeyote.
Kwamba tumekuwa tukijifanya siye ndiyo watu wa Mungu Mkuu kwa kuwa tu tumeacha kunywa pombe, kuchukua wake za watu, kumbe tulikuwa wezi, wanyang’anyi, wakabaji na wanafiki wa kutupwa.
Tumekuwa tukitoa michango mikubwa kwenye misiba na kanisani kwa kuitangaza kwenye mimbari ili tuonekane na tusifiwe kwamba siye ndio wenye huruma, kumbe moyoni tulikuwa tukiumia, ni sifa tu zilizokuwa zikituponza na zaidi sana fedha zenyewe za wizi na rushwa iliyojaa damu.
Tumewadanganya wakulima namna ya kupanda mbegu bora na jinsi ya kulima ili wapate mazao mengi, hali iliyosababisha wao kukumbwa na njaa na wengine kufa kutokana na uongo wetu huo mkuu.
Kwamba tuliwadanganya wanafunzi madarasani na hata wakashindwa mitihani huku tukiendelea kupata mishahara yetu ya kila mwezi, na zaidi sana kupokea fedha kutoka kwa wanafunzi hao kwa jina la ‘tuition’, kitu mbacho si kizuri kwani tunalipwa na waajiri wetu, ingawa kidogo.
Yoote hayo tuliyafanya kwa kuupendezesha ulimwengu na watu wake, kumbe tulikuwa tukikuudhi mno na kukukasirisha kwa matendo hayo mabaya na machafu machoni pako na kwa malaika wako.
Dhambi zetu za kisasa ni nyingi mno na sasa tumeamua kuziacha. Ikiwezekana kwa yanayowezekana kurejeshwa na kutubu tutafanya hivyo, ambapo tukishindwa, basi tutaomba wahusika watusamehe, ingawa tutalazimika kuwaeleza tuliyoyafanya kwao.
Tunaomba haya kwako na tukitaraji msamaha wa kudumu na wa kweli ikiwa hatutarejea katika chembe ya dhambi.
Haya sala ni hiyo. Mwenye kifua na aje tuongeze ukubwa wa dini mpya

Sumaye asema yeye na Kikwete damu damu

Sumaye jana amewaita waandishi wa habari chap chap kwa lengo kumaliza minong'ono kwa,mba alikasirika sana baada ya Kikwete kuwa amechaguliwa kugombea urais na yeye kuachwa.
Akiwa ofisini kwake, kule jirani na baharini aliwaambia kuwa maneno kwamba anamchukia Kikwete ni ya uongo na kwamba hayana maana yoyote, kwamba yana lengo la kuwavurgia uhusiano wao wa siku nyingi.
Baadaye

Tuesday, May 17, 2005

Blogs kibao za Kiswahili

Ndugu zangu,
niko njiani kubadili sura ya blog yangu ili iweze kuwa rahisi zaidi kuisoma na kuonekana.
Pia ninafanya hivyo kuwepo kwa urahisi wa viunganishi pamoja na maendeleo mengine makubwa ya teknolojia hii ya mawasiliano huru.
Viunganishi vingi vitakuwa vikionyesha blogs kibao, hasa zinazotangaza Kiswahili na lugha zingine za makabila ya Tanzania, itaogopa kuonekana kwamba nataka kuendeleza ukabila kwa kufanya hivyo.
Karibuni na tuungane mkono wana blog.

Mihogo inaashiria hali mbaya, tusidanganyane

Jamani,
Nimekuwa nikijifikiria mara zote, hivi kwanini kasi ya kuwepo kwa mihogo jijini Dar es Salaam inakuwa kubwa sambamba na ongezeko la vijana wanaotoka vijijini?
Kila kona sasa ukipita unakutana na vijana wakisukuma matolori wakiuza mihogo, tofauti na zamani ambapo mhitaji alitakiwa kwenda sokoni tu kupata bidhaa hiyo. Sasa ni kila kwenye kiambaza, kila mlango wa kuingia ofisi kubwa na hata kwenye maeneo ya maduka makubwa katikati ya jiiji.
Mihogo ninayoizungumzia hapa ni mibichi, michanga ambayo haijakomaa vyema (najua kuwepo kwa kihogo inayoonekana kuwa michanga siku zote kutokana na mazingira na hali ya hewa huska).
Kwangu mimi kuwepo kwa idadi kubwa ya wanaouza mihogo, hakuna maana kwamba hamu ya kutafuna mihogo imeongezeka, la hasha. Ni shida tu.
Ni shida kwa kuwa nimeshuhudia mwenyewe kwamba watu wanatafuna mihogo hiyo na baadaye kunywa maji ya bomba yasiyochemshwa ili kushibisha matumbo yao basi.
Baada ya kula na kunywa maji, mchana unakuwa umetoka! Hakuna tena siui kusubiri ugali au chips. Nani atazikamata hizo chips kwa bei yake..Ni kina dada tu wanaofanya kazi zenye mishahara mikubwa. Chipsdume zimepanda bei hadi sh. 400 kwa vipunje kadhaa. Sasa nani ataweza gharama hiyo kubwa.
Najua kwakiwango hicho cha sh. 400, mhusika anaweza kula vipande vya mihogo vya sh. 150 na sh. 50 akashusia maji, kwa maana hiyo atakuwa ametumia sh. 200 na kiwango kama hicho kinachobaki kinakuwa cha kesho.
hayo ndiyo maisha ya vijana wengi jijini Dar es Salaam.
Wao wanasema kuwa tutabanana hapa hapa na kuwa shibe haina bei.
Tafakarini. Tujadiliane kwa hoja juu ya hili

Wednesday, May 11, 2005

Kasi ya ahadi zako Kikwete inatisha

Jamani, hapa Bongo mambo yaenda yakiongezeka, kila kukicha, wakati Kikwete anapotambulishwa kwa Watanzania, kana kwamba hawamjui kwamba ni kiongozi wao, amekuwa anatoa ahadi.
Sina ugomvi na utoaji wa ahadi za kiongozi huyo wa kitaifa ambaye amechaguliwa na CCM kuwa mgombea wake kwa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.
Kila anapokutana na wananchi, Kikwete amekuwa akiwaelea kwamba atawapatia vijana ajira na kwamba sasa wasiwe na wasiwasi na maisha yao, yatakuwa poa kishenzi. Yaani baada ya kuapishwa kwake, basi itakuwa kuku kwa mrija, soda kwa uma na kila aina ya raha.
Basi bwana, vijana wanaposikia hivyo, si furaha hizo, wenye vijisenti vyao baada ya kuuza tai moja au jozi moja ya viatu, basi wanaishia baa na kunywa...kunywa ...au kwa wale wenzangu ni kwenye gongo.
Nasikia alipofika Zanzibar na kuwaeleza ahadi zake, Kikwete alisema kuwa hakuna noma kabisa, nafasi za kazi ni bwerereeee... jamaa zangu nasikia wakaishia kwa kiongozi mmoja ambaye kwake anauza gongo kama maji ya miwa na pweza.
Acha vijana wanywe...wakanywa na hata wawili wakapigana na kutoana meno. Makubwa haya.
Tatizo langu na Kamanda wangu kikwete (yeye ni Kanali na mimi ni Serviceman)ni kuwapa matumaini hayo, ambayo kwa kweli hivi sasa ni tatizo la dunia nzima, siyo kwa nchi masikini pekee, bali hata kwa matajiri. hakuna kazi.
Sasa tusubiri tuone hizo nafasi za ajira ambazo kila kijana ana uhakika wa kupata awe amesoma au hajasoma.

Thursday, May 05, 2005

Masharti ya kazi yako Kikwete haya hapa

Shikamoo,
NATUMAI kwamba sasa umeshusha pumzi baada kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kuwa mrithi wa mpendwa wetu, Rais Benjamin Mkapa baadaye mwaka huu.
Najua kuwa ulijawa na wasiwasi, kukosa usingizi na hata kutishiwa na mvi za haraka, ukipanga na kupangua namna ya kupata ushindi ili uweze kushirikiana na Watanzania kuhakikisha kwamba neema kuu inapatikana kwa wananchi wote.
Mchakato wa safari ndefu ya kuomba kuteuliwa ulianzia Dodoma wakati ukichukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama ili ukiwakilishe katika uchaguzi mkuu kwa nafasi ya Urais.
Kazi kubwa ya kusaka wadhamini uliendelea nayo kwa siku zaidi ya 21 ambapo ulizunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na hatimaye uliwasili Dodoma kuzirejesha fomu kama taratibu zilivyokuwa zikihitaji.
Baada ya kurejesha fomu, ulisubiri vikao vya Chama vilivyoanza mapema wiki hii na hatimaye jana umepata ridhaa ya wanachama na hivyo kupata fursa ya kwenda mbele ya Watanzania wote, wakiwa waajiri, ukiomba kupatiwa kazi nambari wani nchini.
Ni matumaini ya Watanzania wote kwamba kazi hiyo, utaipata kwani umeonyesha kuwa na sifa zinazotakiwa na waajiri, ili uweze kutimiza matumaini makubwa waliyonayo kwa kazi nzito utakayoibeba kwa kutumia busara, mawazo ya wengi na Katiba ya nchi ambayo ni mama wa maamuzi yote ya maana.
Watanzania wana imani kubwa nawe, ndiyo maana kwa kuanzia wana-CCM ambao, kwa hakika, wana uwakilishi mzuri kwa mtazamo wa jamii nzima, kwamba utakuwa pambazuko jipya la ustawi wa maisha kwa ujumla wao, bila kuegemea maeneo, uwezo, rangi au hata kipato cha mtu au kikundi.
Kutokana na matarajio hayo, kazi uliyoomba ina masharti yafuatayo ambayo wengi tuna imani kwamba utayatimiza kwa neema ya Tanzania mpya kama ambavyo umekuwa ukieleza wakati ukiomba ridhaa ya Chama. Masharti yenyewe ni haya yafuatayo:-
v Kwamba utakuwa mtu wa watu, utakuwa kiongozi wa wanyonge na kubwa zaidi utajali kila mtu kwa nafasi yake, bila kuwapa nafasi ‘manyang’au ambao wana ujanja na mbinu chafu kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe kwa kutumia ajira yako mpya utakayoianza Novemba, 2005.
V Kwamba usiwaangushe Watanzania, na matumaini yao yaonekane kweli kwamba nafasi uliyoomba na hatimaye kuipata ulistahili. Kwamba wamekuwa na imani na utumishi wako katika nafasi zingine.
V Kwamba yote yaliyojiri katika mchakato wa kuomba ridhaa ya Chama sasa yatakuwa historia na utakuwa kitu kimoja na wengine wenye mapenzi mema na wewe binafsi na Watanzania.
V Kwamba utakuwa na mtazamo wenye mwanga wa kujenga na kulinda umoja wa kitaifa na kuwa hautafanya maamuzi ambayo yatakuwa yakiwafurahisha wengine, hasa wafadhili, na kuwakandamiza wananchi, waajiri wako.
V Kwamba utahakikisha kuwa mstari wa mbele kupinga na kuwatetea walio katika dhuluma na mateso. Na kubwa zaidi utasimamia haki na kulinda haki za binadamu wote wa Tanzania na ikiwezekana kutetea haki za wasiokuwa raia, ndani na nje ya mipaka yetu.
V Kwamba hutasita kuchukua maamuzi makubwa yanayoweza kutafsiriwa na ‘mabwanyenye’ kuwa ni uonevu, ilhali yananufaisha wanyonge wa nchi hii katika kuondokana na umasikini, ukosefu wa ajira, ujinga, utegemezi na maradhi.
V Kwamba utaunda timu kabambe ya watendaji wa kazi na wala siyo kuzungukwa na ndugu, marafiki au mashemeji ambao hawana uwezo wa kiutendaji, bali ni ‘wenzako’ au kuonekana kuwa unalipa fadhila ambazo walitoa katika mchakato wa kuomba kuteuliwa na hatimaye kuchaguliwa na Chama. Kila msaidizi wako ajitanabaishe kwa uwezo wake wa kiutendaji mbele ya umma.
V Kwamba utatumia busara za hali ya juu, pia kwa kuwashirikisha wengine katika kufikia maamuzi makubwa ya kuiingiza nchi katika mikataba (au hata mifarakano) na mataifa mengine, ili nchi isiingie katika ‘tundu la simba’, ambamo kujinasua baadaye kutaigharimu nchi muda, rasilimali na hata damu.
V Kwamba utakuwa muwazi kwa umma kwa maana ya kuwaeleza mipango, mafanikio na hata matatizo ya serikali yako, ili kujenga na kudumisha silka ya uwajibikaji ambayo ni siri kubwa ya maendeleo endelevu.
V Kwamba unatakiwa mnyenyekevu kwa wazee, vijana, watoto, walemavu wa jinsia zote; wanawake na wanaume.
Mheshimiwa, hayo ndiyo masharti makuu unayotakiwa kuyatekeleza kadri ya uwezo wako ukizingatia kuwa kufanya hivyo unatimiza wajibu wako kwa wananchi waliokupa ajira kuu.
Katika utekelezaji wa yote hayo, unatakiwa kujua kwamba umeomba kazi ambayo itakulazimu kupokea malalamiko kila siku, kila saa.
Utapokea malalamiko unapokunywa chai, unapoondoka kuelekea ofisini kwako, utapokea malalamiko hata unapokaribia kupumzisha mwili wako usiku.
Kubwa na muhimu ya kukabiliana na malalamiko hayo ya waajiri wako ni kuyapa nafasi ya kuyatekeleza kwa mustakabali wa mama Tanzania na watu wake.
Wakati ukiomba kazi hiyo ulisema umenuia kujenga Tanzania mpya, nguvu mpya ya maendeleo ya kasi na ari mpya.
Tunaomba sasa utekeleze mara baada ya kuapa kuanza kazi yako Novemba, 2005.
Kila jema.

Wednesday, May 04, 2005

Kikwete jua haya

Kwanza nakupongeza,
pili ni kwamba umepata kazi kubwa mno ambayo itatuhakikishia kwamba muda wako wa kuliongoza taifa hili sasa umefika, kwani mara ya kwanza, 1995 ulipojitokeza kuomba nafasi ya Urais wa Tanzania, kura hazikutosha.
Sasa kura zimetosha. Ninakuomba utuonyeshe kwamba unastahili kwa kuwa mtendaji bora kama mabavyo umekuwa ukifanya katika nafasi ulizowahi kushika.
Makutakia kila jema na uendelee kubarikiwa.

kumekucha

Tayari CCM kimepata mgombea wake leo. Huyo siyo mwimgime bali ni Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Amepata kura kibao, kwa kuwabwaga wengine. Kura za watu wawili walioinga nao kwenye kinyang'anyiro zikijumlishwa ndio zinapatikana kura zake zote.
Dk. Salim alipata kura 45, Prof. Mwandosya aliibuka na 33, huku Kikwete akipata 78. Ni kama hadithi. Ni ushindi wa kishindo.
Ninamtakia kila jema

Monday, April 18, 2005

CCM imtose yeyote bila kujali 'pembe' zake

Aprili 15 saa 10.00 jioni ulikuwa muda wa mwisho kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaomba ridhaa ya Chama kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurejesha fomu zao.
Ni siku ambayo ilifunga ukurasa wa mbio za wanachama 11 waliojitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa hiyo.
Wanachama hao tayari wamerejesha fomu zao zilizojazwa na wadhamini waliowapata mikoani kama taratibu za Chama zinavyotaka.
Masikio sasa ya Watanzania na wasio ni kupata habari za kuanza kwa taratibu ndani ya Chama za kupata jina la mwanachama mmoja miongoni wa hao waliojitokeza ili kupambana na wateule wengine kutoka vyama vya upinzani.
Kimsingi, wagombea kutoka vyama vyote kwa Urais wana nafasi na haki sawa za kuongoza Tanzania endapo wapiga kura wataamua iwe hivyo.
Vipo vyama ambavyo tayari wagombea wake wanajulikana, wengi wakiwa ni viongozi wa vyama hivyo wanaojipachika ugombea miaka nenda rudi na kuweka mizengwe kwa wanachama wenzao pamoja na kwamba katiba zao zinaruhusu kila mwanachama kujitokeza kuomba ridhaa ya vikao halali kuteuliwa kwa nafasi ya kugombea urais, ubunge na hata udiwani.
Mgombea wa CCM atajulikana usiku wa Mei 4 au alfajiri ya siku inayofuata baada ya wanachama wenye dhamana ya kuwakilisha wenzao katika Mkutano Mkuu kupitisha jina moja tu.
Hakika ni kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitapitisha jina la mgombea ambaye atakuwa na maslahi ya taifa zima bila kujali wajihi wake, sura, mvuto wake wala ulimi wake hata kama umepakwa asali na kutoa maneno matamu.
Lazima Chama kitaangalia ni kwa kiasi gani mtu anayeteuliwa analinda maslahi ya taifa na siyo Chama pekee, kwamba atakuwa mtu ambaye akisema anasikilizwa, anaheshimiwa na wananchi na hata watu wa nje. Na pia kikubwa zaidi ni kuwa na tabia ya kuwasikiliza wengine kama kiongozi bora anavyotakiwa kuwa.
Kwa maana na hiyo, siyo wanachama tu wa Chama bali wananchi kwa ujumla hawatarajii Chama kuteua mtu asiyekuwa na udhu katika moyo wake, mwili wake na matendao yake.
Kila Mtanzania anajua na ana hakika kwamba CCM itashinda uchaguzi mkuu, kwa hiyo atakayeteuliwa aanatarajiwa kuwa mtu asiye na mawaa ambaye anaweza kuipeleka nchi pabaya na kuharibu maendeleo yaliyopo, amani iliyopo na Muungano wetu.
Hakuna Mtanzania anayependa kuona Chama kinaleta mtu ambaye hajui kwamba nchi bado ina watu ambao wanaogelea katika umasikini mkubwa, watu wanaozingirwa na magonjwa na kutandaa kwa ujinga.
Imani ya wananchi wengi, bila kujali itikadi za vyama vyao ni kwa ‘kada’ mbalimbali za Chama ambazo zitaanza kazi ya kupitia na kuhakikisha kukamilika kwa taratibu zilizotakiwa kwa kila mgombea.
‘Kada ninazozungumza hapa ni ngazi zote za kupitia fomu na baadaye kuanza kuwajadili wagombea kabla ya kuwafikisha kwenye vikao muhimu ambavyo vitakuwa na jukumu zito la kuhakikisha kwamba anapatikana mwanachama mwadilifu na mnyenyekevu ambaye atakuwa na sauti inayokubalika kwa wanachama wenzake na wananchi kwa ujumla wao.
Wanachama wote 11 wana nafasi sawa ya kuteuliwa na ngazi hizo, lakini wote hawawezi kulingana kiutendaji, kitabia, kiumri na hata kimtazamo. Kila mmoja ana yake ambayo anaona akishirikiana na wengine anaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo zaidi na kudumishwa kwa amani iliyopo.
Mwanachama yeyote miongoni mwao anayedhani kwamba ni bora kuliko wengine anajidanganya na kujijengea wigo wa fitna, kinyongo na mambo mengine yanayofanana na hayo endapo hatateuliwa.
Kila aliyechukua fomu na kuzirejesha anapaswa kutambua kwamba Chama siyo mtu binafsi bali ni mfumo ambao unaendeshwa na vyombo mahsusi kabisa vilivyowekwa kwa ridhaa ya wanachama wake.
Hivyo, hakuna mwanachama anayeweza kulalama kwamba ameshindwa kwa sababu ya mizengwe kama ambavyo nchi imekuwa ikishuhudia kwa vyama vingine vya siasa vilivyotapakaa kama uyoga.
Yeyote atakayejidai kwamba ‘amewekeza’ ili kujihakikishia anaibuka mshindi atakuwa akijidanganya na kuiba mawazo yake mwenyewe. Kama aliwekeza kwa kugawa fedha-shauri yake. Kama aliwekeza kwa wanachama kwa kuwagawa kimakundi –atajiju na kama aliwekeza kwa mtaamo kwamba Chama ni chake-ameula wa chuya.
Lazima wote waelewe kwamba CCM imekuwa na nguvu kwa muda mrefu kutokana na kushonana, kushikamana na kuheshimiana kijadi kwa wanachama na wasiokuwa wanachama bila kujali rika wala makundi ya hovyo ambayo kimsingi ni ya kibaguzi tu.
Watanzania wana imani kubwa na viongozi wa CCM. Wana imani na busara zao. Wana imani na mitazamo yao, kwa maana hiyo kamwe hawawezi kumpitisha mwanachama kwa kuwa tu ni rafiki ama ndugu. Atakayepitishwa atakuwa ana uwezo na ari ya kutenda atakachokuwa ametumwa na Chama na wananchi wa Tanzania.
Viongozi, kwa maana ya wenye fursa ya kuchagua mgombea wa CCM wana dhamana kubwa ya kuhakikisha kwamba anapatikana kiongozi mwenye udhu ambaye atasaidiana na vyombo vingine kuwavusha watoto wa Tanzania hadi kwenye neema ya asali na maziwa.
Mtazamo na nguvu ya mawazo na imani ya wenye dhamana ya kuchagua mwana-CCM lazima ijikite katika dhana kwamba heri lawama kuliko hasara. Lazima apatikane mwanachama safi, mkweli, mwepesi wa kukiri mapungufu yake na kujirekebisha.
Huyo lazima awe mtu ambaye hachukizwi na upinzani bali aone kwamba ni changamoto safi ya kutekeleza majukumu na ahadi na ambaye ana kichwa chenye kubeba ubunifu wenye maana ya kuondoa shida za wananchi wa maeneo yote; vijijini na mijini.
Mwenye sifa hizo na za ziada yumo miongoni mwa wanachama 11. Huyu ndiye tunamtaka kuongoza Tanzania ya leo.
CCM inaweza.

Wasomi wanapokuwa majasusi kwa nchi yao!

KILA binadamu anatamani kuwa na maisha mazuri ili afurahie kuishi kwake na wote wanaomtegemea, ikiwemo familia, ndugu na jamaa zake.
Zipo mbinu nyingi zinazotumiwa na binadamu kufanikiwa. Wapo wanaoanza biashara na kufanikiwa, wapo wanaosoma sana na kufanikiwa na wapo wanaoibuka tu kutokana na bahati zao.
Wapo pia binadamu wanaotumia mbinu chafu kufanikiwa, ikiwemo kuua, kupora na matukio mengine ya kutisha ambayo hatimaye yanawapa mafanikio makubwa.
Hakuna binadamu mwenye akili timamu anayejibidisha katika shughuli zake bila kuwa na matumaini ya kufanikiwa siku moja.
Kujibidisha huko kunatokana na kusukumwa na tamaa za kawaida za kibinadamu za kupenda vitu vizuri, huku tumbo likishika nafasi ya kwanza. Tumbo linaongoza kwa kuwa linapenda kujazwa kila baada ya saa tatu ili mtu aendelee na maisha yake.
Miongoni mwa watu wanaojibidisha ni wasomi. Hawa ni kundi pekee ambalo limeelimika kwa kwenda shule na kupitia vyuo mbalimbali. Kwa kifupi hao ni wanazuoni ambao wanatarajiwa kuwa waongozaji wa wengine katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Ni wasomi ambao hutumika sana katika kupanga mipango ya maendeleo na dira sahihi zitakazosaidia kuhamasisha wengine kuzifuata ili kufikia malengo.
Wasomi hufundisha shuleni hadi vyuo vikuu, lengo likiwa kuendelea kujenga mtandao mkubwa wa wasomi ambao wataunganisha nguvu zao kuleta maendeleo.
Lakini katika dunia ya sasa, wasomi wengi hawapendi tena kazi za kufundisha wala kutoa dira, bali kila mmoja anajitahidi kuwa na shirika lake lisilokuwa la kiserikali (NGO) kwa lengo la ‘kusaidia’ jamii.
Wengi kutokana na usomi wao ni hodari katika kuandika michanganuo na hupata fedha kutokana na njia hiyo na kunufaika zaidi wao, wake au waume, na familia zao, pamoja na kwamba michanganuo huandikwa na kupachikwa jina kwamba “ni ya kusaidia jamii”.
Ni kutokana na hali hii ya kuneemeka kwa migongo ya watu wenye shida, baadhi ya NGO zinazojieleza kuwa zinatetea haki za binadamu, wanawake, watoto na wanaume haziaminiki kwa jamii na zipo zikiwa na sura za “mali ya familia” zaidi.
Sasa NGO (Non Governmental Organisations) hazisimami kwa jina hilo, badala yake ni ‘Non Governable Organisations’, kwa maana kwamba zipo tu bila kusimamiwa wala mtu wa kuzifuatilia.
Kutokufuatiliwa huko sasa kumeibua utaratibu mwingine mbaya zaidi ya kuibia jamii. Sasa hizo NGO ambazo nyingi zinaongozwa na wasomi, ni maficho ya mikono michafu ya taasisi za nje ambazo haziitakii mema nchi hii.
Wasomi hao badala ya kusaidia nchi sasa wamegeuka kuwa majasusi ambao wanatoa kila wanaloona linawaafaa mabwana wao ambao humwaga ‘rupia’ kama njugu ilimradi kupata taarifa wanazohitaji kupitia utafiti wa hovyo unaofanywa kwa malengo mabaya.
Inashangaza sana kuona wasomi wetu wanageuka kuwa magaidi na majasusi wa mataifa na taasisi za nje kwa kuwa tu wameona vipande vya fedha kutoka kwa ‘Wazungu.’
Kutofuatiliwa kwa NGO hizo na vyombo vya serikali kunafanya taasisi hizo kuwa na uhuru wa ajabu na kufanya zinavyotaka, kwani haziingiliwi wala kutazamwa kwa jicho na chombo chochote.
Wasomi hao viongozi wa NGO wanapoulizwa kuhusu kuhusika kwao na ujasusi wanaruka kimanga na kudai kwamba hawajui lolote kuhusu hilo na kutoa maelezo kwamba wapo kwa ajili ya kusaidia wananchi wa Tanzania.
Ingawa wanapofuatiliwa kwa undani, uwezekano wa kukutwa kwamba ni majasusi ni mkubwa na ndiyo maana ‘wenye’ NGO wamekuwa wakiungana kupinga namna yoyote ya kuchunguzwa na serikali.
Hivi hawa pamoja na usomi wao wanashindwa kuelewa kwamba hakuna serikali inayoachia tu mambo ya taasisi kwenda kama wanavyotaka, hata kama ni kichaka cha majahili?
Kuachia tu NGO kujiendesha zinavyotaka kuna hatari ya kusababisha madhara makubwa siku zijazo na kuwaacha wananchi ‘wakisaga meno’, madhara ambayo itakuwa vigumu kuyarekebisha kwa muda mfupi.
Wapo wasomi hao na NGO zao wanaoaminiwa na serikali na hata Chama, lakini kumbe wapo humo kwa ajili ya kutimiza malengo yao ya kuwatumikia majasusi wa nje. Na katika kufanya hizo zinazoitwa tafiti wapo wanaopata fursa za kujiingiza hata katika maeneo nyeti ya nchi, na wakati wanapokamilisha ‘utafiti’ wao huwasilisha ripoti kwa hao wahisani wao.
Ikiwa wasomi ndiyo wako namna hiyo, je wananchi ambao wanapaswa kuwaheshimu kutokana na taaluma zao, wawaweke katika kundi gani?
Wananchi wanapaswa kuwa macho na NGO hizo uchwara zinazoibuka kila siku kwa takwimu za hovyo zisizokuwa na ukweli wowote, zinazotumiwa tu na wale wanaoitwa wafadhili.
Ni vyema basi, serikali kwa kutumia vyombo vyake kuhakikisha kwamba NGO zinafutiliwa kwa karibu zaidi ili kuepusha madhara hayo yanayoweza kutokea.

Saturday, April 02, 2005

'Kishamapanda' aaga dunia akililia ushirika

Ni Balozi Paul Bomani
Na Simon Martha Mkina
FAMILIA ya Bomani inalia. Wanamlilia baba, babu na mjomba wao. Wanalia kwa kuwa amefariki dunia wakiwa bado wanahitaji busara kutoka katika kichwa chake kilichokuwa kikifunikwa na nywele nyingi. Nywele zilizojaa rangi nyeupe-mvi.
Wanadiplomasia wanalia. Wanalia kumpoteza mwenzi wao. Wanalia kwa kuwa watakosa ucheshi na ushirikiano wake aliouonyesha bila kuwepo kwa chembe ya unafiki.
Wasomi wanalia. Wanalia kwa kumpoteza kiongozi aliyewapigania. Wanalia kwa kuondokewa na mwanataaluma mwenzao ambaye alijitolea kuwapigania, akiwa na matumaini kwamba hata watoto wa makabwela wanasoma na kupata elimu ya chuo kikuu. Alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Chama cha Mapinduzi kinalia. Kinasikitika kumpoteza mmoja wa wapiganaji wake waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Watanzania wanaishi kwa amani na kuwepo kwa maendeleo ya haraka. Alikuwa mdhamini wa Chama.
Nchi nzima imezizima kwa kishindo kwa kuondokewa na mwalimu, kiongozi na msomi aliyebobea katika masuala ya ushirikiano wa kimataifa na uchumi.
Wanaobubujikwa bahari ya machozi ni wakulima. Wao wanalia kwa kwikwi zenye sauti kuu. Mashavu yao yamefunikwa na kimiminika chenye ladha ya chumvi chumvi, huku wakiwa wamekosa matumaini ya kumpata atakayeziba pengo la kuwapigania.
Hawa ni wanaushirika wanaodiriki kusema kuwa gwiji huyo ameondoka na funguo za mlango wa kuendeleza ushirika. Kwamba wanaobaki watakuwa watu wa kutapatapa wakisaka ziliko ufunguo, lakini wasizipate, hadi atakapoibuka mwenye nia ya dhati na uchungu wa watu hao.
Niliyoandika hapo juu yanaonyesha kwa jinsi gani, Balozi Paul Lazaro Bomani au kwa jina maarufu – Kishamapanda- alivyokuwa mtu wa watu kwa maana ya kuwa karibu nao wakisaidiana kwa jambo moja ama jingine.
Ndugu na marafiki zake wa karibu waliokuwa pamoja, wanaeleza kuwa jina la Kishambapanda alipewa na jamaa zake, hasa marafiki baada ya kugundua kuwa Paul alikuwa mtu asiyekata tama.
Kwamba alikuwa mtu ambaye akidhamiria kitu, lazima kipatikane na kufanikiwa. Akishindwa kwa njia hii, basi alikuwa akitumia njia nyingine kuweza kufanikisha.
Kishamapanda ni neon la Kisukumka lenye maana ya mtu wa mwisho kutoa maamuzi. Mtu gwiji wa kila jambo na mtu ambaye wote humtukuza na kumthamini kwa kile anachosema.
Mzee Bomani, kama ambavyo nilipenda kumwita nikikutana naye, ama nyumbani kwake, ofisini au katika vikao vya Wasukuma wa Mwanza wanaoishi Dar es Salaam, amekufa akiwa bado anahitajika na umma wa Watanzania.
Ni mzee ambaye amekuwa akipigania ‘kufa’ kwa ushirika na hadi anakwenda kaburini alishindwa kuelewa sababu zote zinazotolewa kwa kukosekana kwa na ushirika wenye nguvu.
Hakupenda kuwa mnafiki wa nafsi yake na ndiyo maana kila akiulizwa imani yake kuhusu kutokomezwa kwa umasikini Tanzania, Mzee Bomani alikuwa na majibu mafupi tu mawili; kilimo na ushirika.
Majibu hayo yana maana pana mno endapo yanapata mchambuzi makini. Yeye hakupenda kuchambua, alikuwa akiwaachia wanaomwuliza kujikita katika tafakuri ili kupata maana halisi ya maneno yake.
Lakini, kitu kikubwa alichokuwa akikisisitiza Mzee Bomani ni kwamba kuboreshwa kwa kilimo, hasa kile kisasa kutakuwa chachu ya kupatikana kwa mazao mengi ambayo yatauzwa kwa bei nzuri na kuwa mlango wa wakulima kujikomboa na janga kubwa la umasikini.
Wakulima lazima wahakikishiwe mazao yao yanakuwa na bei nzuri na wanalipwa kwa wakati, alisisitiza Mzee Bomani ambaye wengine walikuwa wakimwita ‘Mzee Ushirika’ kutokana na kuwa na imani kubwa katika mfumo huo.
Mzee Bomani amekua katika ushirika. Ameoa katika ushirika na umaarufu wake kwa kiasi kikubwa ulitokana na ushirika.
Na siyo yeye pekee aliyeweza kuelezea manufaa ya vyama vya ushirika, bali idadi kubwa ya Watanzania ambao waliungana katika maeneo wanakotoka na kuunda ushirika wenye nguvu kuanzia miaka ya 1950 hadi miaka ya 70.
Katika kipindi hicho, Ushirika wa maeneo ya Mwanza, Bukoba na Kilimanjaro ulikuwa na nguvu kubwa hata kuwa tishio kwa watawala wa mwisho wa Tanganyika kwamba ilikuwa njia ya kuunda umoja wenye siasa iliyojificha ili kupambana na utawala wao.
Mzee Bomani ndiye alikuwa kinara wa ushirika wa Mwanza ukijulikana kwa jina la Victoria Federation of Cooperative Unions Ltd. Hapa alitumia mwanya huo wa uongozi kuwahamasisha wakulima kulima pamba kwa wingi na kuhakikisha kwamba inauzwa katika vyama vya ushirika kwa bei kubwa.
Mara baada ya uhuru, alikuwa miongoni mwa mawaziri wa kwanza wa Tanganyika huru akiwa Waziri wa Maliasili na Ushirika, akishughulikia pia kilimo. Kuchaguliwa katika nafasi hiyo kulitokana na mwanga wake katika masuala ya ushirika nchini.
Ni kutokana na jitihada zake hizo za kutetea ushirika, Mzee Bomani aliweza kupata fursa ya kuwa Rais wa Taasisi ya Dunia ya Wakulima wa Pamba.
Mbali na ushirika, alipenda sana kuona mila za Watanzania zinatunzwa na kuenziwa kwa manufaa ya kizazi kilichokuwepo na hata kitakachokuja. Katika hili, alihimiza kuanzishwa kwa Umoja wa Wasukuma.
Akiwa Rais wa umoja huo, Mzee Bomani alihakikisha kwamba Wasukuma wote wanazifahamu taratibu zilizokuwepo kale na jinsi wazee wa kabila hilo walivyokuwa wakiishi.
Kutokana na utumishi wake uliotukuka, aliweza kushika nyadhifa nyingi katika serikali ya Tanganyika na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Miongoni mwa nafasi hizo ni Waziri wa Fedha:
Akiwa katika nafasi hii, Mzee Bomani aliweza kufanikisha kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Afrika Mashariki, jambo ambalo lilisaidia kwa kiasi kikubwa kukomaza jumuiya hiyo, ingawa baadaye ililegalega na hatimaye kuvunjika mwaka 1977.
Akiwa Waziri wa Biashara, Viwanda na Madini, aliweza kusukuma mawazo ya kuanzishwa kwa kiwanda cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro, ambacho hadi leo kinafanya kazi kwa ubia.
Mzee Bomani akiwa Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa aliweza kuishawishi Marekani na nchi zingine kuanza kuelewa maana ya ukombozi wa nchi nyingi za Afrika zilizokuwa zikitawaliwa kimabavu na wakoloni.
Ni msimamo huo uliowezesha, kwa njia moja ama nyingine kupatikana kwa uhuru wa nchi za Msumbiji, Angola, Zimbabwe na baadaye Namibia.
Aliyoyafanya Mzee Bomani ni mengi, lakini inatosha kusema tu historia ya Tanzania haiwezi kukamilika ikiwa jina la Mzee Bomani halitatajwa kutokana na wingi wa mazuri yake.
Hivyo ndiyo nilivyomfahamu Paul ‘Kishamapanda’ Bomani
HISTORIA YAKE
Mzee Bomani alizaliwa Januari Mosi, 1925 katika kijiji cha Ikizu, Musoma na kuanza darasa la kwanza katika shule ya Msingi ya Wasabato ya Nassa iliyoko wilaya ya Magu, mkoani Mwanza mwaka 1939.
Ilipofika mwaka 1945, Mzee Bomani alipata nafasi ya kusoma Chuo cha Ualimu cha Wasabato cha Ikizu, kabla ya kwenda kusomea Stashahada ya Ualimu nchini Uingereza katika Chuo cha Loughborough, kilichopo Leicester mwaka 1954.
Baadaye mwaka 1976, Mzee Bomani alijiunga na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Baltimore, nchini Marekani akisomea uhusiano wa kimataifa kabla ya kuingia tena katika duru za kazi za serikali.
Hadi anafariki, jana Aprili Mosi, mwaka huu, Mzee Bomani ameacha watoto tisa, wajukuu kadhaa na vilembwe.

Thursday, March 31, 2005

Ngasongwa wangu maskini!

Jamani,
Yaani huyu Ngasongwa amenishangaza kweli, ilikuwa achukue fomu ya kugombea Urais kupitia Chama chetu, lakini akaingia mitini.
Tuakamsubiri kwamba labda anasubiri mkewe ama mtoto wake ndo asindikizane naye, lakini wapi...hadi sasa bado hola! Hatujui nini kinatokea.
Hadi sasa zimebaki siku kama 14 tu iwe mwisho wa kurejesha fomu, sasa sijui ataweza au namna gani. Tusubiri, ingawa matumaini kwamba atachukua fomu yanaendelea kufifia.
Sina uhakika amekumbwa na maswaibu gani.
Tuko pamoja nitawaeleza. Kitakachotokea.

Unafiki huu utabebwa kwa mbeleko gani?

HIVI sasa sehemu kubwa ya nchi yetu imegubikwa na gumzo kuhusu nani ataibuka kuwa mshindi katika kinyang'anyiro cha kiti cha urais kwenye uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Mazungumzo ofisini, hasa ofisi za serikali ambako bado kuna muda wa gumzo, kwenye migahawa, baa na maeneo mengine ya mapumziko na hata njiani; mjadala ni nani kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yule wa Zanzibar.
Kila mmoja anazungumza lake, huku akieleza zaidi kuhusu mgombea anayetamani aongoze nchi kwa miaka mitano au 10. Huyu anatoa sifa kemkem za mgombea wake, nyingi zikiwa za kumpamba ili aweze kuwavuta wengine kumuunga mkono
Sifa zinazotolewa na mashabiki wao, nyingi siyo 'nguo' sahihi za hao wanaotamani kukalia kiti cha enzi cha Tanzania. Wengi hawawezi hata kutanabaishwa kwa maneno na matendo yao.
Wanaotangaza kugombea, wote tunawafahamu nyendo zao za mchana na hata usiku, lakini wapambe wao wanasahau hayo na wanaendelea kupayuka kana kwamba mgombea wanayemtamani hana mawaaa ya tabia, mawazo wala maungo yake. Kwao mgombea wao ni safiiiii!
Hilo ni kundi moja kati ya kundi kubwa la wapambe ambalo limeibuka baada ya Chama Cha Mapinduzi kuwatangaza waliochukua fomu kukiomba Chama kuwateua ili wakiwakilishe katika uchaguzi kwa nafasi ya Rais.
Kuna kundi jingine la watu ambao kwao kila mgombea anayejipitisha mbele ya nyuso zao ni wao. Hawa hawana msimamo. Hawa ni wanafiki. Hawa ni mbwa mwitu ambao wanavaa ngozi za kondoo, lakini kubwa zaidi ni watu wasiokuwa na 'udhu'. Ni watu ambao Waingereza wanawaita 'Opportunists'.
Hawa wapo tu kwa kila mmoja, hawana uchaguzi. Ni sawa na wachezaji wa kamari. Hawana uhakika na mgombea wanayemsimamia. Kwao kila anayejipitisha wanakenua meno hadi magego yanaonekana.
Wao kazi kubwa ni kuonekana wakitabasamu na kucheka hata kama mgombea anayehitaji ridhaa ya vikao vya Chama ameongea jambo lisilochekesha ama kuwa na chembe ya kufurahisha
Hawa ni wale ambao kila mgombea anayewafikia wanaonekana kunawa viganja na vidole vyao, kana kwamba wanajiandaa kula ugali wa Kisukuma; kwamba wanavuta pumzi ili kazi ikianza wawe na misuli iliyosimama kuuvamia ugali mgumu unaovaa gamba baada ya muda mfupi mara unapopakuliwa chunguni.
Kunawanawa mikono ni unafiki ambao hauna mfano, wao hawana uhakika na uchaguzi wao, wanaona heri kuwa na wote kwa kuwa miongoni mwao mmoja lazima aibuke mshindi ambaye watajidai ni wao!
Wanadai kujiweka katika 'safe side' ili kama ataibuka 'kidedea' basi awe wao na ili aweze kuwafikiria katika 'ufalme' wake unaokuja baada ya Oktoba 30, mwaka huu.
Kauli kubwa inayotolewa na midomo yao ni 'tutakupa mzee-usiwe na wasiwasi'. Hii ni kauli ambayo hadi sasa wameitoa kwa wanaotarajia ridhaa ya Chama kupitishwa ambao idadi yao imefikia 11.
Karibuni nilifurahishwa na kauli ya Mkuu wa Mkoa mmoja ambaye alitangaza hadharani kwamba anampigia debe mgombea fulani. Huyu, kama alinukuliwa sahihi, hana unafiki na anaeleza kile midomo yake kinachopokea kutoka kwenye nafsi yake. Yuko tayari kwa matokeo yoyote na wala hakuona haya kutamka aliyotamka.
Kiongozi huyo alionyesha njia na wengi tukadhani kwamba atakuwa mfano wa kuigwa, kumbe wapi! Unafiki ndio kwanza unashika kasi kubwa. Kila anayepita kuomba wadhamini anaelezwa na viongozi wa eneo analotembelea maneno yale yale aliyozoea kuyasikia katika mikoa aliyofanya kazi ya kukusanya wadhamini
Kumbe basi, kwa maana hiyo na kama itafanyika tathmini, itaonekana wagombea wote watapitishwa na wapiga kura katika vikao mbalimbali. Lakini ukweli ni kwamba kura ni siri ya mtu na ataipiga akiwa mwenyewe, na lazima apatikane mmoja tu atakayesimama kugombea urais.
Pamoja na kwamba kauli za namna hiyo za –tutakupa mzee- zinaonyesha kwamba wagombea wote ni safi, lakini zimejaa unafiki wa ajabu, ambao ukichunguzwa ni sawa na dhambi nyingine yoyote ya kunena uongo.
Sasa kauli za -tutakupa mzee- zisiwavimbishe vichwa wagombea wote na kuona kwamba tayari wamekalia kiti cha enzi cha Tanzania. Bado kazi ni kubwa na watakaoshindwa wala wasiwanunie wale waliowaeleza kwa kwamba -tutakupa mzee!
Ni kweli ni kauli za kutia moyo, lakini sasa wagombea watakaposhindwa wasigeuke mbogo na kudai kuwepo kwa mizengwe kwa kuwa tu walipiga hesabu zao na kubaini kuwa wajumbe wote wamewahakikishia- 'tutakupa mzee'.
Wagombea wote wajue kuwa katika hiyo kauli ya 'tutakupa mzee' kuna unafiki ambao anayeitoa anakuwa na malengo yake, mengi yakiegemea kwenye ubinafsi zaidi badala ya hali halisi.
Inawezekana kabisa hawa wanafiki hawa ndio wakawa chanzo cha kuibuka kwa chuki miongoni mwa wagombea. Hivi ni mgombea gani atakubali kwamba ameshindwa vibaya ikiwa ‘diary’ yake inaonyesha alikuwa akiungwa mkono na idadi kubwa ya wajumbe wa mikutano husika waliomhakikishia –tutakupa mzee!
Kama wapiga kura wanahitaji kupata heshima kutoka kwa wananchi na thawabu kutoka kwa Mungu, ni vyema wakasimama katika ukweli na kuachana na 'tutakupa mzee' wakati wakijua kuwa hawatatoa kura kwa mtu ambaye hafai kuwa kiongozi wa nchi.
Nina uhakika kuwa kila binadamu awaye yoyote ana utashi na matamanio yake, kwa maana hiyo kila mmoja ana mgombea anayetamani awe kiongozi wake, lakini anaogopa kutamka hadharani kwa kuogopa mtu wake kushindwa na kupata aibu.
Mwanazuoni mmoja wa Marekani, Bernard Malamud, aliwahi kutamka kwamba ni heri wenye kueleza ukweli wa wazi na wakaonekana wabaya, kuliko wanaoeleza unafiki na kuonekana wazuri, kumbe moyoni wamejaa ubinafsi.
Malamud anaeleza kuwa hawa ndiyo huipeleka jamii katika maisha magumu kwa kuwa walionyesha unafiki ambao mara nyingi hauna mwisho mzuri, kwani hubainika baada ya muda hata kama muhusika atakuwa ameingia kaburini.
Hivi nini kinashindikana kuwa wakweli na badala yake watu ‘wanakalia’ unafiki ambao 'udhu' wake haudumu kwa muda mrefu?
Hawa wanaofanya unafiki wa namna hii, wakiwachaganya na kuwarubuni wagombea tuwabebe kwa mbeleko gani ili kuwafikisha kwenye ukweli, uwazi na usafi ambao ni silaha kubwa ya demokrasia na maendeleo?
Tubadilike sasa, inawezekana.

Wednesday, March 23, 2005

Mishahara ithaminishwe kwa soko la fedha

MAANA halisi ya neno mshahara, kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ni fedha anazolipwa mtu kila mwezi kwa kazi aliyoajiriwa kufanya.
Katika mazingira ya Tanzania, mishahara ya waajiriwa wengi hutolewa mara moja kwa mwezi, aghalabu kila tarehe ya mwisho ama mwanzo wa mwezi unaofuata.
Lakini basi, katika mataifa mengine, kama Afrika Kusini na Swaziland, waajiriwa hupokea mishahara yao kila inapofika mwisho wa wiki; Ijumaa.
Katika hali ya kawaida, wafanyakazi ama waajiriwa hutegemea mno malipo yao ya kila mwezi kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku pamoja na familia zao kwa matumizi mbalimbali.
Mishahara ndiyo kipato halali kinachokubalika kwa waungwana, ingawa wapo wafanyakazi wanaoishi kwa kupata mapato ya ziada kwa njia haramu.
Hao wenye kutegemea njia nyingine haramu hufanya hivyo kutokana na kupata mwanya wa kutumia nafasi walizonazo kupata ziada kwa njia za rushwa; lengo lao likiwa ni kuishi maisha ya ukwasi kinyume na mapato yao halali.
Wenye tabia za kupenda kupata mapato yasiyokuwa rasmi, kwa maana ya haramu ndio wanaonekana kuwa na majumba ya kifahari, kusomesha watoto wao nje ya nchi ambako hulipa gharama kubwa, ndiyo hao wanakuwa na hisa kubwa katika kampuni za ndani na hata nje ya Tanzania.
Ama kwa hakika kila mmoja anapenda kuwa na maisha mazuri ambayo yatampa uhuru wa kuchagua ale nini, avae nini, asomeshe watoto wake wapi na kwa gharama gani na atumie chombo gani cha usafiri.
Hata hivyo, kutokana na kubanwa kwa mishahara kutoka kwa waajiri, watu waungwana wasiokuwa na tamaa, wamekuwa wakiishi maisha yanayoonekana kabisa kujaa huzuni hata kama tunakutana nao mijini wakiwa wamefunga tai na kuvaa nguo zinazong'aa na kuvutia.
Idadi kubwa ya waungwana hao wana maisha magumu. Sababu ya kuwa na maisha ya namna hiyo ni kulipwa ujira mdogo usioendana na soko halisi la fedha kwa wakati husika.
Ikumbukwe kuwa waajiri hawana taratibu za kupandisha mishahara mara kwa mara. Wao husubiri kumalizika kwa mwaka mmoja, miwili au hata mitano. Wao wanachoangalia zaidi ni mwajiriwa wake amezalisha kiasi gani.
Kushuka kwa thamani ya shilingi kwao hakuna maana zaidi ya kulalamikia malighafi, gharama za usafiri kuongezeka na masuala mengine yanayohusu uzalishaji wa bidhaa zao ama utoaji wa huduma wanazofanya.
Ni mara chache mno kusikia mwajiri akilalamikia mishahara midogo ya watendaji wake na labda kuwashirikisha ili kufikia muafaka wa kulipwa kiasi kinachoweza kuwafanya kuishi maisha wanayotaka.
Ieleweke kuwa thamani ya fedha zetu (na za nchi nyingi tu duniani) huthaminishwa kwa soko la fedha kwa maana ya mlinganisho na dola ya taifa kubwa na tajiri la Marekani.
Kiwango cha ubadilishaji hutegemea uimara wa fedha hiyo ya Marekani. Ikiwa thamani yake imeimarika, basi fedha za madafu kama zetu thamani yake inakuwa kubwa zaidi na ikitetereka, shilingi inapanda kidogo.
Ingawa kwa kiwango kikubwa dola ya Marekani huimarika kila baada ya muda mfupi, hata saa nne na chini ya hapo.
Kuimarika kwa dola ya Marekani kuna maana kwamba bei ya bidhaa nyingi kutoka katika nchi hiyo au nchi nyingine zinazouza bidhaa na huduma zao nje huongezeka na kufanya bei ya bidhaa hizo zinapoingia nchini kuuzwa kwa bei ya juu zaidi.
Hali hiyo haionwi na waajiri wengi na wafanyakazi huendelea kuwa na kiwango kile kile cha mishahara hata kama uimara wa dola umeongezeka na kufanya bei za bidhaa na huduma kupatikana kwa kiwango cha kutisha kwa thamani ya shilingi zetu.
Ni kutokana na hali hiyo, kampuni nyingi za nje na hata taasisi zetu za serikali na binafsi zimekuwa zikitoa mishahara kwa thamani ya soko la fedha kwa maana ya kutumia dola ya Marekani kulipa wale wanaoitwa Ma-TX.
Tunao wataalamu wa kigeni kama hao katika wizara na idara zetu za serikali ambao wanalipwa kwa kutumia nguvu ya soko la fedha. Na hali hiyo inawafanya kuwa na maisha mazuri kuliko hata huko kwao wanakotoka zaidi ya watendaji wenye uwezo sawa na wao wenye ngozi nyeusi.
Pamoja na kwamba wapo wanaolipwa na wafadhili wa miradi ya nje, lakini nao pia wamekuwa wakipokea ujira wao kwa nguvu ya soko la fedha na ndiyo. Mishahara yao na marupurupu mengine huchukua sehemu kubwa ya fedha za miradi hiyo na hata mikopo.
Kutokana na hali hiyo, Rais Benjamin Mkapa amewahi kuwaeleza wafadhili wetu kwamba wanalipa wataalamu wanaowaleta kutoka kwao fedha nyingi mno ikiwa ni mishahara, kiasi kwamba asilimia kubwa ya kukamilisha miradi inabaki mifukoni mwa wataalamu hao wanaoishi maisha ya ukwasi wa kutisha.
Ni vyema kiongozi ajaye, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akawa na sera mpya ya kukwamua hali duni za wafanyakazi kwa kuanza kuwalipa mishahara kwa kutumia nguvu ya soko la fedha lililopo. Ikiwa wafanyakazi wataneemeka, basi ni dhahiri kwamba hata wananchi wengine wote watafaidika katika mzunguko wa fedha utakaokuwepo.
Hapa sina maana kwamba kila nguvu ya dola inapoimarika, basi mishahara ibadilishwe, la hasha, bali kuwepo kwa mlingano wa dola ya Marekani na malipo ya kila mwezi angalau kuwawezesha wafanyakazi kupata mishahara itakayoweza kukidhi mahitaji yao ya lazima.
Mlingano huo unapaswa, angalau kuwa karibu zaidi na gharama za mahitaji ya mwezi kwa mfanyakazi, hii ikiwa ni pamoja na yeye, mke au mume na watoto angalau watatu. Gharama hizi ni nyumba, chakula, usafiri, matibabu, elimu na hata dharura.
Katika hali ya kawaida, maisha ya wafanyakazi wengi wa Tanzania ni mabaya na hakika maslahi yao yanapaswa kuangaliwa upya.
Malalamiko ya wafanyakazi yamekuwa mengi, lakini kubwa ni kiwango kidogo cha mishahara, hasa kima cha chini (sh. 48,000 sawa na dola za Marekani 48 tu kwa mwezi), kiasi ambacho hakiwezi hata kutosheleza maisha ya wiki moja ya mtumishi wa umma mwenye familia ya watu wanne. Je, wanaishi vipi kwa wiki zingine tatu?
Ikiwa wafanyakazi watalipwa ujira kulingana na soko la fedha lililopo, ni wazi kuwa tija itaongezeka na hata rushwa kupungua
Sasa ni wakati muafaka kwa kiongozi yeyote atakayeingia Ikulu kuhakikisha kwamba anawaondolea manung'uniko wafanyakazi wa Tanzania juu ya mishahara midogo ambayo haitoshelezi wao kuwa na maisha mazuri.
Inawezekana kuwa na Tanzania yenye watumishi wenye neema na wananchi wote kwa ujumla.

Thursday, March 17, 2005

Ngasongwa Rais wa Tanzania

Jamani,
Nimepiga hesabu zangu na sasa naona napata jibu sasa; kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne ni Juma Ngasongwa.
Huyu kwa sasa ni Waziri wa Viwanda na Biashara.
Huyu bwana, nimeona dalili zote, sina ujuzi wa Sheikh Yahya, lakini inawezekana kabisa akawa yeye. Dalili hizo kwa sasa nazificha kwa manufaa yangu na watu wangu.
Lakini, hadi leo hajachukua fomu. Ilikuwa achukue jana, lakini hakutokea kwa Mangula kuzipokea na alisubiriwa hadi watu wakakata tamaa, wakaondoka kwenda makwao na wengine kuishia kwenye vibanda vya nyama choma na bia.
Haya tusubiri. Akichukua nawajulisha mapeeema na kuwapa dalili nilizozificha kwa sasa
Kila heri kwake na wengine wote waliochukua fomu

Nani kasema vyuo vikuu ni kwa wawekezaji tu?

SIKU kadhaa zilizopita nilielezwa habari kwamba kiongozi mmoja rafiki yangu aliandika barua kwa uongozi wa chuo kikuu akieleza kusikitishwa kwake na kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa ‘kushindwa kwa wahitimu kuwaridhisha wawekezaji.’
Mheshimiwa huyo alieleza mengi akionyesha kwamba mambo mengi yaliyokuwa yakisaidia wao kuonekana wana uwezo wakati wakisoma vyuoni, sasa hayapo na kwamba wanafunzi wengi wanaohitimu vyuo vyetu vikuu sasa wanashindwa kujieleza kwa lugha ya kigeni wanapopata fursa ya kusailiwa na kampuni ama idara zinazodhani kuwa lugha hiyo ndiyo yenyewe! Hakuna tena nyingine, kwamba bila hiyo hakuna ajira, hakuna maendeleo na wala hakuna amani.
Hao nadiriki kueleza kwamba wamepotoka. Hawajui. Ni waongo na wanaonekana kuwa wanafiki wakubwa kwa kushindwa kuwatendea haki Watanzania wenzao.
Inawezekana kabisa kiongozi huyo ninayemheshimu sana, alipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wawekezaji ambao walimweleza kusikitishwa kwao na jinsi wahitimu wa vyuo vyetu vikuu wasivyoweza kumudu kuongea Kiingereza kwa ufasaha.
Mbali na mawazo hayo, mwanazuoni mwingine hivi karibuni alinieleza kwamba hakuna wanafunzi wenye uwezo mkubwa kitaaluma kama Watanzania, isipokuwa wamekuwa wakikwaza na lugha inayotumika. Kimsingi, alieleza kuwa hali hiyo inatokana na kukosa misingi mizuri ya matumizi ya lugha za kigeni kuanzia nyumbani na kufundishwa kwa kiwango cha chini katika ngazi za awali.
Sina ugomvi na mwanazuoni huyu wa mwisho, lakini siungi mkono kabisa mawazo ya kiongozi ambaye inaelekea anataka kuwaeleza Watanzania kwamba vyuo vyetu vinavyotoa elimu ya juu vipo tu kwa ajili ya wawekezaji wenye kukitukuza zaidi Kiingereza.
Kiongozi huyo anasahau kabisa kwamba kuanzishwa kwa vyuo hivyo ni tofauti kabisa na mawazo yake. Anasahau kuwa vyuo vilianzishwa kwa lengo kubwa la kupatikana kwa wataalamu wa kusaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali; za uchumi, elimu, sheria, sayansi, mifugo, siasa na maeneo mengine.
Mbali na kupata wataalamu wa maeneo yanayochochea uhuru zaidi na maendeleo zaidi, wahitimu wa vyuo vikuu tunawatarajia kuwa ‘wachokozi’ wa hoja za kujenga kwa kuwa tunaamini kwamba wana ufahamu mpana wa mambo mengi.
Kwa maana hiyo basi, wahitimu wa vyuo vikuu tunataka wawe vyanzo vya tafakuri jadidi ambazo zitasaidia kujenga mfumuko imara wa mawazo na mtazamo murua wa makubaliano yatakayokwenda sambamba na namna ya kuondoa umasikini, ufisadi, ujinga na mambo yanayofanana na hayo kwa watu wetu.
Sasa anapoibuka kiongozi akipiga kelele kwamba wahitimu wa vyuo vikuu hawaelewi Kiingereza tumwelewe namna gani?
Hivi ikitokea kwamba wawekezaji wengi ni wafanyabiashara kutoka Bara Hindi; kwa mawazo yake kiongozi huyo atapendekeza vyuo vyetu vikuu vifundishe Kigujarat. Ikitokea wawekezaji ni kutoka Uchina, basi vyuo vifundishe Kichina na ikitokea wawekezaji wengi wanatoka Japan, basi wanavyuo wajifunze Kijapani.
Sina hakika kwa mtazamo wa bwana mkubwa huyo nchi hii itafikia mahali kuwa na maendeleo tunayohitaji ikiwa wengi watakuwa na mawazo hayo; kwamba wahitimu wetu wawepo kwa ajili ya wawekezaji tu.
Ni mtazamo wake huo unaotaka tuwe na picha kwamba wahitimu wetu hawaelewi wanayofundishwa? Je walipataje shahada zao? Au anataka kutulazimisha tuamini kile kinachoelezwa kuwepo kwa upendeleo katika utoaji wa viwango vinavyotakiwa ili mwanachuo kuhitimu vyema na hatimaye kupata shahada yake!
Mbona idadi kubwa ya wanavyuo waliomaliza kabla ya kuwepo wawekezaji ndiyo hao hao leo wanaendelea kufanya kazi za umma na kusaidia hata maendeleo yanayoonekana kuwepo kwa sasa.
Huyu kiongozi anataka kutuambia kwamba kiwango chake cha kujua wahitimu bora ni kuzungumza maneno kama chiriku kwa kutumia lugha ya kigeni? Je hao anajua walikotoka, wamesoma wapi a familia zao ziko namna gani.
Huenda ikawa wanavyuo wengi wametoka katika shule za kawaida ambako mafunzo ya lugha ya Kiingereza, mbali na kutozingatiwa zaidi, hata waliokuwa wakiwafundisha katika elimu za awali; msingi ni wale waliokuwa walimu wa UPE.
Katika mazingira ya namna hiyo, huyo kiongozi anatarajia kuwa na wanavyuo wangapi ambao wanaongea kama chiriku lugha ambayo siyo yao. Lugha ambayo mwanafunzi akitoka tu darasani, tena anapomaliza kipindi mwalimu wa somo hilo, basi yes…yes…yes…zinakufa hadi kipindi kingine.
Imani yangu, kama ilivyo kwa wengi ni kwamba wanavyuo wetu wengi wanaelewa na kufahamu wanachofundishwa ama kukifanya kwa kutumia lugha ya kigeni, lakini wanakwama kuwa wabwabwajaji wazuri wa lugha hiyo ya kigeni kutokana na nilichokieleza awali.
Hali ya namna hiyo ndiyo inayofahamika kwa wengi, na ndiyo maana hata viongozi wetu wa kitaifa wanapotaka kuwasilisha hoja zao vyema kwa Watanzania hawatumii lugha ya kuazima. Wanahofia kuwepo kwa kutokuelewana na kutofikisha ujumbe sahihi kwa walengwa.
Najua wapo viongozi wetu wengi tu wenye mawazo ya kuona kwamba Kiingereza ndiyo chenyewe! Hivi ni lini hawa wataachana na mawazo kama ya mwezao na badala yake wawe na inami kwamba wanavyuo wanapohitimu wanatakiwa kuwa mwanga wa ushirika na wananchi wengine katika kuibua maendeleo zaidi, tena wananchi wengi wakiwa maeneo ya vijijini?
Nani kawaroga hawa na kuwapandikizia mbegu mbaya akilini mwao kwamba elimu kwa wakulima na wafugaji wetu vijijini itatolewa na wale wanaojua Kingereza tu. Wanasahau kwamba wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria, elimu ya kujikinga na magonjwa na kufuta ujinga itatolewa tu na wale wenye ufahamu mkubwa wa kupepesa kingo za midomo yao kwa Kiingereza.
Mawazo ya kingozi huyo yananikumbusha kichekesho kingine ambacho kiliniacha ‘hoi’ kwamba taasisi za kuendeleza Kiswahili zinapotoa taarifa zake kwa umma zinaandika kwa lugha ya kukopa; Kiingereza! Na wanaowaandikia ni Waswahli wenzao. Inasikitiha na kushangaza kweli!
Hivi kweli katika hatua za namna hii kuna nia ya kukuza Kiswahili chetu, ama tunadanganyana tu kwa mbwembwe ambazo zinawapendezesha zaidi wawekezaji na Wazungu wengine huku tukisahau kabisa kinachotakiwa kufanywa kusaidia lugha yetu na maendeleo yetu kwa ujumla?
Iwapo nchi itaendelea kuwa na watu wetu wenyewe ‘wanaokiponda’ Kiswahili, bado safari ya maendeleo itakuwa ndefu mno na mwisho wake kuwa mbali tofauti na tunavyofikiria.
Tunaowatarajia kukitetea Kiswahili wanashindwa kutekeleza majukumu yao ingawa wanajua kwamba muda utafika na wenye mitazamo sahihi wataamua kwamba lugha yetu ndiyo mhimili wa maendeleo yetu na siyo vinginevyo.
Hebu tujiulize, ni nchi gani ambayo leo hii inafurahia hatua kubwa za maendeleo kwa kuwa tu zilitumia lugha za kukopa?
Hivi tunasubiri hata hili nalo tufundishwe na Bill Gates ambaye, pamoja na kutaka soko la wanaozungumza Kiswahili kwa ‘zana’ zake za kompyuta, lakini pia anafanya kazi ya kukuza lugha ambayo inaonekana kukua kwa kasi, bila kujali unafiki wa watu wetu.
Kiswahili oyeeee.

Thursday, March 10, 2005

Matokeo ni kipimo cha Watutsi

MWISHONI mwa wiki iliyopita, wananchi wa Burundi waliyapokea matokeo ya kura ya maoni waliyopiga mwishoni mwa Februari, mwaka huu kwa furaha kubwa.
Furaha yao ilitokana na ukweli kuwa walichotazamia ndicho kilichotokeo, kwamba wengi walikubaliana na utaratibu wa kuwa na Katiba mpya ambayo kimsingi inaonekana kuwa 'dawa' ya kumaliza tofauti zao na hatimaye kukomeshwa kabisa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimemaliza uhai wa idadi kubwa ya watu na kufifisha maendeleo ya nchi hiyo.
Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 300,000 wamekufa nchini humo katika mapigano na uhasama wa wenyewe kwa wenyewe ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 12.
Inaonekana kuwa waliojiandikisha walikuwa milioni 3.1, na kwamba asilimia 88 ya idadi hiyo walijitokeza kupiga kura hiyo ya maoni huku asilimia 90 ya idadi hiyo ikipiga kura za ndiyo kwa Katiba mpya.
Matokeo ya kura hiyo yana maana kwamba sasa kutafanyika uchaguzi wa amani ambao utakuwa wa kidemokrasia zaidi, badala ya kushuhudia 'uchafu' mwingi kama uliokuwa ukijitokeza katika uchaguzi uliopita. Uchaguzi wa wabunge unatarajiwa kufanyika mwezi Aprili, mwaka huu.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vinatokana hasa na uhasama wa kikabila baina ya Wahutu ambao ndiyo wengi na Watutsi wanaowakilisha jamii ndogo.
Wahutu wanatajwa kuwa asilimia 85 ya Warundi wote, Watutsi asilimia 14 na idadi inayobaki inagawanywa kwa makabilia madogo madogo yaani asilimia moja tu. Burundi ina watu karibu milioni saba.
Katika Katiba mpya, Wahutu watakuwa na wabunge asilimia 60, huku Watutsi wakipata wabunge asilimia 40 ya wabunge wote. Kunatarajiwa kuwa na wabunge 200.
Mbali na idadi hiyo ya wabunge, pia Katiba hiyo inaeleza wazi kwamba nafasi za juu za uongozi jeshini zitagawanywa kwa idadi sawa miongoni mwa maofisa waliopo wa makabila hayo. Ingawa ukweli ni kwamba hadi sasa wapo Watutsi wengi wenye vyeo zaidi ya Wahutu. Kwa hiyo, inawezekana kabisa Wahutu wakapandishwa kwa wingi kufikia vyeo vinavyotakiwa.
Mengi yanaweza kuelezwa kutokana na makubaliano hayo, kubwa likiwa kwamba je Watutsi kweli watakubaliana na Katiba hii mpya au wamesukumwa tu kimkumbo na Wahutu ambao ni wengi?
Swali hili ndilo litakaloulizwa na wengi, hasa wasiopenda matokeo yaliyopatikana. Matokeo hayo, pamoja na ukweli kwamba ni nguvu ya Wahutu kwa kuwa wako wengi, lakini yanaonyesha jinsi kundi la watu hao lisivyokuwa na uchoyo wala uchu wa madaraka. Limeamua kugawana na kaka na dada zao ili kuleta amani.
Wengine watasema, ikiwa ni demokrasia ndiyo lengo hasa la kura ile ya maoni, kwanini misingi ya mfumo wa uchaguzi wa demokrasia usichukue mkondo wake bila kujali idadi ya watu? Hii ina maana kwamba kila mtu awe na kura moja na kusiwe na ulazima wa kujali makundi ambayo yanapendelewa, kama inavyoonekana sasa kwa Watutsi.
Historia inaonyesha kwamba Burundi kama ilivyo Rwanda, ina idadi ndogo ya Watutsi, lakini ndio wenye sauti na wasiopenda kuona kundi jingine likiongoza. Mifano ya hali hii ipo na ndiyo ukweli. Watutsi wao wanajiona na kujithaminisha kwamba ni 'wateule'; kazi yao kubwa ikiwa kuongoza makundi mengine.
Lakini basi, matokeo ya kura hiyo ya maoni pamoja na mgawanyo wa madaraka unaotakiwa kufuatwa na Katiba hiyo, ni tunu kwa wapenda amani wote, hasa Waafrika wenyewe wakiongozwa na Tanzania.
Ikumbukwe kwamba Tanzania ndiyo nchi ya kwanza iliyobeba mzigo mzito wa kuwasuluhisha Warundi, kazi iliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (Mungu amumweka mahali pema) na baadaye kuchukuliwa na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela ambaye naye alimpa majukumu Makamu wa Rais wa nchi yake, Jacob Zuma.
Wote hao kwa njia moja wamekuwa wakipigania amani kutawala nchini humo kwa kujua kwamba Afrika ni moja na watu wake ni ndugu. Viongozi hao wenye kutukuka wameendelea kuwa na imani kwamba migogoro ya Afrika itatatuliwa na Waafrika wenyewe bila kusubiri 'wajomba' kutoka Marekani na Ulaya.
Wapenda amani wote watafarijika zaidi kuona Watutsi sasa wakiaachana na mawazo kwamba wao ndiyo nguzo ya uongozi na kukubaliana na utaratibuu uliopendekezwa katika Katiba mpya ya Burundi yenye mtazamo wa kuleta, siyo amani tu, bali maendeleo endelevu ya nchi hiyo.
Dunia itawashangaa mno Watutsi watakaposimama dede tena wakianzisha mapinduzi kwa lengo tu la kutaka wao waongoze.
Katiba ya sasa ya Warundi haina kinyongo na mtawala yoyote awe Mtutsi ama Mhutu, lakini kikubwa ni kwamba wote wafuate matakwa ya Katiba na mtazamo wa wananchi wote bila kujali makundi.
Kuwepo kwa wanachama wa Kitutsi katika chama cha FRODEBU chenye idadi kubwa ya Wahutu na kuwepo kwa Wahutu kwenye chama cha UPRONA ambacho kina Watutsi wengi ni budi kuendelezwa na kuchukua sura ya Katiba mpya ambapo umoja na mshikamano utaongezeka na kuimarika kwa mema ta Burundi na Afrika kwa ujumla.
Kuwepo kwa mchanganyiko wa wanachama wa makabila hayo makubwa ni dalili njema ambazo hakika zinapaswa kuendelezwa na ikiwezekana kuondoa chembe za ubaguzi ndani ya vyama vyote 21 vya siasa vyenye usajili nchini humo.
Utengano wa kikabila ukiondoka kwenye vyama, kama inavyohimizwa na Katiba mpya, kutasukuma kuondoka kwa ubaguzi katika makazi na hatimaye jamii nzima ya Warundi.
Kila kitu kinawezekana. Basi, iwezekane kwa Warundi pia. Umoja wenye nguvu zaidi upatikane na kuwepo kwa Burundi yenye mwanga wa maendeleo bila wananchi wake kuwa na wasiwasi kwa kuwa tu jirani yake ni Mhutu au kuwa na shaka kwa kuwa jirani yake ni Mtutsi.
Katiba Mpya, Mtazamo Mpya, Maendeleo Endelevu ndiyo viwe dira na silaha kubwa kwa mustakabali wa Burundi.

Saturday, March 05, 2005

Nani kawapokonya ‘moyo’ wa kuona wagonjwa?

KILA kiumbe mwenye nyama, mifupa, damu na maji mwilini anaugua, anakufa na anapata matatizo kadha wa kadha ya afya. Hakuna anayeweza kutamba kwamba yeye ni bingwa wa kukwepa ajali wala ‘kukimbia’ matatizo mengine ya kiafya.
Haijalishi wewe una mali kiasi gani. Una usomi kiasi gani na una cheo kikubwa kiasi gani katika kampuni, serikali ama katika taasisi za binafsi na hata dini.
Wote tunaugua. Tunakufa na tunapata matatizo mengi kila kukicha.
Ni kweli wapo wanaoweza kujaribu kukwepa magonjwa yanayoepukika kwa kiasi kikubwa, lakini siku ya siku hujikuta wakiwa mahututi vitandani wakijiuguza kwa malaria, ukimwi, homa na mengine yanayofanana na hayo.
Vyandarua vinatumika. Dawa za kudhibiti zinatumika. Kinga zinatumika na bila kusahau tahadhari, lakini bado magonjwa hayo na yenye ujirani nayo yanawakabili binadamu na yanaonekana kutopungua licha ya kazi kubwa zinazofanywa na serikali kutangaza namna ya kukabiliana nayo.
Inaonekana kabisa idadi ya wagonjwa wa magonjwa mengi haipungui na inaongezeka kila uchao. Takwimu nyingi zinazotolewa na wataalamu wetu wa afya hazina ukweli wa hali halisi, kiasi ambacho kinaweza kufanya watu kujipa moyo kwamba hali ni shwari, kumbe ni kinyume chake.
Vitanda vilivyoko katika hospitali zetu, zahanati na wakati mwingine kliniki vinabeba idadi kubwa ya wagonjwa. Wapo wanaougua kwa muda mrefu. Wapo wanaougua kwa muda mfupi. Miongoni mwao wapo wanaopona na kuruhusiwa na wengine hupoteza maisha.
Wagonjwa wengine huugulia na kupata tiba majumbani kwao ama kwa jamaa zao. Hawa nao kama walivyo wale wanaotibiwa hospitali, idadi yao ni kubwa na inaongezeka.
Inaonekana kabisa kwamba katika kipindi hiki ambacho madaktari wanakuwa wengi zaidi na kuwa na utaalamu mkubwa zaidi, magonjwa nayo yanaongezeka, tena yakiibuka kwa usugu mkubwa unaotisha.
Kwa hiyo basi, wagonjwa wataendelea kuwepo sambamba na kuwepo kwa idadi kubwa matabibu na vifaa vya kisasa kabisa vya kutoa nafuu kwa wagonjwa.
Nakumbuka zamani, haikuwa taabu kumsikia mtu akitoka kazini na kuaga kwamba anapita hospitali kusalimia wagonjwa. Haikuwa lazima awe na ndugu ama jirani zake kwenda kusalimia.
Wengi walikuwa wanakwenda kutoa pole kwa wagonjwa hata wasiowafahamu ama kuwa na uhusiano nao. Kilichokuwa kikifanyika ni mtembelea wagonjwa anapoingia wodini ni kuanza kusalimia wagonjwa na kuwapa pole.
Idadi kubwa walikuwa wakienda kutoa pole wakiwa na vijizawadi. Wapo waliobeba matunda, maji na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.
Mhusika alikuwa akichukua vijizawadi kulingana na uwezo wake na haikumlazimu kugawa wodi zima, bali kwa watu wachache kutegemea na uwezo wa ‘mfuko’ wake siku hiyo.
Hakika hii ilikuwa picha nyingine muhimu iliyokuwa ikielezea maisha ya Watanzania wengi ilivyokuwa. Kwamba ni watu wenye upendo, ushirikiano na kuthamini utu wa wengine.
Watu hawakusubiri wakati wa sherehe za kidini kama Krismas, Idi ama Diwali kwenda kuwaona na kuwajuliana hali wagonjwa. Ilikuwa ni kama ratiba kwa baadhi ya watu kwamba watakwenda wodini ama majumbani kwa wagojwa mara moja kwa mwezi ama tatu…nne na wengine walijiwekea utaratibu wa kila mwisho wa wiki.
Sina uhakika ni nani amewaroga Watanzania kiasi cha kuipoteza tabia hiyo adhimu ambayo hata ilifika mahali majirani zetu wakatuona ni ‘wendawazimu’ wakidai kwamba Tanzania kuna muda wa kupoteza!
Hao ndiyo walikuwa majuha kweli. Hakuna aliyewasikiliza na utaratibu huo uliendelea siku nyingi mno. Hata baadhi ya walio vijana leo waliendeleza tabia hizo kutoka kwa wazazi na walezi wao.
Haikuwa kupoteza muda. Haikuwa kupoteza fedha. Haikuwa kujipendekeza kwa mtu awaye yote. Ilikuwa ni hali ya upendo na kufuata taratibu za kistaarabu, siyo lazima za dini.
Majirani zeru hao pia walidai kwamba eti Watanzania wanaogopa kifo, kwa hiyo walikuwa kijijengea namna ya kuwa karibu na Muumba kwa kufanya mema kwani imeandikwa katika vitabu vitakatifu kwamba anayejali wagonjwa ana ongeza thawabu zake mbinguni.
Hawa nao ni ‘wakora’. Wanakuja na hoja kwamba mbona sasa hakuna watu wanaotembelea hospitali kusalimia wagonjwa. Wanadai kuwa hivi sasa watu wanaona kifo ni kitu cha kawaida. Ehhh makubwa!
Wengine wanadai kwamba hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja ni mbaya, hivyo hakuna anayeweza kuruhusu familia yake kufa njaa kwa kuwapelekea zawadi za pole wagonjwa.
Hivi nani kawaeleza kwamba kutembelea wagonjwa kunahitaji fedha. Kwani nani analazimishwa kuwanunulia matunda ama maji yake na maji ya kawaida ya kunywa. Nani?
Kinachoonekana sasa ni kurogwa. Tena kurogwa kweli. Hivi kwanini tusirejee kwenye utamaduni wetu wa kutembeleana jamani. Tuanze sasa.
Wale wachache wanaoonekana kutoa michango ama vijizawadi vyao kwa wagonjwa wanataka eti hadi kuwepo na ITV, Channel Ten, DTV, Star TV, Channel 5, magazeti na hata mapaparazi wa magazeti ili mashemeji, wajomba na wake ama waume zao wawaone wakikenua mijino yao wakati wameshikana mikono na wakubwa wa hospitali wanaopokea misaada kwa niaba ya wagonjwa.
Kama hakuna vyombo vya habari, basi anaahirisha msaada wake hadi ifanyike kazi ya ziada kuwapata mapaparazi hao.
Hali hii ni hivyo hivyo kwa wale wanaotoa misaada kwa watoto yatima, wasiojiweza kutokana na umri na binadamu wenzetu wengine ambao wanaonekana kuwa na upungufu katika maumbile yao.
Kila mmoja anaweza kutoa michango kwa moyo wa dhati bila kujali kutangazwa ama kujulikana na watu wa namna hii ndiyo, huenda kwa kiasi kikubwa, wakaiona pepo inayoelezwa kwenye vitabu vitakatibu.
Leo waweza kuwa wewe, mtoto wako, mke, baba, mama na jamaa katika familia yako akakumbwa na tatizo la afya na kukuta akilala kitanda cha hospitali bila kutarajia. Nani anapenda kuona mwili wake ukisumbuliwa kwa sindano ama vidonge kila mara. Hakuna.
Uzima wako leo usikufanye kuwa mwendawazimu wa kiburi cha uzima, wakati huyajui ya kesho.
Tukatae kurogwa. Inawezekana. Tuwape pole wagonjwa kwa kuwatembelea hata tukiwa mikono isiyolambwa kwa ‘kuzezema’ mafuta na asali.

Wednesday, March 02, 2005

Yuko wapi mgombea mwenye usafi wa theluji

NAKUMBUKA vyombo vya habari vya Marekani vilivyokuwa vikiwachafua wagombea Urais wa nchi hiyo mwaka jana, 2004.
Kilichokuwa kikiandikwa ama kutangazwa na vyombo hivyo ni kichekesho. Ilikuwa ni kuchafuana tu. Na hakika watu walipenda kusoma uchafu huo kwa kila mmoja kuwa na matakwa yake.
Wengine walitaka kucheka tu. Wengine walitaka kujua maisha ya undani ya wagombea, lakini kubwa lilikuwa kwa wauza magazeti. Wao walitaka kuuza magazeti yao kwa kuandika chochote.
Ingawa ni kweli, kwa kiasi kikubwa kilichokuwa kikiandikwa kilithibitishwa kwa asilimia chache na hata na wagombea wenyewe wakuu, John Kerry wa Democrat na George W. Bush wa Republican. Mgombea binafsi Raph Nader yeye hakuwa na matatizo sana na vyombo hivyo.
Kilichotawala zaidi ni kuandikwa kwa maisha binafsi zaidi kwa maana ya kuchafuliana. Magazeti yalikuwa yakiandika kushindana ni mgombea yupi kati ya Bush na Kerry aliwahi kuua watu wengi wasiokuwa na hatia walipokuwa vitani.
Gazeti moja likiandika Kerry ndiye aliyeua zaidi, gazeti jingine linaibuka kwamba siyo kweli na kutoa takwimu kwamba ni Bush.
Chombo kimoja kikiandika kwamba Bush alikuwa mvuta bhangi kingine kinakanusha kwa kueleza kwamba ni Kerry ndiye alikuwa gwiji wa misokoto mingi kwa siku.
Kali zaidi ikawa ni nani miongoni mwao alikuwa mtu wa watoto; aliyekuwa hodari wa kutembea na vimwana alipokuwa bado na ‘nguvu’ za kuzunguka kutoka nafasi moja hadi nyingine.
Ama hakika ilikuwa ni burudani ya aina yake kusoma magazeti hayo; mchezo ambao haukuyatofautisha magazeti makini wala yale yaliyozoeleka ya udaku. Kilichokuwa kinachimbuliwa ni kile cha miaka mingi ya nyuma.
Huko kulikuwa ni kuchafuliana. Hakuna maana nyingine iliyoweza kuelezwa na yote yaliyokuwa yakiandikwa. Kila chombo kilikuwa kinapigia debe mgombea wake.
Hayo ya Marekani sasa ndiyo yanajitokeza hapa kwetu, ambapo wote wanaoonyesha nia ya kutaka kugombea ama waliojitangaza tayari kupitia Chama Cha Mapinduzi ‘wanashushiwa’ kile kinachoelezwa na vijana wa kisasa kuwa Tsunami; kwa maana ya nyundo ya kuwamaliza.
Wanaofanya hivyo siyo wengine ni vyombo vya habari kwa namna mbili, kwanza kwa kutumiwa na watu wenye nia kwa wagombea ambao wanadhani wana nguvu zaidi, ama kwa magazeti yenyewe kuwapendelea wanaodhani wanafaa kushika nafasi ya urais wa Tanzania.
Pamoja na kwamba hadi sasa bado hatujashuhudia machafu zaidi, lakini kinachoandikwa kinatia kichefuchefu, kwa kuwa habari zenyewe zinakosa kichwa wala miguu, zinaibuka tu- bila kuwa na misingi thabiti ya uandishi wa habari.
Magazeti yanaibuka na habari kwamba Fulani hafai kwa kuwa ni mzee, eti ana mvi nyingi, eti ni kijana- kwamba atavuruga nchi, haaminiki, akiibuka mrefu magazeti yanakuja na habari kwamba ni mrefu sana, hafai atafanya kuwepo kwa marekebisho ya kiti chake katika ndege ya rais, akiwa mfupi magazeti hayo hayo yatakuja na habari kwamba hafai kwa kuwa akikaa kwenye kiti hicho hicho atakuwa akining’iniza miguu. Alimradi hakuna kizuri kwa yeyote.
Ni kwa kugundua au kuona kuwepo kwa hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Benjamin Mkapa amewatahadharisha wote wenye nia ya kugombea nafasi ya Urais kuacha kabisa biashara ya kupakana matope.
Anawataka wote kutumia njia za kuomba ridhaa, kwanza ya wanachama kwa amani na utulivu na kwa njia za kistaarabu badala ya kuanza ‘kuvuana’ nguo mbele ya umma.
Mkapa akatanabaisha kwamba atakayegundulika kufanya kampeni chafu za namna hiyo atakuwa anakosa sifa za kuwa kiongozi bora anayeweza kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wake.
Mbali na Mkapa, CCM ina taratibu zake ilizojiwekea kumpata mgombea wake, ambaye kwa hakika ndiye atakuwa kiongozi wa nchi hii, na sifa hizo zimepitishwa na Chama hicho makini lengo likiwa ni kumpata nahodha atakayeendesha vyema ngalawa ya maendeleo yaliyopo na kuyazidisha.
Taratibu hizo ziko bayana na miongoni mwake ni pamoja na kiongozi anayefaa kuwa mwepesi kujirekebisha. Awe tayari kukosolewa na kukubali kwamba amekosa, hata kama siyo hadharani na kurejea alipojikwaa na kusimama imara huku akitanguliza mguu wake wa kulia ama kushoto kuanza ‘marathoni’ ya kuwakomboa Watanzania na umasikini, magonjwa na ujinga.
Hakuna binadamu awaye yote asiyetenda makosa ama kwa kutambua au kutotambua, ndiyo maana kuna neno kutubu hata katika vitabu vitakatifu.
Watanzania wenzangu hasa mashabiki wa wagombea watarajiwa ama wale waliojitangaza, ni vyema wakaibuka na hoja za maana katika kumuuza mtu wanayemtaka, badala ya kutumia magazeti kuwauzia wananchi ‘uchafu’ wa mmoja na mwingine ambao hautusaidii katika mustakabali wa nchi yetu.

Bravo RPC Mssika

KWA muda wa miaka miwili, safu hii iliyokuwa ikitoka katika gazeti dada la hili, Mzalendo linalochapishwa kila Jumapili ilisimama kutokana na sababu zilizoshindwa kuzuilika.
Sasa safu imerudi na itakuwa ikichapishwa kila Alhamisi. Ni matumaini yangu kwamba wapenzi wa safu hii watafurahi kuisoma na kuendelea kupata mtazamo mpya katika masuala mbalimbali, hasa yanayogusa moja kwa moja maisha ya Watanzania.
Ni matumaini yangu kuwa wapenzi na mashabiki wa zamani na wapya wa safu hii wataendelea kuniunga mkono na kunitia moyo. Kama ilivyokuwa awali, mashabiki wako huru kutoa mawazo yao kwa maana ya kupongeza, kushauri na hata kujadili kwa hoja zenye kujenga, lengo likiwa ni kuboresha.
Safu hii haitasita kusifu, kukemea, kushauri na hata kuonya kama ilivyokuwa ikifanya na hiyo ndiyo nafasi yake katika kuijenga jamii yetu ambayo inapambana kuondokana umasikini wa mali na hata fikra.
Katika ufufuo wa safu hii leo, nazungumzia suala zima la usalama wa raia na mali zao katika mkoa wa Shinyanga. Nakumbuka vyema kwamba mkoa huo wenye wakazi wengi wa kabila la Wasukuma haukuwa na amani kwa maana kwamba wezi, majambazi na hata majangili walikuwa wengi. Maisha ya raia yakawa ya wasiwasi iwe mchana kweupe ama usiku wa giza nene.
Mbali na watu hao wabaya, wauaji nao hawakuwa haba, walikuwa wakiua, kama mvua kinamama wazee kwa tuhuma za uchawi. Ama hakika ajuza hawakuona raha ya kuendelea kuishi. Muda wote roho zao zilikuwa juu juu wakitegemea kutokea kwa wakata mapanga.
Wafanyabiashara nao hawakuwa na raha hata kidogo. Muda wote walikuwa na wasiwasi wa kuvamiwa na kuporwa mali na fedha zao na wakati mwingine hata roho zao huku wanafamilia wao wakifanyiwa vitendo vya kinyama ikiwemo kubakwa.
Ni kutokana na hali hiyo, idadi kubwa ya wafanyabiashara wenye asili ya Asia waliongeza kasi ya kuhama Shinyanga na kwenda maeneo mengine ambako wana hakika ya kufanya shughuli zao bila woga mkubwa.
Wauzaji wa madini ya dhahabu na almasi, yaliyojaa katika ardhi ya mkoa huo, hawakuwa na raha na kazi zao; kisa kuvamiwa na manyang’au na maharamia wenye uchu wa kutajirika haraka.
Ama hakika, habari za wafanyabiashara kuuawa, ajuza kukatwa mapanga na hujuma zingine za aina hiyo zilikuwa zimezoeleka masikioni mwa wananchi wa huko na hata maeneo mengine ambako taarifa hizo zilifika.
Hata wageni nao wakaanza kuogopa kutembelea maeneo mengi ya mkoa huo wakiwa na vijisenti vyao. Maharamia hayana dini, hata kama waliokuwa wamebeba vijisenti vichache kupelekea wazazi wao wakawa wagumu kwenda kwao.
Kwa ujumla, hali ya usalama katika mkoa wa Shinyanga, hasa mjini, wilaya ya Kahama na maeneo mengine ilikuwa mbaya mno. Hali ilikuwa inatisha.
Hata hivyo, baada ya hali hiyo kuwasumbua wakazi wa mkoa huo kwa muda mrefu, hatimaye nuru ya amani na usalama ilichomoza baada ya Afande Abdallah Mssika kuhamishiwa katika mkoa huo akiwa Mkuu wa Polisi wa Mkoa mwaka 2003.
Kuwasili kwa Afande Mssika, awali hakukuonyesha tofauti kubwa ya kuwepo kwake na wale waliomtangulia, kwani matukio ya kutisha yaliendelea kutokea.
Medani za kijsehi suala la Mssika kuonekana hana tofauti na waliomtangulia linaeleweka vyema kwani ndiyo kwanza alikuwa akisoma mazingira mazima ya kuwepo kwa matukio hayo.
Hatimaye baada ya kukamilisha uchambuzi na upembuzi wake, Afande Mssika, mwenyewe kwa kushikiana na vijana wake wa kazi, aliingia ‘msituni’ na kuanza mashambulizi mazito.
Inaelezwa kwamba alichofanya Afande Mssika ni kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wote wakubwa waliokuwa wakitajwatajwa kushirikiana na majambazi na maharamia wanahojiwa na yeye mwenyewe.
Mbali na hao, aliwahoji watu wote vijijini waliokuwa wakitajwa kuhusika katika masuala ya kuwaua bibi wenye macho mekundu kwa tuhuma za uchawi.
Mbinu hiyo aliyotumia Mssika pamoja na zingine, baada ya muda mfupi ilizaa matunda kwani wizi wa kutumia silaha, uharamia na hata mauaji ya bibi wenye macho mekundu ulipungau kwa kiasi kikubwa.
Mbali na juhudi hizo za jeshi la polisi, pia kupungua kwa kiasi kikubwa kwa uharamia kulitokana na wananchi, raia wema kuwa na imani na jeshi la polisi kwa maana kwamba walianza kutoa taarifa sahihi kwa jeshi hilo. Hawakuwa tena na wasiwasi kwamba siri wanazotoa kwa jeshi zitavuja na kuwafikia wahusika wanaotajwa na kuwa mwisho wa watoa siri.
Inaonyesha kwamba raia wema walipoteza imani na jeshi hilo mkoani humo kwa kuwa waliokuwa wakipewa siri walikuwa wakizivujisha kwa wezi, majambazi na wauaji na wao maisha yao kuwa hatarini. Nani anakubali kufa kwa kutoa taarifa ambazo baadaye zinavuja ? Hayupo.
Taarifa zinaonyesha kwamba hadi kufikia mwaka 2003, mkoa wa Shinyanga ulikuwa miongoni mwa mikoa iliyokuwa ikiongoza nchini kwa kuwa na matukio ya kinyama dhidi ya binadamu yanayofanywa na binadamu wenzao wenye roho za paka.
Kazi ya polisi ni kulinda raia pamoja na mali zao, lakini wananchi wanaolindwa wanapokosa uaminifu kwa jeshi lao wenyewe, kazi ya walinzi hao inakuwa haina maana na kuwepo kwao kunatia shaka.
Hata hivyo, wanapopatikana viongozi wenye mtazamo wa dhati wa kutenda kazi zao ipasavyo, wananchi wanaishi maisha ya raha na kuondokana na wasiwasi ambao hauwatofautishi na wakimbizi katika nchi yao.
Kazi anayoendelea kuifanya Afande Mssika inapaswa kupongezwa na kuigwa na askari wote. Na ieleweke kwamba utendaji unaoonekana kutukuka wa Mssika haukuanzia Shinyanga, ngazi zote alizopita askari huyo mkakamavu zinadhihirisha anavyoweza kujituma kuitumikia nchi na watu wake.
Bravo Afande Abdallah Mssika.

Monday, February 21, 2005

KONA HIIIIIYOOOOO IMERUDI

Jamani huwezi kuaminiu, baada ya kuwa imekwama kwenye kompyuta zetu na kwenye ubongo wangu bila kuwafikia wasomaji wangu, hatimaye safu yangu iliyokuwa ikitoka kwenye gazeti la Mzalendo, sasa imeruhusiwa kuanza kutoka tena.
Ingawa sasa inatoka kwenye gazeti la kila siku la Uhuru kila Alhamisi
Ni mapinduzi makubwa, wasomaji watarajie mtazamo mpya wa fikra mpya.
Tuwe pamoja.

Sunday, January 30, 2005

Sumaye atangaza kuwania Urais

Mtendaji Mkuu na msimamizi kiongozi wa shughuli za serikali, Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Frederick Tluway Sumaye amevunja kimya na sasa anawania nafasi ya juu kabisa ya uongozi; Urais.
Anasema kwamba ameamua kuingia katika knyang'anyiro hicho kwa kuwa ana uwezo wa kuongoza nchi. Pia anaeleza kwamba anahitaji kuendeleza mazuri yote ya Mkapa na kuyaboresha yale ambayo yalionekana kusuasua.
Pamoja na hivyo, amesema kwamba anataka kuwaonyesha wapinzani wake, hasa magazeti yaliyokuwa yakimsakama kwa kutumiwa na maadui zake, kwamba yote mabaya yanayosemwa juu yake niuzushi, hayana maana.
Mie, kama walivyo Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao, namtakia kila jema katika safari yake.
Naomba na wengine wenye kudhani kwamba wanaweza kuwakwamua Watanzania wachukue fomu za kugombea Urais.
Natamani nami niwe mmoja wao, lakini hiyo milioni moja ntaipata wapi jamani.
Naombeni michango, nikishinda narudidha fedha zenu na faida ya asilimia 10000.
Nisaidieni jamani

Bado Shinyanga

Jamani bado niko Shinyanga kwa Wasukuma. Hawa jamaa bwana ni wakarimu kweli, kila ninapoingia nyumba moja, nakula, nyumba nyngine napewa chakula, nikikosa sana nakunywa maji ama soda. Ukikataa wanadai kwamba unaringa kwa kuwa unakaa Dar. Basi ni kua tuuuu, lakini lazima uwe makini,ukizidisha sana unaongezeka kilo bila mpango na kukaribisha magonjwa.
Narejea Dar wiki ijayo kupitia njia ya kati kwa barabara ambayo mheshimiwa Magufuli Pombe anadai kwaba baadaye mwaka kesho itakuwa ikipitika hata kwa taxi kutoka Dar hadi Mwanza. Tusubiri. Maana barabara hiyo niivyoiona wakati nikia huku ni balaa tupu, mahandaki ibao na huo ni wakati ambapo mvua zilikuwa zimekoma kwa muda, sasa sielewi mvua itakapoongeeka inakuwa namna gani.
Mashabiki wangu wananiuliza kwanini nimekuwa kimywa, nawaambia kwamba jamani huku kugusa tu mtandao, alfu inakutoka, sasa muda huo huo nitume habari kwa wakubwa wangu na kusalmia jamaa na halafu kublog.
Vuteni subra nikirejea Dar kazi ni kama kawaida.
Tukijaaliwa.


Friday, January 21, 2005

Shinyanga kwa baiskeli..hawajambo

Najua wengi mtakuwa mkiulizana vipi huyu mzee wa Kona Yangu amefia wapi?
Hapana sijafa bado...ni masuala ya kazi tu za milipuko.
Unaambia hivi sasa niko Shinyanga, mji wenye utajiri kibao mpaka baiskeli.
Nina siku ya sita sasa na nimekuwa huko vijijini ambako mtanda kwao ni sumu.
Haya nawahi msafara wa kiongozi mkuu, ukikuacha kazi huna na watoto wanakufa njaa.
Tuko pamoja katika ujenzi wa Tanzania mpya.

Saturday, January 08, 2005

Hawa viongozi watabadilika lini?

Naombeni ruhusa yenu kwanza niwatakie heri ya mwaka mpya nami pia mnitakie heri hiyo hiyo.
Mama Nchimbi ameandika akiwataka viongozi wa Tanzania kutoa heri ya mwaka mpya kwa Watanzania wote ili waweze kuishi kwa amani, kupata maendeleo makubwa na hata kuwa na uchaguzi wa heri.
Nami natumia nafasi hii kuwapa Wana-Blog wote heri ya mwaka mpya ambao uwe na heri kwa ukamilifu wake na pia waweze kutimiza malengo yao ambayo hayakutimizwa mwaka uliopita.
Nimepata wazo jipya mwaka huu ukiwa bado mapema; nimekuwa nikijiuliza kwanini viongozi wetu hawataki kuleta maendeleo ya haraka na ya uwazi mkubwa ambapo kila mmoja wetu atafaidi matunda ya uhuru?
Jibu lake nimelipata kwamba kumbe hao viongozi wetu hawana muda kabisa jamani wa kufulia mambo ya maendeleo ya wananchi.
Kinachofanyika ni wao kuwa bize mno na kutafuta wapi teni pansenti inatoka, wapi watakwenda kuomba, hasa kwa wafanyabiashara wa Kiasia ili waweze kuwasomesha watoto wao Ulaya na wengine wanakwenda mbali kidogo, eti wako bize wakipanga mikakati ya kuiba kura.Ajabu kweli.
Kumbe jamani hawana muda wa kutuhudumia sisi.
Wao kumbe nao ni sawa tu na waandishi wetu kwamba wao wako bize na kutafuta mishiko hawataki kusoma ili waandike waelimishe, waonye na hata kupongeza. Kazi kubwa ni kujua mishiko iko wapi.
Jamani tutafika kweli!

Wednesday, December 29, 2004

Watanzania kwa kuwekeana kauzibe hawajambo!

KILA siku zinapigwa kelele na serikali kwamba hivi sasa kuna kila juhudi za kuwawezesha wananchi kumiliki asali na maziwa ya nchi. Kelele hizo zinalengo la kuonyesha kwamba serikali inafanya kila linalowezekana ili wananchi, bila kujali hali yake ya kiuchumi wafaidi matunda ya uhuru yaliyopatikana mwaka 1961.
Ndiyo ni uhuru wa mwaka 1961, lakini sasa yaonekana kabisa uhuru huo umebaki kuwa historia na kusherehekewa kila mwaka inapofika Desemba 9.
Lakini, nina wasiwasi ikiwa sasa kila mazingira na kila hewa (kwa maana ya uchumi na sekta zote za kustawisha jamii) inaonekana hapa zinamilikiwa na watu ambao hata historia yetu hawaijui; hivi hapa bado tuna uhuru kweli au tunao wa bendera na historia tu.
Ni hao sasa kwa kuwa tu wanamiliki ardhi wakajenga viwanda, wakachimba wanavyotaka kila kitu, na kutojali madhara watakayoacha baada ya miaka yao 33 au 66 kwisha ndi wanaofaidi mno.
Hapa naomba mnielewe vyema, kwamba nazungumzia uhuru na siko nje ya topiki hiyo ambayo ni pana mno (nitaitafutia muda wake maalum).
Mipango na kile kinachoitwa mikakati ya kuondoa umasikini inapendeza kweli inavyosomeka kwenye karatasi, lakini sasa utekelezaji wake naona ni zero kabisa.
Nasema utekelezaji wake ni sifuri kwa kuwa tumekuwa na mipango kibao ya 'kugawana' umasikini, lakini wanaoonekana kupunjwa zaidi ni hao wake wa wakubwa, sisi tunagawiwa sehemu kubwa mno ya umasikini huo, na wao wakipata kiduuchu.
Hiyo ushahidi upo, mbona pesa nyingi za mikopo zimekuwa zikitolewa mijini kwa mashangazi, wajukuu, mashemeji wa hao wakubwa wanaozigawa. Watazame nyuso zao, hawana hata mshipa wa aibu, hawajali kwamba pesa hizo zinatakiwa kupelekwa vijijini, wao wanazigandisha hapa mjini, hasa Dar...wanaziiiiila mpaka basi.
Mtindo huu ndio unaonipa wasiwasi wa kufanikiwa kwa mipango mingine kibao mizuri ya kuondoa umasikini.
Sasa nije kwenye topiki yenyewe, kumetokea ugomvi hapa wa ajabu kweli, Ipo kampuni moja ya Wazawa-sema wenyeji-ukipenda (ingawa uzawa ndilo lenyewe, hili kwa watu wenye ukweli halikwepeki, isipokuwa kwa wanafiki linaonekana mwiba mkali), kampuni yenyewe inaitwa NICO, kwa kweli watu wenye uwezo wao wamejikusanya na kuwekeza fedha zao huko kwa mamilioni.
Lengo kubwa la NICO likiwa ni kununua hisa katika kampuni na mashirika makubwa ya serikali ambayo bado hayajauzwa kwa weupe na hata weusi wenye ngozi ya ukaburu uwe wa kusini ama mashariki.
Sasa bwana hao jamaa wanaendelea na kampeni zao za kuwashawishi wananchi wengine wote kununua hisa kwa sh. 250 kila moja. NICO wanataka kwamba wananchi wengi zaidi wamiliki uchumi kwa kujikusanya kwa maana ya kujenga mtaji mkubwa.
Ghafla bin vuuu, hao jamaa wakiwa wanapata mafanikio, likaibuka dudu fulani linaitwa PSRC, naliita dudu kwa kuwa lina miparaganyiko kibao, wananchi wengi wanalilalamikia dudu hilo.
Ni kweli PSRC imeundwa na Rais, ikiwa ni asasi ya kusimamia urekebishaji na uuzaji wa mali zilizokuwa za serikali (usiseme umma maana waliozifaidi walikuwa ni wale wakubwa waliopewa dhamana ya kuziongoza).
Lakini, nimeshangaa kweli, kama ambavyo wengi wana wa nchi walivyoshangaa kwamba akaibuka kiongozi wa hiyo PSRC akidai kuwa wananchi wawe macho na ununuzi wa hisa, akimaanisha za NICO (hawezi kukwepa hilo, alikuwa wapi kusema zamani?).
Huyo kiongozi anawakanya wananchi wasiendelee kununua hisa...ili mali zote zitakazouzwa ziwe za hao wanaowaona wao ndiyo wanaofaa kununua mali zetu zilizokuwa zao wakubwa (nasema hivyo kwa kuwa wakubwa waliomaliza mali za umma ndio hao hao leo wanaendelea na dhamana katika ngazi kubwa za serikali, tasisi na ofisi zinazoitwa nyeti...tunawajua hata wakiwa katika kutoa maamuzi ya kuuza ama kutouzwa kwa shirika).

PSRC linamalalamiko kiboa kutoka kwa wenye akili, yaani wananchi wa nchi hii. Wanajua kwamba dudu hilo limeuza mali kibao kwa bei ya cheeee, na wengine wakiuziwa mashirika mengine hata kabla hawjamaliza madeni ya mashirika ya awali waliyonunua na pia hata waliotelekeza baada ya kununua wanapewa kipaumbele...haya
Kumbe bwana wapo wenye akili zao, hawajali hao jamaa wa dudu hilo...PSRC wanasema nini. Bwana mmoja juzi akajitokeza, anaitwa Dk. Salim Ahmed Salim akanunua hisa za milioni moja sambamba na watu wengine kibao.
Dk. Salim kama walivyo wengine wamegundua siri ya ujanja...hawakubaliani na maneno kwamba huenda NICO imeibuka kuelekea uchaguzi mkuu ikitaka kuwasaidia watu kadhaa kupata urais.

Kinachofanywa na PSRC ni kauzibe tu wananchi wenye mali zao, wao kwa kuwa, (wananifanya niamini) eti wanapokea 10%, basi wanaona heri kuuza tu kwa yeyote hata kama ni muuza dawa za kulevya au jambazi...si analeta hela bwana na cha juu...
Jamani Watanzania kwa kuzibiana...haya bwana...waachieni hao wanaoonekana kuwa wanunuzi zaidi.
Nasema itafika mahali tutajuta...na vijana wetu watahoji mengi na ikiwezekana hata kutuchapa viboko...wakipigania 'maendeleo' yao upya ambayo sisi tuliwaachia maharamia waliokuja kwa kutulambisha asali kumbe inapofika kwenye utumbo mpana inageuka kuwa shubiri ya ajabu.

Tukijaaliwa.

Friday, December 24, 2004

Nsuji go mva gukang'wiwagwa go moto

Wasukuma wana msemo kama unavyosomeka hapo juu ambao maana yake ni kwamba supu ya mbwa hunywewa ikiwa ya moto, ikipoa basi hainyweki maana inakuwa nzito na mbaya.
Maana ya msemo huo ni kwamba ni vyema kuchangamkia kila jambo kungali mapema ikiwa linaonekana linaleta faida.
Sasa nawahimiza Watanzania wenzangu kuwa macho na kujituma zaidi katika shughuli zao. Ikiwa mwaka huu wameshindwa kutimiza malengo yao, basi Inshallah mwaka kesho kila mmoja afanye hima kuanza mapema jitihada zake za kujikwamua na umasikini.
Kila heri katika shughuli za kila mmoja.

Mama yangu...Wameachiwa!

Ni ajabu na kweli...Tanzania juzi ilikumbwa na simanzi baada ya kutapakaa kwa habari kwamba wazungu wawili Waingereza walioua dada yetu wameachiwa huru.
Wameachiwa huru eti kwa mamlaka aliyonayo Mkurugenzi wa Mashitaka, kwamba eti hawana kosa la kuua.
Ninavyoandika hivi sasa vijana hao waliokuwa wametoka Fallujah na kuja kutumbua Dar es Salaam, wamewasili kwao na wanakula kuku kwa mirija wakituona jinsi sisi Watanzania tulivyokuwa wajinga.
'Nini bwana Tanzania- u ken jasti kili endi go, noo bode tachiz uu-, ndivyo wanavyosema sasa wakiwa na wachumba wao. Pumbavu zao.
Yaani jamani wameachiwa kabisa, tena katika kesi ya mauaji...najua kwamba Wamatumbi wenzetu wakiua hata kama kwa kusingiziwa hawawezi kuachiwa kwa muda mfupi namna hiyo, tena kesi ikiwa bado inasikilizwa katika mahakama ndogo kabla hata ya kusomea mashitaka katika mahakama kuu yenye dhamana kwa kesi za mauaji.
Hao Wazungu hawajakaa hata mwezi mmoja ndani, ambako nako walikuwa wakila kuku kama kawaida, wameondoka lakini nasema damu ya binadamu itawafiuata huko waliko.
Waone ngozi zao...wamezoea kuua...wamewaua Wairak na hawajachoka, sasa wanakuja kuua watu wetu...washenzi wakubwa.
Jamani nyie mnaokaa huku Ulaya mkiwaona naomba muwafikishie salamu zangu kwamba nawatukana sana Watanzania wengi wanawaona kama mashetani wasiokuwa na mikia. Waangalie kwanza pua zao.
Magazeti mengine nayo bwana hayana utaifa, eti yakaandika aliyeuawa ni changudua, kuonyesha kwamba siyo binadamu kamili kama walivyo waandishi ama wahariri wa gazeti hilo, nao siwaogopi nawaambia wakafie mbali kama waliona wazungu hao wauaji ni wa maana sana kuliko Mtanzania mwenzetu.
Napata mawazo kwamba Tony Blair aliyeidhinisha Wairak kuuawa kama kuku alizoza na vingozi wetu na wakakubaliana suala hilo liishe kinyemela. Hata afadhali kidogo kwa kuwa vingnevyo tungesikia tu hao jamaa wametoroshwa na wako kwao siku nyiingi...njia hii naona waliistukia
Kweli nimeamini umasikini kweli mzigo, yaani mtu kwa kuwa tu anaweza kusaidia kukupa mkate, basi anakuwa na sauti hata ya kutoa roho za watoto wako. Makubwa. Mungu atunusuru na haya maswaibu.
Hivi kweli angekuwa Mtanzania huko Uingereza amehusishwa na mauaji, wangemwachia washenzi wale. Nasema wasingethubutu kufanya hivyo kwa kuwa wanaamini kuwa damu yao ni nzito kuliko maji kama ambavyo maji yetu yalivyo mepesi kuliko damu.
Kuwatukana binadamu ni dhambi lakini Mungu atanisamehe kwa hili.


Thursday, December 23, 2004

Barua ya Rais Ben (Eksiklusivu)

Shikamoo Rais Ben,
Nimelazimika kukuandikia barua hii, kwanza kwa kukupa pole na kazi. Pia kukutakia sikukuu njema ya Krismas pamoja na Mwaka Mpya (Inshallah) tukifika.
Pamoja na salamu hizo, napenda kukueleza kuwa nimeamua kutumia njia hii ya kuwasiliana na wewe kwa kuwa njia zingine zote ni ngumu mno kukuona. Sana sana kama ingekuwa inaweekana kuongea na wewe kwenye luninga ningefanya hivyo, lakini haiwezekani.
Vinginevyo ningeandika barua, lakini nayo na uhakika na ushahidi wa kutosha kwamba lazima ingefunguliwa na watu wengine kabla ya kukufikia mikononi mwaka na pengine huenda wasikufikishie kabisa.Tunajuana bwana Watanzania.
Nimeamua kuchagua njia hii ya Blog kwa kuwa ni salama, haraka na ya uhakika zaidi. Inawezekana kabisa ikasomwa na watu wengine, lakini hilo siyo tatizo kubwa maadam utaipata.
Ninachoeleza katika waraka huu ni kwamba nina kila sababu ya kukupa 'five' baada ya kuwa umeibuka na kutambua sasa umefika wakati wako wa kuwasimamia zaidi masikini kwa lengo lile lile ambalo mara zote umekuwa ukilipigania la kuondoa umasikini.
Sasa, pamoja na kwamba umechelewa mno kuibuka na hoja hiyo, najua imepokelewa kwa mikono miwili na kwam moyo mkunjufu na kila mmoja.
Ni hivi majuzi tu umeeleza kuwa mkakati wa wanyonge kumiliki rasilimali (MKURABATI) unaanza kazi na utahakikisha kwamba kabla ya kuondoka madarakani, mwishoni mwa mwaka kesho, umasikini wa wananchi utakuwa umepunguzwa kwa kiasi kikubwa.
Najua na nina uhakika kwamba wewe ni mtu wa kutimiza ahadi zake na ndiyo maana nimeona nitoe pongezi kungali mapema kweupeee.
Njia mojawapo ya kutimiza hili, kwa mujibu wa mkakati huo ni kuwapa uwezo wananchi wa kukopa kwa kutumia rasilimali walizo nazo na siyo lazima ziwe zimethamanishwa na wakadiriaji, ama idara zingine ambazo zina urasimu wa kutisha.
Katika hilo, mtu anaweza tu kuweka ardhi yake ama nyumba yake kama dhamana hata kama hazina hati ambazo kupatikana kwake katika mazingira ya sasa zinaweza kugharimu thamani ya nyumba yenyewe ama kiwanja kwa vile wahusika na huduma hiyo ni walaji kweli wa rushwa. Hili nadhani unalijua kama ambavyo hata Jaji Warioba aanavyoeleza katika ripoti ya tume yake ya kuainisha mianya ya rushwa.
Hapa kinachotakiwa ni serikali za vijiji tu kuthibitisha kwamba fulani ana miliki kitu fulani na benki au taasisi zingine zinakuja na kuangalia thamani yake ikilinganishwa na mkopo unaoombwa.
Hili kimtazamo litawanufaisha hata wananchi wetu wa vijijini ambao wana ardhi kubwa, lakini wanashindwa kuilima kutokana na kukosa mitaji na watoto wao wengi kukimbilia mijini ambako kuna kila kitu kuanzia mwanga muda woite, huduma bora za afya na jamii.
Kitu kingine ni kwamba hizo fedha za mikopo basi kweli ziwafikie wahusika na zisikomee mijini tu ambako wake na mashangazi na wajomba wa wahusika ndio huzifaidi kama ambavyo tumeshuhudia katika mikakati mingine ya kuondoa umasikini inayoendelea.
Ben..huu unachokifanya ni kizuri na tunaomba uendelee hivyo katika kipindi chako kifupi kilichobaki na historia itakukumbuka na kukukumbatia kwa mbawa zake.
Nakutakia afya njema hadi tutakapoonana tena.

Simon Martha Mkina
Uhuru na Mzalendo,
Barabara ya Lumumba,
S.L.P. 9221,
DAR ES SALAAM.
Tel (Mob): 0744 020880

Tuesday, December 21, 2004

Ona mshikano huu baada ya mwenzao kuchinjwa

NIMESIKITISHWA sana na habari ya kuchinjwa, maana ya kutolewa uhai na risasi tatu alizopigwa mwandishi huyo wa habari wa Gambia, Deida Hydara.
Hydara nimewahi kuwa naye Afrika Kusini mwaka jana, nakiri kwamba alikuwa mtu mchangamfu, mwenye haiba, mwenye busara lakini asiyeogopa kueleza ukweli.
Sasa kalamu yake na sauti yake ya upole wala sura yake akiwa hai haitaonekana tena kwani maharamia yametumia mikono yenye dhambi kumuua.
Pamoja na kuwa na masikitiko makubwa ya kifo hicho, nimefarijika kwa mshikamano ambao waandishi wa Gambia wameuonyesha ikiwa ni njia ya kulaani mauaji hayo ya kinyama.
Vyombo karibu vyote vya habari jana havikutangaza wala kuchapisha habari.
Magazeti hayakutoa habari, redio nazo zikasimamisha matangazo yao, kwa maelezo kwamba zinaalaani kuuawa kwa Hydara na kushutumu wanasiasa ambao huenda wanahusika na kifo hicho kwa kuwa mhariri huyo wa The Pointi hakuwa na hiana, alisema pailipokuwa panastahili na alisifu panapostahili.
Je haya yanawezekana katika nchi yetu? Sijui, maana naanza kuona kuna mgawanyiko mkubwa katika sekta ya habari na waandishi wenyewe. Hawapendani na kila mara ni kukandiana, wapo wanaojiona wamesoma sana, wengine wakijiona kuwa nii wazoefu na pia wengine kujiona kwamba wanajulikana mno kwa kuwa tu Rais anawajua kwa majina.
Mungu ampe mapumziko ya heri Hydara.

Mrembo Mtanzania aanzisha gazeti Marekani

NAKUBALIANA kabisa na busara za Mwalimu Julius Nyerere ambaye wakati wa uhai wake aliwahi kueleza kwamba Watanzania tumechelewa kwa kiasi kikubwa katika kuyafikia maendeleo.
Mwalimu kutokana na hilo alituasa kuanza jitihada zetu kuyafikia maendeleo kwa kukimbia na siyo kutembea kana kwamba tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Nina hakika msukumo huo ndio unaotuongoza sasa katika sekta nyingi nchini na hata kwa Watanzania wanaoishi nje ama wakisoma, wakitafuta maisha na wengine wakitafuta watoto wao watakao wawe machotara wa Kizungu (unajua kila mmoja anakuwa na ndoto zake anapokwenda Ulaya na Marikani).
Habari kwamba Binti mmoja Mtanzania ameanzisha gazeti Marikani zimenitia moyo sana. Ni dhahiri binti huyo anaanza kukimbia kuwafikia wale waliotangulia. Gazeti lake ( Ni jarida hasa) tayari limo ndani ya mtandao wa kisasa wa mawasiliano usiokuwa na mizengwe.
Binti huyo msomi wa chuo kikuu kinachoheshimika cha Harvard cha Marikani ameanzisha gazeti liitwalo MIMI. Kimsingi gazeti hilo linalenga zaidi kuwapa nafasi mabinti na kina mama wa Kiafrika walioko ndani ya Bara au nje ili waweze kufahamiana na kuonyesha jinsi walivyo sawa na kina mama wengine wa nchi tajiri kana kina Oprah, Janet Jackson, Hillary Clinton na wengine.
naomba kauli mbiu ya gazeti hilo iwe; WAO WANAWEZA WANA NINI NA SISI TUNASHINDWA TUNA NINI.
Kitu kikubwa ambacho ninamuomba msichana huyo Mtanzania aitwaye Lola Kingo aangalie uwezekano wa kuwa na gazeti dada la Kiswahili ambalo litaweza pia kueleweka vyema kwa Waafrika zaidi ya milioni 160 wanaozungumza Kiswahili.
Niko tayari kumsaidia kulirekebisha, kwa lugha akama atakuwa ameanza kusahau Kiswahili na pia kulipitia kwa maana ya utaalamu wa uandishi wa habari.
Soma gazeti hilo la Lola kwa kukongoli hapa:http://www.mimimagazine.com
Nina hakika Lola atakubaliana na mimi.
Namtakia kile jema katika safari yake ya kujikomboa

Monday, December 20, 2004

Krismas njema

NAJUA kila mmoja wetu ana imani tofauti na mwingine, huku kila mmoja, kama alivyoandika Ndesanjo macha kwamba, akiamini kwamba dini yake ndo bora na ina Mungu ambaye ni kiboko sana kuwasikiliza na kuwatatulia matatizo wafuasi wake.
Mengi ameyaeleza Macha na sipendi kuyarejea.
Isipokuwa napenda kabisa kwa dhati ya moyo wangu kuwatakia wote wanaosoma makala zangu na wanafamilia wenzagu wa blog, Krismas njema.
Unaweza kuona kama nimechanganyikiwa kutuma mapema namna hii, lakini napenda kukueleza kuwa ninafanya kitendo cha busara mno na hata mie najisifu kuweza kuandika leo salamu hizi kwa wasomaji wangu na wanaBlog kwa ujumla.
Wajua kwanini nafanya hivyo; Jibu ni kwamba hujui.
Lakini mimi najua; nafanya hivi kwa kuogopa mahanatha yanayoweza kutokea hapa kwetu bila taarifa kwa muda mrefu hata kunifanya nishindwe kuwasalimia na kuwatakia heri.
Unajua hapa Bongo umeme unaweza kukatika kwa siku kibao na nikakosa njia ya kuwatakjieni heri. lakini pia mambo ya huku ni ya ajabu mno, naweza kukosa fedha za kwenda kwenye cafe, maana jamii nzima ya kwetu huku haitanielewa iwapo sitafanya lolote eti kuwanunulia nguo ama kuwatoa kwenda kula out. makubwa haya....kuvaa na kula vizuri hadi sikukuu, tena Krismas.
Najua kesho nikiwapa hizo pesa, basi nakaukiwa ile mbaya huku nikianza mihangaiko ya kusaka karo..msichangae hapa Bongo bajeti zipo, lakini hazipangiki zikapangika. Du...Sijui tutafika. Tusubiri!
Jamani nisiseme sana, lakini salamu zangu za kuwatakia heri zimefika.
KILA HERI YA SIKUKUU NA MBARIKIWE NA MUNGU MKUU.

Mwalimu Nchimbi sasa nawe blog

NAWEZA kujidai kwamba nimekuwa nikisoma makala zilizokwenda shule za Mwalimu Rehema Nchimbi hata kabla hazijawafikia Watanzania wenzangu. Hiyo ni kwa sababu nazisoma kwanza na kuzipangia wapi zikae na zitoke na kichwa kipi cha kuvutia wasomaji.
Kwanza nimpongeze mama huyo wa shoka kwa jinsi anavyoipenda nchi yake. Pamoja na kwamba muda wake kwa sasa ni mdogo mno, akiwa anatumia muda wake mwingi katika masomo, bado anaweza kuandika mawili matatu kwa ajili ya hatma murua ya mama Tanzania.
Pamoja na pongezi hizo, napenda kumuhimiza mama Nchimbi kufanya kila linalowezekana kuwa mwanachama wa mawasiliano ya haraka na ya kisasa katika kupashana habari ya BLOG.
Mie nimeona faida zake, nimepata marafiki akina Ory na wengine kibao ambao kila kukicha wananiandikia ama kunipongeza na kunirekebisha pia.
Sasa ikiwa mama Nchimbi atakuwa mwanaBlog, nina uhakika makala zake zinazoelezea msimamo wake usiotetereka, zitasomwa na wengi. Nina uhakika kuwa hivi sasa soko la magazeti katika Tanzania linagombewa mno, huku wasomaji wakiwa ni wale wale ambao kipato chao siyo kikubwa.
Kutokana na sababu hiyo, nakuwa na wasiwasi kwamba huenda wasomaji wa mama Nchimbi wako wachache, hasa ikizingatiwa soko halisi la magazeti ya Uhuru ambalo limekuwa likitafsiriwa vibaya.
Ikiwa mama huyo angeweza kufungua Blog, nina hakika angeweza kabisa kuongeza idadi ya wasomaji wake ambao nina hakika, watakuwa wakizifurahia na kupata elimu ambayo itasaidia mchakato wa kujikwamua kimaendeleo, siyo ya nguo tu na mwili bali pia akili.
Makala zake anazotuma akiwa Afrika Kusini nimezitoa kwenye magazeti yetu ya Uhuru na Mzalendo na zimepata sifa kutoka kwa wasomaji...ambao ni mashabiki wake waliokuwa wakiuliza alikopotelea. Sasa amerejea na mashabiki wake ni hao hao.
Mama Nchimbi ingia sasa kwenye ulimwengu wa Blog. Unakua kwa kasi ya mwanga.

Thursday, December 16, 2004

Waandishi na vitambi vya semina

Inachekesha kweli, eti wananiona kwamba najidai kwa kuwa tu eti ninakataa kupokea shilingi mbili tatu katika semina wanazoalikwa waandishi.
Nakataa kwa sababu zangu, kwanza nikiona ni mazingira ya rushwa ndiyo kabisaaaa, baada ya kazi zangu naondoka hata ikiwa ni kiasi gani cha fedha, lakini sisemi kwamba sichukui kabisa...ninapoona ni mshiriki halali kabisa kwa barua na ninatakiwa kushiriki kwa siku kadhaa, basi nakubali ikiwa ninapokea kiasi sawa na washiriki wengine.
Kwanini nijidhalilishe bwana, eti kwa kuwa mie mwandishi...basi napewa kiduuchuuu...huku washiriki wengine walioalikwa kama mimi wanapewa fedha lukuki...sina fedha nyingi lakini nmathamini utu na heshima yangu na taaluma.
Pamoja na kwamba nakabiliwa na hali ngumu ya fedha, lakini sichukui 'udhalilishaji' na ninapofanya hivyo, bila kuwalazimisha wengine, wananiona kuwa eti naringa kwa kuwa ninazo...jamani sina kitu ndo maana niwaeleza kwamba kila siku mnipe ushauri wenu kama nianze kuimba, ama kukata viuno jukwaani ili kuongeza kipato, kwani bosi wangu hataki kuongeza senti kwenye kijimshahara changu.
Hata hivyo, huwa napata moyo sana napoungwa mkono na baadhi ya waandishi wenzangu kutoka magazeti na vyombo makini. Nao hugoma bila kushurutishwa na huondoka na mimi ama hubaki, lakini wakidai kupewa haki sawa na siyo kubaguliwa.
Hainiumi sana kwa kuwa ninapogoma na kupigiwa kelele na makanjanja, kwa maana ya waandishi wasiokuwa na vyombo na ambao wanajipachika taaluma, basi moyo wangu huwa na furaha kubwa.
Hao wanaolalamika nimegundua ni wale ambao hata kama kuna bia, wataamua kukaa hadi mwisho wa shughuli wakisubiri kimiminika hicho cha rangi ya kahawia. hawajali kama wanachelewesha habari walizotumwa.
Matokeo yake, kunapotokea semina, warsha, makongamano na hata matamasha, mara kwa mara, basi wao, kwa kuwa wanafakamia mibia, minyama ya kuku, ming'ombe na masambusa, basi wanaota vitambi tu wakifurahia matumbo yao kuongezeka.
Wanapata faraja sana hawa wanapoelezwa kuwa;;;fulani, du umenenepa! Na wanakuwa na kichwa ngumu wakiapa kuzamia kila semina hata bila kualikwa almuradi wasipoteza ukubwa wa matumbo yao.
Heeee...kumbe uandishi wa kisasa ni kuwa na mavitambi yasiyokuwa na mpango ya semina na warsha za kuwavunga wananchi....eti semina za ukimwi zinafanywa kwa waandishi tu....na wanaoguswa (pamoja na kwamba waandishi wamo) wanasahaulika.
Wakichukia heri, wasipochukia...Alhamdulilah


Wednesday, December 15, 2004

Polisi wetu wanachekesha kweli!

JUZI walikanusha kwamba mtoto, mwanafunzi wa shule aliyeuawa wakati wa harakati za kupiga kura uchaguzi wa chini katika ngazi za serikali huko Mbagala, alikufa kutokana na kuchomwa kwa bisibisi.
Baada ya wananchi kung'ang'ania na kuja juu wakipinga kauli hiyo ya polisi na kusindikizwa na nguvu ya vyama vya siasa, hasa CUF- polisi waliuteka mwili wa mtoto huyo na kwenda nao...baadaye wakaupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi na ndipo walipokiri kuwa mtoto huyo mwanafunzi alipigwa risasi...kama ambavyo ndugu na wananchi walivyokuwa wakiamini na wengine kuona kwa macho yao.
Hata hivyo, polisi wakadai kuwa risasi aliyopigwa mtoto yule haikuw ayao, bali ya watu wengine ambao walihojiwa na mmoja wao kuonekana kwamba anamiliki aina ya silaha yenye kutumia risasi zilizotoa uhai wa mtoto yule.
Hili likapita na mtoto mwanafunzi akazikwa...huku polisi wetu wakitoa ubani wa sh. 50,000.Hongera polisi wetuuuuuuuu kwa upole huo na kuthamini wengineeeeeee!
Mapema wiki hii nikashangaa tena kuona polisi wetu wakiwakokota watu 17 kutoka bandarini Dar waliokuwa wakijiandaa kupanda boti kuelekea Pemba.
Walikamatwa eti walikuwa wakihisiwa kwamba walikuwa na nia ya kwenda kujiandikisha katika zoezi linaloendelea upande ule la kuandikisha wakazi wa kudumu ili iwe rahisi kupiga kura mwakani na miaka ijayo.
Najiuliza? Hivi hawa polisi wameingiwa na mdudu gani? Mbona wanafanya mambo tu ya ajabu ajabu!
Hivi jamani kweli unamthibitisha vipi mtu anayesafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwamba anakwenda kujiandikisha?
Au wanataka kunieleza kwamba kila wakati wa uchaguzi ama kujiandikisha basi wananchi tusisafiri hadi anapopatikana raisi, wabunge ama wawakilishi wapya?
Sijui tutafika wapi na haki za msingi za wananchi ni zipi?


Kuuza akili Tanzania kazi ngumu

Jamani hebu naomba mnisaidie, siyo utani...yaani nimefikwa na maji shingoni na sasa sina jinsi kabisa ya kujinusuru na umasikini unaonikabili.
Nashangaa mno hata baada ya kujituma usiku kucha, bado mambo ni mabaya mno na yanazidi kuwa mabaya kiasi cha kukatisha tamaa, ingawa bado sijakata hiyo tamaa.
Kila asubuhi naombwa nauli na watoto, nauli yangu na kodi ya nyumba...basi kila kitu ni kazi na pesa zenyewe hazitoshi kabisa.
Nimeongea na mkuu wangu wa kazi kuongeza kijimshahara anakataa akidai kuwa biashara na mtiririrko wa fedha hauruhusu kwa sasa kufanya hivyo.
Bosi wangu anaeleza eti nichukue mkopo...mwaka jana nilichukua nikidhani unasaidia, nilichukua wa benki, lakini wapi hausaidii, isipokuwa ndo nikaona mambo magumu kishenzi.
Riba ni kubwa mno na wanatoa muda mfupi wa kulipa madeni ya ambayo unakatwa kila mwezi kutoka kwenye mshahara wangu.
Nimekuwa nikiuza akili, kwa maana ya kuandia kuwaelimisha watu wetu, kuwapa changamoto ya maisha, kuwapa mwongozo wa kujiondoa na umasikini na hata wakati mwingine kuwaburudisha kupitia vyombo vyetu vya habari.
Kazi ninayoifanya hapo ni kuuza akili...nimeuza...nimeuza na nikauza...lakini wapi, kila mwaka unaanza na kupita kana kwamba sijafanya lolote.
Du...mambo ni magumu mno na sasa najiona kama kichaa...kumbe siko pekee tuko wengi katika mlolongo wa namna hiyo wa maisha.
Rafiki zangu kadhaa nao nimewasikia wakilalamikia maisha haya...kila mtu anaeleza uzoefu wake...na wachache waliofanikiwa wanatucheka kwamba hatuna akili pamoja na kuuza akili! Ajabu.
Anayesema hatuna akili ni mwenzetu katika uandishi, lakini tunajua siri yake ya mafanikio; Rushwa ambayo mimi siwezi kuifanya kwa kuwa naipiga vita kila kukicha..siipendi na hata wengine wananicheka ninapokwenda kwenye vijisemina na kukataa kusaini sh. 3,000. Nisaini za nini sasa?
Imefika mahali najiuliza iweje sasa ili niweze kuwalea vyema watoto wangu, mke wangu na mama yangu pamoja na wadogo zangu, si unajua tena mambo yetu Waafrika...familia iliyopanuka.
Najiuliza hivi nikacheze muziki wa kukata viuno mbele za watu katika kumbi nyingi za hapa dar, au nijifunze kuimba taarabu ili niende Pemba nikakusanye angalau fedha.
Mambo nayowaza ni mengi na hata natamani nijifunze sasa kuimba Bongo Flava, muziki wa kisasa wa kufoka foka.
Naona vijana wanaofoka foka, hata kama miziki yao haina maana wanatengeneza kweli pesa...kila mmoja akitoa wimbo usiokuwa na maana anapata pesa...anapata mashabiki....anapata magari na anapata nyumba.
Ingawa hayo yanaweza kuwa yamenipita umri, lakini nifanyeje sasa...maana sauti nzuri nimejaaliwa na utunzi wa nyimbo najua.
Hebu wanablog niambieni nifanye nini? Kuiba siwezi...kujikomba kwa watu ili kupewa fedha siwezi...kuwa kuwadi na fitina siwezi...Du!

Tuesday, December 14, 2004

Malaria na vijijini; yote sawa

Nina hakika kwamba wasomaji wa blog na wanafamilia wangu wa utaratibu huu wa mawasiliano wamepigwa na butwaa kutokana na ukimya wangu wa siku kadhaa pasipo kuwasiliana.
Najua maswali yao ni mengi mno na yote yanaweza kuhitimishwa na wasiwasi wa Kiranja wetu katika mawasiliano haya Ndesanjo Macha kwamba huenda nimenyamazishwa na wakubwa ambao, kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakiguswa mara kwa mara na maandishi yangu. Siwagusi kwa ubaya, la hasha! Bali ni katika mchakato mzima wa kurekebishana na kuelekezana lipi lifanyike kwa manufaa ya wananchi.
Kutokuwepo kwangu katika mawasiliano kunatokana na mambo mawili makubwa; kwanza ni safari ya ghafla ya kwenda vijijini Morogoro ambayo ilinikuta, nilielekezwa na mkuu wangu wa kazi kufuatana na kigogo mmoja huko vijijini, eti kukagua uhai na shuhguli za maendeleo. Sijui ni shughuli gani? Labda kilimo cha kizamani cha jembe la mkono na ukosefu wa dawa na uchakavu wa majengo ya shule na zahanati.
Huko vijijini hakuna mawasiliano yoyote, hata yale masimu ya kukoroga- hakuna. Kwanza gari letu lilikuwa likipita kwa shida mno kutokana na ubovu wa barabara.
Kwa kweli nilishindwa kuwasiliana na yeyote hadi siku zangu za kuishi huko kumalizika. Nikiwa huko niliumwa mbu kibao, kuna vyandarua vinavyodaiwa kuwa na dawa ya kuua mbu, lakini havikusaidia kwa kuwa me ninapolala bwana najituma miguu huko na huku, basi kumbe mbu nao wanafaidi vipande vya nyama zangu vinavyogusa chandarua. Kumbe vyandarua hakina dawa wala chochote....basi tu.
Haya baada ya kurejea hapa mjini, Dar es Salaam ndo nikakumbana na bonge la malaria, hadi nikalala nyumbani kwa siku kadhaa na leo ndo nimeingia ofisini na kitu cha kwanza ni kusoma mail zangu na kukutana na familia yangu ya Bloggers.
Nimewamiss sana, sasa msijali, tuko pampja na tuombeane uzima tu.
Tuko pamoja.
Mbarikiwe.

Tuesday, November 30, 2004

Kidogo kidogo.....mwishowe kikubwa!

JUMAPILI Tanzania kulikuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji. Ulifanyika kama ilivyopangwa, lakini ukiwa na dosari kibao.
Dosari kubwa ni vurugu zilizotokea wakati wa upigaji kura, katika jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mikoa ya Mwanza, Morogoro. Mengi ya hovyo na yanayotia kinyaa yalifanyika huku kila chama kikutupia lawama chama kingine kuwa ndiyo chanzo cha vurugu.
Vurugu sizipendi kwa kuwa huonyesha unyani wa binadamu wetu; hakuna ustaarabu kwa watu wazima wanapofikia kuwa wezi wa kura, kisa wakitaka kuingia madarakani kwa nguvu; bila ridhaa ya wananchi. Haya!
Baya zaidi kuliko hata hilo la kupiga kura ni kutumika kwa nguvu za kivita katika kuwamaliza wale walionekana kushabikia vyama vyao. Polisi walitumika kufyatua risasi na hata kujeruhi watu kibao. Magazeti yakaonyesha picha za watu waliopigwa vibaya. Wanalia. Wanavuja damu.
Sasa najiuliza, ikiwa katiia uchaguzi huu wa ngazi ndogo, mwaka kesho kwenye uchaguzi mkubwa wa Rais na wabunge na wawakilishi itakuwa namna gani.
Nani alianzisha vurugu? Mbona haiko wazi! CCM inaeleza kuwa ni wapinzani huku wao wakikitaja chama hicho tawala kuwa ndicho kilichoanzisha vurugu.
Vyombo vya habari navyo vimeonyesha upendeleo mkubwa katika kuandika habari hizo za uchaguzi. Vyombo vya Chama vikaandika wapinzani ndiyo wenye vurugu. Huku baadhi vikikitaja CCM kuwa ndiyo chanzo.
Mwanazuoni mmoja wa Uingereza aliwahi kuelea kwamba katika masuala ya uchaguzi, mara nyingi chama kinachokuwa madarakani ndicho huanza vurugu kwa kuhofia kushindwa kwani hakiko tayari kufanya hivyo kwa hiari.
Uhakika wa maneno yake unaweza kuthibitishwa na matukio ya vurugu kubwa ambayo yamewahi kutokea katika baadhi ya nchi ambako kulifanyika uchaguzi, Macedonia, Ufilipino, Mexico na kwingineko.
Kama hii ni kweli, chonde chonde CCM, jamani hatutaki Tanzania yenye vurugu. Tunataka amani na utulivu uliopo uendelee.
Hii hjatari kweli, Watanzania wamejifunza wapi hizi vurugu, ama wamechoka na nini? Tuelezeni ili tuandike
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Sauti ya umma ni sauti ya Mungu

Kumbe wananchi ndiyo wenye nchi. Siyo Rais, Makamu wake ama Waziri Mkuu.
Wananchi ndiyo waajiri wa wote hao, pamoja na kwamba wanavuta matumbo yao yenye kuonekana yamenona kwa kula na kunywa kwa gharama za hao masikini wanaowaongoza.
Kuongoza kutamu bwana, acha kabisa...nani anataka kutoka akishaingia. Kila anayeingia hataki kutoka na anaringa kwa kuwa analindwa na mitutu ya bunduki, vifaru na makomandoo waliosomea kuua kila anayeonekana kumpinga kiongozi wao, pamoja na ukweli kwamba wao mama, baba na kaka zao ni walalanjaa hao hao.
Jamani mbona keki ya nchi inawanufaisha wachahce, viongozi, wake zao, watoto wao, wajukuu na hata nyumba ndogo zao ambazo hazina idadi.
Nguvu kubwa ya wananchi ni katika maboksi ya kupigia kura, lakini nayo, hayawezi kuleta mabadiliko ikiwa kiongozi ama chama hakitaki.
Lakini kumbe kuna nguvu nyingine; ni nguvu ya umma ambayo siyo virungu wala mikuki ya Wamasai, ni sauti tu ya umoja na mshikamano katika maandamano.
Ukitaka kujua mengi juu ya dhana hii ya sauti ya umma ni sauti ya Mungu soma makala ya Ndesanjo Macha ambaye ameiandika katika gazeti la Mwananchi, Tanzania.
Pia ni imani yangu, kama alivyoahidi kwamba ataiweka kwenye blog, basi ataiweka leo ama kesho: Ungana naye katika ukurasa kwa kukongoli hapa:http://www.jikomboe.blogspot.com
Jenga mazoea ya kusoma ukurasa huo kwa kupata mawazo yake ambayo yanaonekana kujengeka katika misingi ya utaifa na kimapinduzi, lengo likiwa moja tu; kujikomboa katika umasikini wa fikra na hata 'mifukoni'. Niliwahi kusoma mahali kwamba fikra zinapokuwa na afya ya kutosha na mifuko nayo hutuna.

Monday, November 29, 2004

Msome Ory Okolloh hapa

Inawezekana kabisa ikawa mara ya kwanza kusikia ama kukutana na jina la Ory Okolloh.
Lakini, nina hakika kwa Wakenya na watu wengine wenye kupenda kusoma, kwa maana ya kupata taarifa na elimu, hasa wanaotumia njia za kisasa kujielimisha watakuwa wakijua huyo ni nani na anafanya nini.
Kwa faida ya watu ambao hawamjui huyo; Yeye, Ory Okolloh kwanza ni msomi, mwanasheria mahiri mtarajiwa kutoka Kenya ambaye kwa sasa anamalizia masomo yake katika chuo kikuu chenye heshima kubwa duniani cha Havard, kiko Marekani
Akimaliza masomo yake nina hakika atarejea Kenya ama nchi yoyote ya Afrika Mashariki kufanya kazi zake za sheria kwa maana ya kusaidia jamii yetu pana ambayo imegubikwa na 'umbumbumbu' wa sheria, ambazo nyingi ni kandamizi. Yeye ataokoa jahazi.
Mungu amjalie masomo mema na afya njema hadi mwisho wa kazi zake za kushika na kupekua mavitabu kibao.
Kila heri Ory.
Kongoli hapa umsome Ory: http://blogs.law.harvard.edu/ory/

Friday, November 26, 2004

Serikali inaiba mali za Nyerere?

Jana niliahidi kuandika majibu yangu kwa barua pepe ya mbunge ambayo ilikuwa ikinishutumu kwa kuwafuatafuata waheshimikwa hao. Ndiyo ni waheshimiwa kwa kuwa wanaendesha magari ya bei mbaya na kuwa na ofisi zenye viyoyozi, hata wale walio katika maeneo yenye bariidi kali.
Wana-blog nawaomba samahani sana maana ahadi hiyo sitaweza kuitimiza leo. Najua tukoo pamoja, majibu hayo kumbe yanatakiwa niwe nimekula, nmeshiba, tena chakula ambacho ni balanced- mlo kamili ikiwa ni pamoja na katunda kamoja.
Leo nitazungumzia muswada wa serikali wa namna ya kuwaenzi waasisi wa nchi; Mwalimu Nyerere na Abeid Amani Karume. Hawa, bila ubishi ni magwiji wa historia ya Tanzania (ikiwa inajumuisha Tanganyika na Zanzibar).
Muswada huo ambao hatimaye ulifikishwa kwa waheshimiwa katika kikao chao cha 17 hivi karibuni ulikuwa na mambo mengi ambayo, yalialalamikiwa sana na familia ya Mwaliu Nyerere kwa kupitia mwakilishi wao Bungeni, mbunge wa kuteuliwa Rose Nyerere.
Dada huyo, baada ya kuruhusiwa na Spika kutoa maoni yake kuhusu muswada huo, alitahadharisha kabisa awali kwamba anazungumza pale kama mbunge, lakini pia anawasilisha msimamo wa familia ya Mwalimu Nyerere kuhusu muswada huo mzima.
Rose akiwa mwenye uchuungu mkubwa lisema mengi mno, lakini kubwa na lenye kuleta maana zaidi ni madai kwamba serikali, ikiwa muswada huo utakuwa sheria (na lazima uwe, kwa taratibu za wabunge wetu, ni kupita tuuuuu), utaidhulumu familia urithi wa baba yao ambao, kwa kiasi kikubwa ameutafuta akitumia sehemu kubwa ya maisha yake.
Mbunge huyo alisema, anaishangaa serikali kuendelea na muswada huo, ukiwa na vipengele vile vile ambavyo vimekuwa vikipigiwa kelele na familia nzima, ikiongozwa na mjane wa Mwalimu, Mama Maria.
Alisema muswada unataka kila punje ya mali aliyoitengeneza Mwalimu Nyerere iwe sehemu ya makumbusho ya serikali ikiwemo nyumba ambayo wanaishi wana familia kule Butiama, nyumba aliyojenga Mwalimu, achailia mbali ile aliyojengewa na wanajeshi baada ya kustaafu.
Rose anaendelea; "Sisi tunashangaa sana, watu hawa wametukiuka, wao baada ya kukaa na sisi na kukubaliana baadhi ya vipengele kuondolewa, ninashangaa leo bado vipo katika muswada ambao umewasilishwa hapa, ni kitu cha ajabu sana, hatuelewi sasa haya mambo yanakuwa vipi".
Muswada wenyewe, kwa maelezo ya Rose (pamoja na kwamba nimeusoma na kuuelewa, napendsa kutumia msimamo zaidi wa Rose), unaeleza kuwa nyumba, viti, meza, machapisho ambayo ni pamoja na vitabu na habari mbalimbali, nguo na hata viatu, vinatakiwa viwe katika kituo kitakachoanzishwa cha serikali cha kumbukumbu za waasisi wa Tanzania.
Muswada hup pia unawataka watu, ikiwemo familia, mwenye kila alichokiacha Mwalimu kukiwasilisha serikalini na kitanunuliwa ikiwa anayekimiliki kwa sasa atataka kupewa fedha. Akitoa zawadi serikali itashukuru sana.
Rose akasema, familia haipingani na wazo la kuwepo kituo cha kumbukumbu, lakini inapenda kuwepo na tofauti ya mali alizochuma Mwalimu akiwa Rais na baada ya kustaafu.
Binti huyo wa Mwalimu akaeleza kuwa ikiwa hilo litatekelezeka, basi wao watabaki kuwa masikini wasiokuwa na kitu kwa kuwa hata nyumba wanayoishi baadhi ya wanafamilia itakuwa ya serikali kwa maana ya kuwa sehemu ya makumbusho.
Rose akasema kuwa muswada huo unatamka kwamba, ikiwa watoto wa Mwalimu wataondoka duniani, basi hawawezi kuwarithisha watoto wao, kwa maana ya wajukuu wa Mwalimu.
Hapa Rose akaeleza kwa uchungu; Yaani mimi hata watoto wangu watanihukumu kwamba nilishindwa kutetea mali za babu yao kubaki mikononi mwao baada ya sisi kufariki, yaani jamani sisi tukifa ndiyo basi, hakuna wajukuu wala vitukuu wa kurithi mali za babu yao?
Akaendelea kulia: "Hatutakuwa na kitu, maana hata machapisho yake ambayo yalichapwa baada ya kustaafu yaliyoko katika familia ama kwenye Taasisi ya Mwalimu Nyerere yatachukuliwa ili yahifadhiwe na serikali katika kituo chake cha makumbusho.
Masikini..Rose alilia kimoyomoyo na kuonyesha machungu aliyonayo, aliondoka baada tu ya kuwasilisha mtazamo wa familia katika eneo la Bunge na kuungana na kijana mwingine wa Mwalimu, Madaraka aliyekuwa akimsubiri dada yake kutoka ndani ya jumba 'takatifu' la wabunge 'watukufu'.
Rose na Madaraka....hao wakaondoka. Rose alilieleza Bunge kuwa hataweza kusubiri kipindi cha michango na majumuishi ya waziri husika kwa kuwa, nadhani alikuwa na uhakika utapita na huenda akapata machungu zaidi ya maelezo ya waziri.
Kweli bwana, wabunge walianza michango yao na kila mmoja alikuwa makini kueleza msimamo wake, lakini hapa nawasifu kwamba waliweza kujitutumua na kuonyesha kuwa Watanzania wanatakiwa kumuenzi Mwalimu na Karume kwa nguvu zote.
Ukiusoma muswada huo, utagundua kwamba kweli yapo mambo ambayo yanatakiwa kutenganishwa, ya familia na ya serikali.
Kitu kimoja cha ajabu, wakati nikiwa nje ya bunge nikiongea na Madaraka, wakapita mawaziri fulani wawili waandamizi ambao walitoka ndani ya ukumbi wa bunge wakati Rose akianza kuwasilisha mtazamo wake.
Mara baada ya kupita, mmoja wa mawaziri wale, akagundua kuwa anayeongea pale ni mtoto wa Mwalimu, Madaraka, akarejea na kuanza kusikiliza alichokuwa akinieleza mtoto huyo anayeshabihiana na Mwalimu kwa rangi; nyeupe.
Akasimama nasi, lakini madaraka bila woga akaendelea kueleza msimamo wake ambao ulikuwa kama wa Rose kwamba serikali inataka kuwadhulumu baadhi ya mali zao halali kama urithi wao.
Kiongozi mwingine wa serikali, siyo waziri lakini ni miongoni mwa vigogo wanaoingia bungeni kwa nafasi yake, alionekana kukwerwa namwenzake kusimama pale, alisikika akisema, twende bwana, siwezi kusikiliza ujinga huo.
Du...nadhani madaraka hakusikia. Nilisikia kwa masikio yangu mazima mawili ambayo ninayaamini kwa kufanya kaze zake ipasavyo. Hayabahatishi.
keso yake magazeti yakaibuka na habari kibao, tena nzuri kweli na ambazo ziliuza kweli siku hiyo magazeti hayo.

Hiyo ndiyo habari iliyonifanya kuacha kumjibu mbunge aliyenitumia mail ya kunishutumu na kunitukana.
MUHIMU: Jana serikali ilitoa msimamo wake katika magazeti kuhusu hili la mtazamo wa familia ya Mwalimu kuhusu urithi wa baba yao. (nitasoma vyema na kuwaleteeni ya kuwaletea)





Thursday, November 25, 2004

Kumbe nao wanablog...endeleeni

SIKUAMINI macho yangu baada ya leo kufungua email yangu na kukuta waraka mmoja kutoka kwa mtu mmoja ambaye amejitambulisha kuwa ni mbunge. Hakutaja ni mbunge wa wapi na wala jina lake ni nani? Isipokuwa tu eti ameandika kutoka Dar es Salaam.
Waraka wake haukuwa mbaya sana, ulinifurahisha. Alianza kwa kunishutumu kwa kuwa eti nimeanza kuwafuatafuata waheshimiwa. Akaendelea kuwa eti nafanya hivyo kwa kuwa nina lengo la kwenda kugombea nafasi kama yake inayotukuzwa mno na wenyewe na hata wapambe wao.
Akaandika kwamba nimekuwa nikiwachoma vidole machoni na kuwatukana kwa kuandika kile alichodai kuwa ni uongo mkubwa. Akaenda mbali kidogo na kueleza kuwa ninawaonea wivu. Eti akadai kuwa siwezi kuupata uheshimiwa huo hata nikitambika uchi. Akasema hata kama nitagombea ahera siwezi kupata ubunge.
Kama kweli ni mbunge basi nampa sifa, akadai kuwa nigombee kwa watu wanaosoma intaneti pekee, labda huko naweza kushinda. Akauliza kwani hao wasomaji wa huo mtandao wako wangapi? Sijamjibu....nampangia majibu yake kesho.
Kitu kikubwa ambacho kimenipa moyo ni kwamba; kumbe na wao wanajua kusoma blog. Haya waingie basi tuwe tunapeana mawazo na zaidi sana sisi wenye akili tutapata mwanya wa kuwapa ukweli wao, hata kama watatutukana na kudai tunataka nafasi zao. Kwani nani kaandikiwa kuwa mbunge. Nani kamwandikia...si ni fedha zako tu ndizo sasa zinacheza! Tunajua na sasa wamenza kujipendekeza... mara ytasikia wametoa pikipiki, wametoa fedha za kujenga shule au kuwaita wapiga kura wao na kuwapa pilau. Du ajabu kweli yaani hawa wanachezea akili za kaka na dada zetu kwa kuwapa chakula cha kutwa. Ngojeni.
Najua wakiwa na blog, basi tutawaeleza ukweli ambao hautaogopwa na mhariri. Kwenye blog kila mmoja anakuwa na uhuru na nafasi ya kueleza 'Kona Yake'. Si mnakumbuka nilikuwa na Kona Yangu gazetini...mhariri na wakubwa wengine wakaipiga chini kiaina. Sasa nablog...sijui watanipata wapi. Situkani wala sifanyi uchochezi kwa yeyote, lakini ukweli natoa.
Nilipokuwa gazetini nilitaka kupambana kidogo, lakini mwalimu wangu mpenzi (amekuwa akinifundisha kupitia makala zake ambazo kabla ya kutoka kwenye magazeti yetu, zinapita mezani kwangu), anaitwa Rehema Nchimbi akaniambia: JITOLEE... USIJITOE.... UPOTEE. Haya ni maneno makali mno ambayo nimeyatunza na yatabaki kichwani kwangu siku nyingi mno....sina uhakika na kile kinachoelezwa kuwa milele (Nitaeleza mbeleni kuhusu hili).
Bahati mbaya sana nimeshindwa kui-link mail ya mtu huyo mbunge. Najitahidi (Macha hebu nipe darasa hapa).
Ukiisoma mwenyewe utazimia.
Ama hakika imenipa changamoto mno.



Tuesday, November 23, 2004

Ugomvi na wabunge ni kuuliza elimu yao

Ukitaka kuwa na maadui wengi wabunge wa Bongo, wewe anza kuwauliza elimu yao kila unapokutana nao, iwe Bungeni Dodoma, Dar es Salaam wanakoishi bila kwenda majimboni kwao au hata wanapopita tu huko walikozaliwa (majimboni kwao hawakai, sijui wanaogopa kuombwa au namna gani?)
Niliketi na rafiki yangu mbunge katika baa moja hivi karibuni wakati nikiwa Dom, alionekana kuwa muungwana kwani alinialika kwa chakula cha jioni. Chakula cha jioni kwa Doma maana yake ni ama nyama choma ama kuku wa kuchoma au supu ya kuku wa kienyeji na ndizi kadhaa. Maugali ya Kisukuma na vyakula vingine vigumu sahau kabisa.
Haya bwana tukiwa tunaendelea na mazungmzo yetu huku tukisubiri vyakula vyetu, tuliendelea na vinywaji na nadhani mbunge yule alifurahi sana baada ya kushindwa kutumia fedha zake nyingi kama alivyotarajia; maana nimesusa kunywa mibia. Nilikuwa napata kafanya kangu na kalipoisha nikabadili; nikanywa kasprite.
Tukiwa tunaendelea; mara mbunge mmoja aliyekuwajirani yetu, alikorofishana na mhudumu wa sehemu ile na hapo wanaanza kurushiana maneno.
mbunge alikuwa kitukana matusi makubwa na kila mara akimuita yule dada kuwa ni malaya....malaya mbwa wewe...utanielkeza nini wewe...kazi yako mpaka tuku....ndiyo uweze kuishi," alitukana mbunge yule ambaye alionekana kuwa amelewa.
Dada naye hakuona haja ya kumstahi...alikuja na matusi kibao huku naye akimrejeshea tusi lile lile la malaya;" malaya wewe mtu mzima hovyo, una watoto na mke, lakini bado unafanya umalaya bila kuogopa ukimwi...utaua familia yakomzee wewe,"
Aliendelea pia huku wabunge na meneja wa baa wakiwasili na kuwasihi watu wale kuacha ugomvi ambao ungeweza kabisa kuvuruga amani katika baa ile inayopendelewa na wabunge na viongozi wengine wanapokuwa Dodoma kwa shuhguli za serikali ama chama.
Akiwa anaondolewa eneo lile...dada akaporomosha bonge la neno lililooonekana kabisa kumchoma mbunge yule na kuonekana kutokwa na mipombe aliyokuwa ameifakamia kana kwamba kiwanda kilikuwa kinafungwa siku inayofuata.
"Mbunge mbunge nini...kwanza hujasoma... mtu mwenyewe darasa la saba...utanibabaisha nini wewe...shukuru tu vijisenti vyako ndivyo vilikupa mafasi hiyo..vinginevyo ungekuwa huko kwenu ukichunga kuku...paka wewe wa maziwa," alizomoka dada yule.
Kila mtu alicheka...lakini mie na mbunge niliyekuwa naye hatukucheka kwa sauti maana angesikia angeona kama nasituko pamoja na adui yake.
Mbunge aliyetukanwa...alinyamaza na kisha akapanua domo lake ambalo nina hakika lilikuwa likivunda kwa harufu ya mipombe aliyokunywa tangu mapema ya siku hiyo.
"Hata kama sijasoma mimi ni mbunge hjuwezi kulinganisha mimi na baba yako," alijitutumua. Kisha akanyamaza.
Aliponyamaza nikagundua kuwa maneno ya dadsa yule yamemchoma na muda mfupi baadaye akanyanyuka na kukodi taxi kurejea alikokuwa amefikia.
Nilikumbuka mbali kidogo...kwamba ukitaka kugombana na wabunge wetu wengi anza kuwauliza elimu yao.
Majibu unayoweza kuyapata hapo utachoka mwenyewe na tayari utakuwa umejenga uadui usiokwisha.
Wao wanasema....hata kama ni darasa la saba...lakini la zamani..huwezi kulinganisha na elimu ya kiwango hicho inayotolewa sasa.
Haya jamani...lakini nachojua mimi la saba ni la saba tu lilwe la mwaka 1970 au mwaka 2004.

Monday, November 22, 2004

Ubunge ni NGO zisizosajiliwa!

Kunapokuwa na vikao vya Bunge mjini Dodoma habari za kuandika zipo nyingi mno.
Mwandishi anayekosa habari huyo anakuwa hajui kazi yake; ukishindwa kuandika habari za vikao, ukishindwa kuandika habari za matukukio ya kijamii, yakiwemo ya kufumaniani na ukishindwa kuandika michango ya wabunge wetu, basi wewe unakuwa huna unalojua katika uandishi wa habari.
Wabunge bwana wana mambo kweli... yaani kila akitembea, akila, akinywa ni habari...ilimuradi wewe asikuone tu...jifiche kwanza.
Yupo rafiki yangu mmoja, Mbunge wa jimbo moja katika mkoa wa Morogoro alikosa bahati ya mtende baada ya kuambiwa kuwa ana wageni kutoka jimboni kwake.
Mbunge huyo alikimbia ile mbaya na kuwaeleza waliotumwa kumuita kwamba -hayupo.
Kumbe hao walikuwa wamemletea habari njema.
Nilipomuuliza mbona anakimbia wageni wake, alinieleza habari iliyoniacha hoi.
Eti kwamba watu wanaamini kwamba wabunge wana fedha nyingi hivyo kila watu mia wanaomfuata tisini wanakuwa waombaji wa misaasda ya fedha.
Kwa hiyo njia nzuri ni kuwakimbia na kuachana nao maana ukiwaona tu basi ujue zinakutoka ngawira kibao ambazo hazimo kwenye bajeti.

Alinieleza kwamba; "unajua bwana huku kwetu unapokuwa mbunge, basi unakuwa umesajili NGO ambayo haijaandikishwa rasmi."
Ahhh...kumbe ndiyo hivyo....haya kjazi kwenu mnaojiandaa kupambana mwaka kesho.
Macha utakuja kugombea? Nijulishe mapema na chama utakachokipitia ili nianze kupita pita kwa wazee na masangoma kuona kama jina lako linafaa

Saturday, November 20, 2004

Giza lachochea ngono!

Nimeandika mengi kuonyesha kwamba wabunge wetu wengi wao wanakuwa vikaoni wakiwaza mambo mengine na siyo hasa kuwakilisha mawazo ya wananchi hasa vilio vyao na shida zao za kila siku kama ukosefu wa maji, dawa na umasikini wa kupindukia.
Wabunge wetu wanashindwa kuonyesha umahiri wao wa kutetea wananchi kwa kupitisha ama kuridhia mikataba bila kuipita na matokeo yake yanaweza kuwa mabaya zaidi miaka mingi ama michache ijayo.
Lakini, miongoni mwa wabunge ambao wamenifurahisha katika bunge hili lililipita ni kuhusu mjadala kuhusu kigugumizi cha serikali ama shirika la umeme Tanzania kusambaza umeme maeneo mengi ya nchi.
Hakuna asiyejua kwamba umeme ni kitovu kikubwa cha maendeleo lakini hapa kwetu wanaopata umeme wengi ni wale walioko mijini, vijijini wao wanaona tu nyaya zikipita juu ya anga zao zikipita kuelekea mijini.
Mjadala wa kuishutumu Tanesco ulikuwa mkali kweli kweli huku wabunge wengi wakizungumza kwa uchungu jinsi wanavyochukizwa na utendaji wa shirika hilo pekee la kusambaza umeme nchini.
Wapo waliodai kwamba ikiwa wapiga kura wao wataendelea kukosa umeme na kuona nyaya tu, basi watahakikisha kwamba wanatuma simba wala watu kuwamaliza Waziri wa Nishati na Madini na Naibu wake.
Wawakilishi hao wa wananchi walihoji kulikuwa na ulazima gani wa kuwapa 'makaburu' kuiongoza Tanesco ikiwa bado umeme unakatikakatika hovyo?
Hivi hakukuwa na Watanzania wenye uwezo wa kuwa mahiri katika manejimenti ya shirika hilo ambalo, pamoja na kuwa pekee, huku likinunua umeme kutoka kwa 'wajanja wa Malaysia', bado linakuwa na utaratibu wa mgawo ama kukata umeme, wakati mwingi bila taarifa.
Mbunge wa Viti Maalum, Rhoda Kahatano kwa uchungu kabisa akasima na Spika akamruhusu kusema yake, du... akaanza kwanza kwa taratibu kwa haiba za kiualimu. Yeye ni mwalimu wa zamani.
Akaendelea na mara akapasua..;' Mheshimiwa spika, kukosekana kwa umeme kunafanya uzazi wa mpango kuwa mgumu zaidi, kila mahali ni giza tu...kwa hiyo hakuna cha kufanya isipokuwa ni kina mama kuzaa watoto wwengi bila mpangilio maalum.'
Heee...akasema tena kwa ushahidi kwamba katika maeneo mengi ambayo hakuna umeme kuna watoto wengi mno kutokana na kwamba wazazi wao wanatumia giza ku....bila mpangilio. Kweli....kama kungekuwa na umeme labda wazazi wao kabla ya kwnda kulala wangesoma vitabu na magazeti au hata kucheza bado kusogeza muda.
Lakini pasipokuwa na umeme, mshumaa ukiisha tu ama kandiri kukosa mafuta...basi baba atapanda kitandani na mama atafanya hivyo na hapo kazi inakuwa moja tu; kutengeneza watoto bila mpangilio.
Alichosema ni kweli nami nikamuunga mkono kwa kuandika habari hiyo ambayo mhariri wangu aliipa kipaumbele na kuiweka kuwa 'lead' story, wasiojua uandishi ni kwamba ikawa habari ya kuuza gazeti...kuubwa ukurasa wa mbele na kweli ikauza kweli wiki hiyo.

Sasa serikali ina mradi wa kusambaza umeme vijijini..ninaiomba iharakishe kufanikisha hili ili tuweze kuwa na uzazi wa mpango.
Bila umeme, uzazi wa mpango utakuwa ni ndoto...basi serikali iharakisjhe utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini kwa kuishirikisha Tanesco na kuacha ndoto za kutoihusisha...kazi hiyo itakuwa ngumu zaidi.

Wabunge wetu ni kupitisha tuuuu...haya!

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu kidogo baada ya kutoka Bungeni, nadhani ni zaidi ya wiki moja sasa. Niko Dar naendelea na kuandika habari katika magazeti yetu.
Sikuweza kuwaeleza mengi kutoka huko kwa 'waheshimiwa' kwa kuwa gharama, kama zilivyoeleza ni kubwa mno.
Nilisema nilipewa kitu kidogo sana cha kuniwezesha kuishi Dodoma kwa siku 14, ambacho kidogo hichoi ilibidi nianze kukigawa nikiwa bado Dar; Niache nyumbani kwa Kina Comfort Rita na Collins (watoto wangu) na mama yao fedha za dharura na pia kuhakikisha kwamba chakula hakikauki kwa kipondi chote. Pia nilipe umeme na maji ili yasikatwe wakati sipo. Kufika Dom nihakikishe nalala na kula na kubakiwa na fedha za gharama za mawasiliano. Du...mambo yakawa magumu kidogo.
Kwa hiyo kutokana na hali hiyo ilibidi nijipe likizi kodogo kwenye blogu yangu. Poleni sana kwa kusubiri mengi kutoka Dom, hata hivyo nasema hakijaharibika kitu. Naanza kuwaletea yaliyojili huko angalau kwa vipande kidogo kidogo.
Ana kweli Wabunge wetu wamechoka, sijui wana umuhemuhe wa uchaguzi ujao au sijui ni kitu gani. Kila mmoja mwelewa alikuwa kipigwa na butwaa kwa jinsi waheshimiwa hao walivyokuwa wakila shushu bila kufanya kazi tulizowatuma.
Hivi nikisema kwamba walikuwa wakipewa fedha za bure, kwa maana ya sh. 80,000 kwa saa chache wanazokuwa ndani ya nyumba 'takatifu' nitakosea?
Hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika. Ninasema hivyo kwa sababu.
Sikiliza...ilikuwepo miswada kibao ya kupitishwa na wao kwa maana ya kuwawakilisha wananchi, wasomi na wasiokuwa wasomi.
Miswada ilikuwa sita, kama sikosei, mingi ikiwa ni ya kuridhia mikataba ya kimataifa ili Tanzania kama zilivyo nchi nyingine iweze kuwa na utambulisho kwa wakubwa wa dunia hii wakiongozwa na Kinara wao, Marekani.
Miongoni mwa muswada ulioniacha hoi, pamoja na wenzangu..waandishi makini ni jinsi wabunge walivyokuwa wakipitisha miswada hiyo.
Kilichokuwa kikifanyika, baada ya waziri husika kusoma muswada wake na kuwataka wabunge kuchangia kabla ya kuridhia, hakuna mbunge aliyechangia na wengine waliokuwa wamejiorodhesha awali kuingia mitini. Walipoitwa hawakuonekana.
Ilinishangaza mno katika muswada wa kuridhia mikataba ya kimataifa ya nguvu za nyuklia. hapa sikuona hata mmoja na baada ya kusomwa na kiongozi wa bunge kuwahoji wabunge kama wanaridhia, waliokuwepo wote walipiga kofi meza zao kuonyesha kwamba wamepitisha.
Du...upitishaji huu uliniacha hoi kwa karibu miswada yote ya kuridhia.
Hivi wabunge wetu ina maana kwamba kila kinacholetwa kwao wao kazi yao ni kukikubali tu bila hata kukichunguza na kukisoma na kukubaliana nacho. naelezwa miswada ya namna hiyo huwafikia kabla ya wiki mbili kuanza kwa kikao. Hivi kwa staili hii nitaamini kwamba wanaisoma, au wanapopokea makabrasha wanapokuwa kwao (siyo majimboni, maana wengi tunapigana makumbo hapa Dar na maeneo ya mijini tu) huyaweka katika makabati yao na kuacha wakisubiri siku ya bunge kuchukua posho?
Hakika maswali ni mengi yasiyokuwa na majibu...wanafanya nini huko Dodoma Bungeni? Au labda tunao wabunge wasiokuwa na uwezo?
Naweza kueleza kabisa kwamba kuhusu muswada wa nyuklia labda ulihitaji nguvu ya ziada ya kujua masuala ya sayansi, lakini kwao ambao ni wabunge wasiokuwa na ujuvi wa masuala hayo kwani wanakatazwa kuwaona wataalamu na kuomba maoni yao?
Najua wabunge wetu, wengi wanaamini wanapokuwa bungeni basi wana akili na ufahamu kuliko watu wengine wote, hili ndilo tatizo linalowafanya kushindwa kutafuta maoni ya wapiga kura kwao kwa kuogopa kuitwa vihiyo.
Kitu kingine kibaya ni kwamba mikataba hiyo ya kimataifa na hata mingine ya hapa nchini inaandikwa kwa Kiingereza na wabunge wetu wengi hawajui lugha hiyo ya kikiloni, siyo kosa lao nawapenda kwa kuwa wanakitukuza Kiswahili. lakini mbona hawasemi na ikatafsiriwa jamani kwa lugha nyepesi ya kwetu?
Ajabu kabisa hii.
Ubaya wa kuingia mikataba ambayo wabunge wenyewe hawaielewi ni makubwa zaidi. Madhara hayo yanawezxa yasionekane leo ama kesho, lakini watoto na wajukuu wetu wakabeba mzigo ambao wabunge wetu kwa kutoelewa waliliingiza taifa katika shimo lisilo na kina cha kujinusuru baada ya kutumbukia.
Yapo mengi, Nitayaeleza baadaye.
Ninaandaa gazeti langu...sorry...la Mzalendo linalomilikiwa na CCM ili kesho watu wasome. Najua wanaosoma ni wachache, sijui hawana fedha za kununua ama ni wavivu kusoma (nitajadili baadaye hili).
Baadaye.

Thursday, November 04, 2004

Mambo yameiva

Nilisema. Lazima kitatokea cha kutokea hapa Bungeni. Nani amekuja kujadili mustakabali wa Tanzania. Nani ana utaifa.
Haya siku ya kwanza tu kufika, yaani kuanza kwa kikao cha Bunge, usiku wake ikawa mambo kama kawaida.
Mbunge 'akafumaniwa' na mkewe akiwa na totozzzz. Ikawa heka heka ndani, wakavunja hata vitasa na kuumbuana waziwazi kwa watu waliokuwepo humo hotelini. Sina uhakika kama mama alitumia silaha yake ya kung'ata kama ilivyo kawaida ya wake zetu wengi wa Kiafrika, hasa Kitanzania.
Haya utabiri wangu ukawa umetimia. Nilisema.
Ngojeni nitakuwa nanyi punde, ingawa mikono yangu inatetemeka...sijui iko namna gani hii, yaani nikitabiri tu inakuwa kweli.
Nilisema awali kwamba huku Bungeni ambako wao 'waheshimiwa' wanapaita patakatifu kuna vituko kweli vya kustaajabisha. Kazi inayowaleta hapa ni kujadili mustakabali wa nchi, lakini wengi wao wakifika tu basi utadhani ndiyo wanatoka jandoni. Kazi kubwa inakuwa ni kutafuta vimwana...ni kunywa mipombe kibao na kula minyama ya Mnadani.
Kutokana na hili, kiongozi wao, Spika aliamua kuwataka kila mmoja wao kuja na mkewe ama mchumba kwa wale ambao hawajaoa ili kukomesha aibu ambayo ilitaka kuwa 'kawaida' ya wabunge, wawakilishi wa mawazo ya wananchi.
Naona nitaacha sasa uandishi huu na kuanza kazi ya Kina Sheikh Yahya.
Subirini kidogo...

Monday, November 01, 2004

Niko Bungeni Dodoma

Nyama choma, moja moto na moja baridi hapa Dodoma, ndiyo biashara ambayo kila mmoja anaifanya, wenye mtaji mdogo twende, wenye mkubwa naohali kadhalila. Hii inatokana na sababu moja kuwa;kipind cha mavuno kimefika.
Nani kakwambia kwamba Watanzania ni mbumbumbu wa uchumi, wacha bwana wanajua ile mbaya. Mbona wanaweza kujuamasuala haya ya demand and supply. Wote wamekwenda shule, basi tu wanapakaziwa eti ohhh hawajui uchumi na biashara na woga kuwaingiahata viongozi wegtu kwamba Wakenya na Waganda watateka soko zima a ajira katika sekta hizo.
Haya...haba Dom kama inavyojulikana kwa wengi, hali ya hewa ni nzurikiasi, joto lipo ingawa siyo kama la Dar.
Ya kuandika kuupa hali ya hapa ni mengi, lain noja kwanza, wajua kwamba kuchat au kusoma mail hapa ni aghali mno na vijiposho navyopewa na bosi wangu havitoshi, kwana vinapunguzwa nikiwa bado dar niache nyumbani, mama watoto naye apate kiasi cha kubadiisha mboga, nije hapa nauli, gharama za simu, kulala, kula na ni bahati nzuri tu kwamba sasa nimesimama masuala ya kinywaji, ndiyo nanipa unafuu kidogo naweza kuishi bila taabu sana.
Hapa kuanzia kesho ni maswali, majibu na vichekesho kibao ndani ya Bunge letu lililopachikwa jina la utukufu kwa maana ya kuwa na hali ya Umungu Mungu, makubwa haya! Mengine yanayofanyika huko hata chembe ya huyo wanayejaribu kumtukuza hayako naye, tena ni machukizo mbee yake.
Nitaandika mengi mno...kaa mkao wa kua....nitaupa vipande vyahapa ili mjue wabunge wetu wako namna gani...mana niliwahi kuandika kuhusu ubinge wao wakaja juu kama kifuu cha nazi na wengine kudai eti waandishi tunawaonea wao wivu kwa kuwa wanaendesha magari makubwa ya kifahari wakati watu wao hawana uhakika wa mlo mmoja, eti kwamba tunawaonea wizu kwa kuwa wanakua vizuri nyama choma na bia tena kwa uhakika na siyo tu wanapokuwa Bungeni abako posho yao tu ya siku moja ni mishahara ya watumishi wa serikali zaidi ya wawili wanaolipwa kima cha chini kwa muda wa mwezi mmoja. Wao wanachukua kwa saa chache tu wanapokaa ndani ya jengo kubwa lenye viyoyozi.
Du..nngekuwa na kalaptop kangu na Bensonline kwa maana ya wireless internet connection, ningekuandikieni mambo kibao, lakini sasa sina cash, ngoja niache na ya kesho.
Nipeni taarifa mwataka nini huku Dodoma? Zabibu, muguu ya mbuzi au nije na bakuli la kuoba misaada
Alamsiki

Thursday, October 28, 2004

Kumbe uwekezaji ni uchukuaji jumla!


MARA nyingi nilikuwa nikiandika kuhusu jinsi utandawazi na hasa uwekezaji na ubinafsishaji wa hovyo unatakavyowaacha watu masikini wa Tanzania kuwa masikini na fukara kuliko maelezo.
Hayo niliyaeleza katika safu yangu iliyokuwa ikichapwa katika gazeti la kila Jumapili la Mzalendo linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi.
Hata hivyo, baadhi ya watu, hasa wanafiki walinijia juu wakidai kuwa nina lengfo la kuchonganisha dola na watu wake. Wenye welewa na wenye akili waliniunga mkono kwa asilimia nyingi huku wakitaka niendelee.
Sikupenda kukorofishana na wakubwa wangu, nikaamua kuacha kuandika. Sasa nashukuru nimepata uwanja mpana zaidi, usiokuwa na mwenye meno ya kuning’ata eti nisitamke mawazo yangu hadharani.
Sipendi kuumia katika kificho, nikiwa lipo nlinalonikera, nasema bila kujali nani anawazo nini ama ana mtazamamo gani tofauti na mimi.
Najua sina haja ya kuifanya jamii yangu wala nchi yangu ninayoipenda sana kuingia katika vurugu ama uvinjifu wowote wa amani ambayoimetafutwa, ikalelewa na hata sasa imekua na kuimarika.
Kazi ya kutunza amani ilifanywa na wazee wetu, wapendwa wetu na watu waliokuwa na uchungu na nchi hii na watu wake. Watu wasiokuwa na chembe ya unafiki wala umamluki. Walikuwa wenye kutamka bayana bila kuwaogopa wajomba wao wa Ulaya na Marekani kwa kuwa tu wangeweza kukatiza misaada yao ambao ina riba! Msaada halafu uwe na riba, toba!
Walipokuja wawekezaji na kupigiwa debe mno kwamba hauepukiki, kila kitu wakachukua na wanaendelea kuchukua, bila kuwa na huruma yoyote, kisa eti oooh tunalipa kodi na tuko hapa kisheria! Nani kawapa hiyo sheria, wananchi au viongozi!
Mwananchi gani alishirikishwa kuwapeni mkataba hiyo…mbona kama ni dhahabu mnajichimbia tu na hata nimeshuhudia mkikataza baadhi ya viongozi wetu kuingia kwenye vyumba vya dhahabu mnayochimba.
Mbona hamrudishi kiasi cha kutosha kwetu mnapojichimbia tu bila kuwepo usimamizi wa wenye mali walio makini? Mbona mnadanganya kuwa mnachimba kiasi fulani kumbe ni zaidi na mnasafirisha zaidi.
Mbona hizo fedha zenu za mauzo hamzihifadhi hapa mnazipeleka kwenu, kisa eti oooh transaction zote zinafanywa na makao makuu. Kumbe nyie mnachotaka ni dhahabu yetu tu, lakini hata kumbe mkiweka hapa fedha zenu lazima zitarudi tu kwenu kwa kuwa hata benki zote ni zenu…
Katika safu yangu moja nikaeleza kuwa uchimbaji huo unaofanywa na wataalam hao kwa kutumia mashine za kisasa, ni kwamba wanachukua na kuchota hata chembe ndogo za dhahabu na kuacha mashimo tu.
Wakimaliza enbeo moja wanahamia jingine na uchimbaji unaendelea bila kukoma, baada ya miaka kadhaa, mashimo tupu yanabaki. Hakuna dhahabu, hakuna udongo, miti na uoto mwingine wa asili vimeuawa kwa uchu wa mali za Watanzania.
Mama Tanzania nani aliwaruhusu hawa, kumbe bora haya madhahabu yangebaki hukoo huko ardhini na labdfa ungefika wakati wajukuu wetu wangeyachimba na kuyauza tena, wakati huo kwa bei kubwa kichizi.
Baba wa Taifa katika kuubwatukia ubeberu wa dunia unaoingia katika nchi changa kwa staili mpya za utandawazi na ugenishaji, alisema maalmasi, madhahabu na madini yote yaachwe tu, kwani huko yataoza? Mbona nasi tumeyakuta na tukaona bora kuaacha kwanza…muda ungefika yangefanyiwa kazi kubwa tena ya maana na yenye kuleta maendeleo zaidi kwa watakaokuwepo.
Ahhh jamani ngoja nipunguze kwanza hasira zangu kwa kunywa kahawa, nikimaliza naendelea..
Haya nimerejea, sasa nasema hiviiii....hao tuliowakodisha ama kuwawekeza, basi muda wao metosha na kile walicholipa kinatosha kabisa kununua mitambo na mashine zetu ili tuanze kuyachimba madini yetu wenyewe na tuyaize wenyewe.
Kama hizo fedha zitakuwa hazitoshi, basi tukope mahali popote, kama waungu ha watakataa na mabenki yao ya dunia na mataasisi mengine ya fedha na 'misaada' basi tuyatose na tukamuone Ghadafi, najua sasa anaweza kutukopesha tena kwa moyo mmoja. Kama naye ataonekana analeta gozigozi...basi wenyewe kwa wenyewe tuchangishane..kutunisha mfuko na tuanze kazi. Hao wataalamu wetu nao wa madini watajitolea kwa kuanzia.
Mwaonaje mawazo haya ndugu zangu...tuko pamoja..ndiyo mzeee
Tukijaaliwa

Tuesday, October 19, 2004

A letter to the late Mwalimu Nyerere

Dear Mwalimu,
This is October 14, so everybody around here has this moral and patriotic responsibility, to remember you. somehow. Many changes have taken place since you passed away five years ago then.
Believed it or not, but Daniel Arap Moi is no longer the President of Kenya. His crown has been taken over by a guy known as Mwai Kibaki, whose first name is Emilio .... It rhymes with Chameleon! However, as we were going to press, it wasn't quite clear who exactly was in charge at the Kenyan State House .... Mr or Mrs Kibaki?
Believe it or not, Yoweri Museveni is still the President of Uganda and unless another Idd Amin comes along to "Obote" him, the mischievous fellow will still be Headmaster of the Kabaka country, this time next year .... And the year after. But he is a nice guy, that old Museveni. He was here in Arusha last February and admitted in public that he is no longer a "Mulokole!" Which means, while millions of East African residents are currently turning to Jesus, Yoweri has just decided to drop Christ. Who needs a Savior when you have the entire armed forces behind you? .... This may well be the reason why the "Lord's resistance army" is giving Kabaka Museveni a run for his troops.
By the way, East Africa has just lost another strong Field Marshall; Idd Amin Dada, the one and only conqueror of the British Empire, died recently at his retirement home in Saudi-Arabia .... Of course you never really liked him very much.
And did anybody tell you that the continent has already gone to the dogs? Believe it or not, the situation here is far much worse than during the colonial era. To make the matter worse, we have run out of strong leaders. There are no more people like you or Patrice Lumumba, Kwame Nkurumah or Samora Machel to advocate for Africa.
The other surviving leaders who were once great fighters are now as strong as Little Miss Muffet who used to be afraid of spiders .... Or something.
Take Nelson Mandela for instance, as soon as he retired from South African Presidency, he succeeded you as the negotiator for the Burundi Peace accord in Arusha, but Madiba forced the Hutus and Tutsis into premature reconciliation then fled from Arusha, like a bat out of hell. You can't blame him either. Imagine such an International figure to be compelled to rely on water being pumped by the Arusha Urban Water Supply Authority (AUWSA) .....
Never mind, but as soon as he got back to his country, Nelson went into showbiz. He was not to be seen again until a few months ago when he turned up in public, embracing, Mrs Graca Machel and declared that, he was retiring. In his own words, Madiba was retiring from, "Retirement!" He still has sense of humor.
Remember Jerry Rawlings? Well, after being chucked out of the Ghanaian State House, old Rawlings has been reduced into a mere puppet of the United Nations, going around as a messenger for .... Okay, lets face it, HIV-AIDS! Kwame Nkurumah must be turning in his grave.
Mummar Gaddafi, the President of Libya, used to be tough, strong and outspoken. He would even scare the former American President, Ronald Reagan out of his wits. As of the present, Gaddafi has turned into a dinner lady.
Last year, the current US Principal, George Bush Junior, beat the daylights out of the notorious King of Baghdad, His Sovereign Saddam Ole Hussein, under allegations that, the Iraq Laigwanan was hiding deadly spears in his Boma. The smitten son of Hussein was forced to seek refuge in the nearest mouse hole, at his home village of Tikrit, before being exhumed out of that grave just in time for Christmas 2003 Holidays.
Fearing that he may become the next victim, Gaddafi, the Chief commander for the Libyan defense forces, raised a white flag of mercy to the Sultan of Washington DC, begging to be inspected lest he also had machetes under his bed ..... I weep for Africa.
The rest of allegedly African leaders are now earning payrolls as public relation officers for the western companies. They are so pathetic that the Prime Minister of UK Tony Blair, constantly summons them into his, 10 Downing Street office, squeeze five of them in a single settee, before proceeding to lecture them on something called, "The African Commission!"

*****
  • Posted to me by a friend, written by Marc Nkwame of Tanzania

Ulisikia muziki wa 80's

Nakumbuka kuwa muziki wa miaka ya 80 ndiyo hasa uligusa zaidi idadi kubwa ya mashabiki kuliko ilivyo sasa. Ninachoweza kusema ni kwamba katika miaka ya hivi karibuni, wazee wanaonekana kusahaulika katika muziki kutokana na ukweli kwamba vijana wanapiga muziki wenye kwenda sambamba na rika lao. Kila rdio ni rap tu, wazee kweli wataweza?
Haya sasa nawakumbusha wazee wenzangu muziki wa miaka hiyo. Kong'oli hapa upate vitu!

Monday, October 18, 2004

Waingereza mpeni kazi Tsvangirai

WIKI iliyopita vyombo vya habari vya magharibi, Marekani na Uingereza vilipambwa na habari kutoka Afrika iliyokuwa kubwa mno kwao. Ilipewa uzito mkubwa kwa kuonekana kwenye kurasa za mbele za magazeti mengi ya nchi hizo.
Mbali na magazeti, vituo vya televisheni vya nchi hizo vinavyoonekana sehemu kubwa duniani ikiwemo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na CNN ya Marekani pia havikuwa nyuma kuitangaza habari hiyo.
Vituo vya redio navyo vilikuwa vikiunguruma kwa habari hiyo hiyo iliyoonekana kuwa muhimu mno kwao.
Habari iliyokuwa ‘ikiimbwa’ na vyombo hivyo ni kuhusu kuachiwa na Mahakama Kuu kwa kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC, Morgan Tsivangirai.
Kutangazwa mno kwa habari hiyo kunaonyesha jinsi nchi hizo zinavyoshabikia na kutaka kuendelea kuwepo kwa matatizo, siyo kwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, bali kwa wananchi wengi wa nchi hiyo.
Maana ya kushabikia habari hiyo ya kutokuwa na hatia ya tuhuma za uhaini na kula njama za kumuua Rais Mugabe inaeleweka; nchi hizo za magharibi zinafanya hivyo kwa kuamini kuwa ni ushindi mkubwa kwa kibaraka wao ambaye yuko tayari kuuza utaifa na wa wengine wanaomshabikia kwa faida yao.
Kabla ya kuonekana hana hatia, vyombo hivyo hivyo vilikuwa vikitangaza kila siku kuwa uendeshaji wa kesi hiyo na mahakama za Zimbabwe haziko huru kwa kuwa zinashinikizwa na Rais Mugabe.
Vyombo hivyo vilikuwa vikibashiri kuwa Tsivangirai atahukumiwa kifungo cha maisha, hukumu ambayo eti Mugabe na serikali yake wameishaipanga.
Ni wazi kuwa Marekani na Uingereza zinamchukia Mugabe na serikali yake kwa kuituhumu kuwa haina mwelekeo na kwamba haijali haki za binadamu za Wazimbabwe.
Sababu za kumchukia Mugabe ni kutokana na msimamo wa kiongozi huyo usiotetereka wa kutetea jamii pana ya Wazimbabwe ambao, kwa miaka mingi walikuwa wakinyimwa haki zao na Wazungu wachache walioko ndani ya nchi hiyo.
Msimamo wa Mugabe ambao umewafanya Wazungu hao kumchukia ni kuruhusu Wazimbabwe, hasa waliopigana kuikomboa nchi hiyo kuvamia mashamba makubwa na yenye rutuba yaliyokuwa yakimilikiwa na Wazungu na kujimilikisha.
Nchi za Uingereza, ambayo Wazungu wengi wa Zimbabwe wana asili yake, ilipigia kelele hatua hiyo ambayo iliitwa kuwa inakwenda kinyume cha haki za binadamu na demkrasia.
Walichofanya wananchi wa Zimbabwe ni kuchukua ardhi yao iliyokuwa ikitumiwa kimabavu na Wazungu hao ambao walikubaliana waiendeleze kwa miaka 10 baada ya kupatikana kwa uhuru wa nchi hiyo mwaka 1980 na baadaye kugawana na wananchi.
Wazungu hao walikuwa wamehodhi ardhi kubwa mno, tena yenye rutuba huku wananchi wazawa wakinyang’anyana sehemu ndogo ya ardhi isiyokuwa na rutuba kwa kilimo na shughuli zingine.
Miaka 10 ikapita na mingine kwa idadi hiyo ikapita, hakukuwa na lolote lililokuwa likifanyika ili kugawana ardhi hiyo na wananchi wengine, na ndipo wananchi walipoamua kuchukua ardhi yao kwa kuwavamia Wazungu hao. Vuguvugu la kuchukua mashamba kutoka kwa wakulima wakubwa wa Kizungu lilianza mwaka 2000.
Na kuanzia hapo, serikali nayo katika utaratibu huo wa kuigawa ardhi ya Zimbabwe upya, ilichukua zaidi ya mashamba makubwa 5,000 ya Wazungu na kuyagawa kwa familia 200,000.
Suala hili lilipigiwa mno kelele na vyombo vya habari na viongozi wa magharibi wakimtaka Mugabe kuacha kuchukua mashamba ya Wazungu na pia kuzuia wananchi kunyang’anya mashamba kutoka kwa Wazungu. Mugabe hakuwa upande wao, alikataa na kuwatetea wananchi wake.
Hasira za Uingereza zikamwangukia kiongozi huyo na kuanza kumwita kila aina ya majina mabaya; ikiwemo dikteta. Marafiki wa Uingereza, Marekani Australia na nchi zingine vibaraka zikaiunga mkono kumshutumu Mugabe na serikali yake.
Katika kuonyesha hasira zao, Uingereza ikakatisha kila aina ya misaada iliyokuwa ikitoa kwa Zimbabwe na kuwashawishi marafiki zake kufanya hivyo, eti kwa lengo la kuiadabisha nchi hiyo ya Afrika.
Sasa ili kupata kile wanachokitaka, Uingereza ikaona vyema kutumia kibaraka, ambaye ni Mzimbabwe ambaye atakuwa akitumiwa kuonyesha kuwa wapo wananchi, Wazimbabwe wanaompinga kiongozi wao.
Hapo ndipo ushabiki wa Wazungu kwa Tsivangirai ukaanza, wakiwa na imani kuwa malengo yao yatafanikiwa, ili kujenga picha kuwa Mugabe na serikali yake inapingwa kwa kiasi kikubwa na wananchi anaowaongoza.
Hivi sasa Tsivangirai anapewa kiburi na mataifa hayo ili tu kutimiza malengo yao ya kumpachika kuwa kiongozi wa Wazimbabwe, wananchi nao ‘wamemshitukia’ ndiyo maana hawakumpa nafasi ya kuongoza. Alishindwa vibaya katika uchaguzi mkuu.
Kwa kuwa Tsivangirai ameshindwa katika uchaguzi wa Zimbabwe, basi ni vyema Uingereza ikampatia kazi katika serikali yao au vyama vya wafanyakazi vya huko kwa kuwa yaelekea nchi hiyo tajiri kwa viwanda inampenda mno.
Kama kunywa naye chai haitoshi, basi ni bora Uingereza au Marekani impe kazi Tsvangirai.
Tsvangirai ana taaluma ya vyama vya wafanyakazi, kwa hiyo kama Waingereza wataona anafaa basi asaidie katika sekta hiyo.

Friday, October 15, 2004

Kwa staili hii, Nyerere atabaki na mwenge tu!

NIMEKUWA nikifiri kila kukicha ni namna gani watu, hasa Watanzania wanaweza kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Mungu amlaze mahali pema) kwa vitendo na kwa uwazi mkubwa.
Mengi yanafanyika, wapo wanaodhani kumuenzi Baba wa Taifa ni kuchonga sanamu zinazoonyesha sura yake katika kumbi na viwanja vyao, lakini ukweli ni kwamba hiyo haitoshi, hata kama utachonga sanamu kwa kutumia dhahabu na lulu.
Wapo pia, hasa wanaojiita wasomi waodhani kumuenzi mzee yule ni kuandaa semina na makongamano kwa kutumia fedha za wafadhili na kuwaita watu wa kada kama ya kwao, kuzungumza mazuri ya Nyerere. Hili, pamoja na kwamba linaweza kuwa na mtazamo mzuri, lakini bado lina upungufu mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya hao wanaoendesha makongamano hayo hawaonyeshi kwa vitendo vyao, kuwa kweli wanamthamini Mzee huyo wa Butiama na Tanzania.
Alaa…nataka kuwasahau…wapo pia wanaoeleza kupanda Mlima Kilimanjaro eti kwa kumuenzi Baba wa Taifa. Hii ni sawa lakini nayo, ina walakini maana hata hao waandaaji wakiangaliwa nyuso zao, mmmh…ni tofauti kabisa na matendo ya kumuenzi Baba wa Taifa.
Hatuwezi kudanganyana maana sisi, wenyewe kwa wenyewe tunafahamiana. Nani mnafiki, nani anafanya nini kwa uwazi na kwa dhati kabisa. Tunajuana kuwa baadhi yetu wanafanya hivyo ili tu kwamba waweze kuandikwa na vyombo vya habari, hasa kuonekana kwenye luninga (TV) wakijidai wanamuenzi Mzee huyo.
Wengi wao ni wanafiki, ni wala rushwa, ni wategezi wa kazi, ni wafujaji wa mali za umma, ni waongo.
Mbona hao hao wameshindwa kukemea mabaya yanayotokea kila kukicha nchini na sasa yameanza kuota mizizi kama vile kuwepo kwa rushwa (hili linaoyesha juhudi pekee za Rais Mkapa zimeshindwea, hapewi ushirikiano wa kutosha), askari kujichukulia sheria mikononi mwao kwa kuua watu wasiokuwa na hatia kwa visingizio lukuki.
Mbona wanashindwa kuwasaidia maskini kuondokana na ufukara wao, mbona ndiyo hao hao wanaoanzisha vyama visivyokuwa vya kiserikali kwa lengo la kujineemesha kwa kushibisha matumbo yao na watoto wao.
'Mbona' hizi ziko nyingi na zinaendelea tu…mbona wanashabikia kuvunjika kwa muungano, mbona wanafurahia wala rushwa (hili nitalisema kwenye mawazo mengine baadaye), mbona hawapigi kelele wanapoona haki zao zinadhurumiwa na watendaji. Mbona….mbona….mbona.
Hao wote wanaojionyesha, lazima kuna 'mbona'…mbona na mbona. Basi ngoja niwaache kwanza hawa.
Ni kutokana na mbona hizo, ndiyo maana yale yote yaliyoanzishwa na Mwalimu Nyerere yanaonekana kusahaulika, tena kwa haraka zaidi na yanakumbukwa tu siku ya kuadhimisha siku aliyotutoka duniani.
Hivi kweli, ni akili gani hiyo ya kuwakumbuka wazee wetu siku tu wanapotimiza miaka kadhaa wakiwa kaburini? Huu ni unafiki.. tuuache sasa.
Ni vitendo pekee vya wahusika hao ndivyo tunaweza kuvithamini ikiwa wataona na kutambua kweli Watanzania wanateseka kwa umasikini uliokithiri na kutafuta mbinu za kuutatua. Au labda watu hao kusaidia kuikomboa jamii ya Watanzania kutoka katika umasikini mkubwa wanasubiri wakiwa marais wetu. Ajabu!
Nina wasiwasi, ikiwa unafiki huu wa kumuenzi Baba wa Taifa utaendelea, baada ya miaka 15, hakuna hazina ya Nyerere itakayokuwa ikikumbukwa. Siyo Muungano, siyo uongozi bora, siyo uwajibikaji, siyo haki, siyo…..Azimio la Arusha limekwenda na hivyo vingine, iwapo atakosekana wa kuvisimamia na kuvipigania, navyo vitafuata.
Kitakachobaki sana sana ni mwenge tu, kwa kuwa sijaona mtu mwenye akili timamu akiupinga kuwepo kwake hasa baada ya kuwa umechukua sura ya kitaifa zaidi na siyo itikadi za chama chochote.
Mungu atupe uzima, tuone yajayo…labda tutakuwa na mchango wa kuyageuza.

Wednesday, October 13, 2004

Tuache unafiki kumuenzi Nyerere

Ndugu zangu,

Watanzania wanaungana na wapenda amani, maendeleo na haki kote duniani katika maadhimisho ya miaka mitano ya kukumbuka siku Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipoaga dunia hii ya wadudi. Alifariki London Oktoba 14, 1999.
Ndiyo ni dunia ya wadudi kwa kuwa imefika mahali ambapo kila mtu sasa anaishi kivyake; anachojali ni yeye na tumbo lake, la mkewe na wategemezi wake. Hakuna anayemuwazia mwingine kwa haki.
Hali ni mbaya mno kwa baadhi ya viongozi wetu ambao wanaonyesha dhahiri kuwa wamepewa kisu kikali na kazi yao kubwa ni kukata kila pande la nyama linalokatiza mbele yao hata bila kuhoji ni nyama ya mnyama gani. Wao wakiona tu kuna damu na mfupa, wanajua inaliwa na hawana mwiko.
Dunia ya namna hiyo Nyerere aliipiga mno vita na hakuwa na umunyemunye wa kubabaikia Wazungu au matajiri, yeye alisimama katika ukweli kwa maana ya kuthamini kila mmoja na zaidi sana alitaka usawa, haki a maendeleo ya pamoja.
Ni kutokana na msimamo wake, Mwalimu Nyerere awali alitokea kuonekana kuwa kikwazo kwa wakubwa wa dunia, Wazungu kwa kuwa tu hakutaka kuburuzwa na kila aina ya maneno yao matamu kama asali lakini machungu kama shubiri yanapoifikia ngoma ya sikio.
Nyerere, nakumbuka kusoma mahali kwamba alikosana mno na Wafaransa ambao aliwaomba kusaidia ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Kilombelo, lakini wao, kutokana na nia zao zilizofichika walitoa masharti kuwa wapewe eneo la Zanzibar ambako wataweka kituo chao cha kijeshi.
Mwalimu aligoma, alikataa tena mchana kweupe. Wakanywea na kuondoka na misaada yao.
Ni Mwalimu huyo huyo aliyekosana na Waingereza kwa kuwa nchi yake iligoma kufuata masharti kwamba Tanzania iache kuwasaidia wale walioitwa na Wazungu hao kuwa magaidi wa Afrika Kusini kwa maana kwamba wananchi wa Azania waliokuwa wakipinga kuwepo kwa ubaguzi wa rangi na uongozi wa nchi yao kushikwa na wazungu wachache.
Misimamo ya Mwalimu inaweza kuelezwa kwa urefu zaidi, lakini ni mingi mno kiasi kwamba inahitaji wino mwingi, sawa na wingi wa maji ya Ziwa Viktoria, ingawa wino huo utakwisha na bado sifaze hazitakwisha kamwe.
Ninawaomba viongozi wetu na hata wewe msomaji wangu kufuata yale aliyoyaamini Nyerere, bila kujali maneno ya hovyo ya baadhi ya watu kuwa maono na msimamo wa Mwalimu Nyerere hauna nafasi katika dunia ya sasa ya mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojiana pia mapinduzi makubwa ya siasa na uchumi wa dunia hii.

Maono ya Nyerere bado yako valid (natumia Kiingereza kuonyeha kwamba nimekasirishwa na watu hao) na bado yataendelea kuwa mwongozo kwa watu wenye kujali uwazi, ukweli na kutamini utu wa mtu.
Rais Benjamin Mkapa anamaliza muda wake, na kwa kiasi kikubwa, ukiacha kusukumwa na mabadiliko ya dunia hii, ameweza kufuata misingi ya Mwalimu Nyerere kwa vitendo na ndiyo maana amekuwa kiongozi anayeogopwa na wala rushwa, mafisadi, walafi na wanafiki.
Tunataka Rais ajaye, Inshaalah, awe kama waliomtangulia. Tusuburi tumuone.

Kwaherini.

Mifupa ya Rwanda kuamsha ‘vita’


Kumbukumbu ya mifupa nchini Rwanda,
injini itakayoleta mauaji mapya


Rwanda sasa yaonekana kujengeka katika nguzo imara za amani na nuru ya umoja wa kitaifa inaanza kung’ara. Hii imewezekana kutokana na juhudi za serikali ya Rais Paul Kagame kutokomeza mganyiko wa wananchi kutoka jamii mbili kubwa nchini humo; Watutsi na Wahutu.
Jamii hizo mbili kubwa awali zilikuwa na uhasama mkubwa hata kusababisha mauaji ya halaiki ya wananchi takriban milioni moja wa Rwanda mwaka 1994.
Katika mauaji hayo Watutsi wengi zaidi ya Wahutu, walipoteza maisha katika mapigano yaliyochukua siku 100 tu.
Dalili za kutokea kwa mauaji hayo zinaelezwa zilianza kujitokeza mapema, na hata baadhi ya taasisi za Umoja wa Mataifa na nchi wafadhili kuarifiwa, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuzuia vita hivyo vya Wanyarwanda wenyewe kwa wenyewe.
Vita hivyo na hata matokeo yake, sasa ni historia na itabaki kuwa kumbukumbu, siyo kwa wananchi wa Rwanda na wapenda amani duniani kote miaka nenda rudi.
Rais Kagame katika mikakati yake ya kuhakikisha vita hivyo havitokei tena, amekuwa akitumia mbinu mbalimbali kutimiza azma yake kwa lengo la kuwa na Rwanda yenye amani na utulivu.
Kiongozi huyo, amekuwa akifuatilia kwa ukaribu zaidi kila hatua ya kutokomeza punje za uhasama kila zinapoanza kujitokeza.
Rais Kagame anaelezwa kuwa amekuwa akiwaonya wote anaowang’amua kuwa na nia ya kuwabagua watu wa jamii nyingine.
Kwa kutumia televisheni na redio za serikali, Rais Kagame amekuwa akiwataja kwa majina na hata picha zao kuonyeshwa, wote wanaoshukiwa kuwa na chokochoko za kuvuruga umoja wa Rwanda ambao sasa unaimarika zaidi kuliko kipindi chochote cha historia ya nchi hiyo.
Anaelezwa kwamba hana uvumilivu kwa viongozi wenye tabia za kibaguzi na pindi wanapogunduliwa wamekuwa wakifukuzwa kazi kila kukicha.
Mbali na hatua hizo, Rais Kagame amekuwa akitumia hata mbinu za ‘medani’ kuhakikisha kwamba uhasama na mbinu zozote chafu zinazuiwa kabla hazijaleta madhara makubwa.
Katika kuhakikisha kwamba silaha zinabaki mikononi mwa majeshi pekee, Rais huyo amekuwa akitoa wito kwa wananchi wote kusalimisha silaha hizo, ingawa baadhi wanakaidi hatua hiyo na kuzificha.
Taarifa zinaeleza kwamba kiongozi huyo mwenye taaluma kubwa ya vita vya nchi kavu, aliwahi kuwaamuru wananchi wa kijiji kimoja kukusanyika kwenye uwanja wa wazi na kuziacha nyumba zao, huku yeye na watendaji wengine wa serikali wakipekua nyumba hadi nyumba kutafuta silaha zilizofichwa.
Zoezi hilo liliwezesha kukamatwa kwa silaha nyingi na wahusika walifikishwa mbele ya sheria kujibu tuhuma za kukaidia amri ya serikali.
Kagame mwenyewe, katika kumbukumbu ya miaka 10 tangu kutokea kwa mauaji hayo mwaka, alisema kwamba hatasita kuwachukulia hatua kali zaidi wote wanaoonyesha kutojali amani iliyopo na kuchochea uhasama baina ya jamii za nchi hiyo.

Habari zaidi zinaeleza Kagame ameapa ‘kummaliza’ yoyote mwenye uchu wa kumwaga damu ya ndugu zake Wanyarwanda kwa kisingizio cha ama ujamii, madaraka, wivu au hata mali.
Njia hizi zinasifiwa na wengi ndani ya mipaka ya Rwanda na hata nje, huku baadhi wakimwelezea kutofuata misingi ya haki za binadamu katika kutekeleza mikakati yake.
Vyovyote inavyoweza kuelezwa, Kagame ni mwokozi wa amani iliyopotea kwa muda mrefu kiasi cha kusababisha chuki miongoni mwa jamii za Rwanda.
Pia Kagema anawataka watendaji wote wa serikali kuwa na ajenda ya kutokomeza utengano kwa kila kikao ama mkutano unaofanyika.
Sambamba na njia hiyo, serikali ya Rwanda imeanzisha makumbusho ambayo yatakuwa yakitunza mafuvu na mifupa ya watu waliokufa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, lengo likiwa ni kuwakumbusha ubaya wa vita Wanyarwanda na hata wageni wanaopata fursa ya kufika nchini humo.
Njia hii, pamoja na kwamba inaweza kwa muda huu, kuonekana inafaa kutambulisha ubaya wa vita, lakini ni njia isiyofaa hata kidogo.
Haifai kwa kuwa inaongeza machungu na kuendelea kuwakumbusha wengi machungu ya kuuawa kwa ndugu zao huku wakiwafikiria wachache waliokatisha maisha ya wapendwa wao.
Busara siku zote inaonyesha kuwa njia sahihi ya ufumbuzi wa matatizo yaliyotokea ni kusahau mabaya ya nyuma. Sasa iweje leo Rwanda inayaanika mabaya yaliyotokea ili kuepusha kutokea tena. Inawezekana kabisa katika makumbusho haya waliofikiria walipotoka na sasa wanapaswa kujisahihisha.
Ni vyema mafuvu hayo na mifupa yote inayoonyeshwa kuzikwa upya ikiwa ni ishara ya kuzika mifarakano na kusameheana daima.
Binadamu, kama walivyo wanyama wengine wote, hujenga chuki kila wanapoona muuaji wa ndugu zake na hili haliwatengi wananchi wa Rwanda hasa wa jamii ambayo ndugu zao waliteketea kwa wingi.
Inaaminika kwamba jamii ambayo ndugu zao hawakufa kwa wingi, ilitokana na jamii iliyoonekana dhaifu, kujihami na kinyume cha hivyo, labda leo historia hiyo hiyo ingekuwa ikitambulisha vifo vya watu wa jamii moja.
Hisia kwamba kuanzishwa kwa makumbusho yaliyojaa mafuvu na mifupa ni njia mojawapo ya kutaka kuogopesha jamii moja, huenda zikawa na ukweli kwa asilimia kubwa.
Inawezekana kabisa kwamba mafuvu na mifupa hayo, badala ya kuwakumbusha mabaya ya vita, yakachochea chuki miongoni mwa jamii na hata kuwasukuma walioonewa zaidi, kulipa kisasi bila kujali matokeo ya hasira zao.
Itakumbukwa kwamba Alfred Nobel, mwanakemia, raia wa Sweden aliyefariki mwaka 1896, alikuwa na mawazo kwamba dunia inaweza kuwa mahali pa usalama zaidi ikiwa kila nchi itakuwa na silaha kali zaidi.
Nobel ambaye alipata utajiri mkubwa kutokana na kutengeneza na kuuza silaha kali sehemu nyingi duniani, leo hii angefufuka angeweza kabisa kuikana kauli yake ya hovyo.
Angeikana kutokana na ukweli kwamba, hata kabla ya miaka 20 kufika akiwa kaburini, kulizuka vita kuu ya kwanza ya dunia na baadaye ya pili.
Mawazo hayo ya Nobel na vitendo vyake ndiyo leo yanaiweka dunia kuwa mahali pa wasiwasi, hakuna amani ya kuishi kwani kila mmoja anahofia kuzuka kwa vita kutokana na nchi kuwa na silaha kali na hata za sumu.
Ni hakika kuwa wapenda amani kote duniani hatutakaa kimya, tutanyanyuka na kupayuka hata kwa kutumia ndimi za kalamu zetu tukiomba kuendelea kuwepo kwa amani na umoja miongoni mwa Wanyarwanda kwa nia ya kujiletea maendeleo ya haraka.
Mungu aibariki Rwanda, Mungu aibariki Afrika.

Huu siyo mzigo halali wa ukimwi!


Viongozi wa Afrika wanaubebesha ukimwi mzigo usio wake

UKIMWI ni kweli unaua, ni ugonjwa ambao hadi sasa haujapata tiba ya uhakika wala chanjo ya kuzuia maambukizi yake.
Ni ugonjwa ambao, wataalamu wa sayansi ya tiba wanaendelea kuchanganya watu kwa kutaja sababu za chanzo chake ambazo zinakinzana kutoka kwa mtaalamu mmoja hadi mwingine
Wapo wanaodai kuwa ugonjwa huo ulianzia Afrika ambako eti watu, Waafrika walikuwa watundu mno kiasi cha kuwaingilia wanyama jamii ya nyani ambao wanaelezwa kuwa na virusi vinavyofanana na vya ukimwi katika damu.
Hao wa ni waongo, kwani wengi wanaoamini na kueleza hivyo ni wazunbgu, ambao kwa namna yoyote ile wana sababu ya kuipamba Afrika kwa mabaya, sawa na walivyokuwa mababu na mabibi zao waliopachika jina baya bara hilo; waliiita Afrika kuwa Bara la Giza.
Bara la giza kwa kuwa tu eti watu wake ni weusi na kwa kuwa maendeleo yake yalikuwa nyumba, wao wanaeleza hakukuwa na ustaarabu. Eti kwamba ustaarabu walileta wao.
Hivi ni ustaarabu gani huo? Wa kula kwa kutumia vyumba au wa kujisaidia katika vyoo vya kukaa. Kama ni nyumba zilikuwepo, kama ni mila na tamaduni zilikuwepo tena ambazo hazikuwa na tone la kusababisha mtafaruku katika jamii.
Jamii ilijumuika katika rika; kwa maana kwamba watoto walikuwa na makundi yao, wasichana nao walikuwa kivyao, wazee nao walikuwa na makundi yao. Utaratibu huu haukuwa wa aibu kama ambavyo tunashuhudia leo upuuzi uliojaa kwa jamii, bila kujali rika.
Ni ustaarabu gani walileta? Kuvaa uchi bila kujali nani ni nani na ana cheo gani katika familia au umri.
Haya ngoja niyaache hayo ya ustaarabu wa ajabu wa Wazungu.
Wataalamu wengine wanaeleza kuwa ugonjwa wa ukimwi ulitengenezwa katika maabara na Wazungu hao hao ambao walikuwa na lengo eti la kutaka kupunguza kizazi cha Afrika aambacho kilikuwa kikiongezeka kwa kasi. Lakini kumbe walikosea mahesabu na mambo yakawa yakiwafika hata wao.
Haya tuachane na sababu za kuwepo ukimwi, turudi kwenye hoja yetu ya msingi.
Hoja ya leo ni kwamba sasa hakuna kiongozi wa Afrika anayekubali kuwa ameshindwa kuwaletea wananchi wake na kuwaondolea umasikini. Kila mmoja anatoa visingizio vingi mno.
Ingawa ni kweli, kwamba ukimwi unachangia kuwepo kwa umasikini katika Afrika, lakini viongozi wanaubebesha mzigo mkubwa mno kwa kutoa takwimu ambazo hazina ukweli kabisa.
Kwanza idadi ya watu wanaokufa ni kubwa mno utadhani ni ugonjwa kama mdondo unaoua kuku kwa kila dakika mbili au tatu baada ya kuku kuwa ameambukizwa ugonjwa huo.
Hivi inawezekana namna gani kwamba katika wilaya moja kila siku wanakufa watu 2000? Je kijiji hicho kina watu wangapi? Hivi kama kina wakazi 200000 maana yake ni kwamba watu wote wa kijiji hicho watakwisha kwa miezi mitatu tu! Hii inawezekana vipi na kwa namna gani watu hao waliambukizwa kwa wakati mmoja kwani twajua ukimwi unachukua muda mrefu kuanza kujitokeza.
Takwimu hizo za uongo zinanikumbusha hao viongozi wa Amerika walivyosambaza taarifa za uongo kwamba katika jimbo la Darfur, eneo ambalo lina machafuko huko Sudan, kwamba wanakufa watu 10,000 kila siku. Huu ni uongo mkubwa, hivi wako watu wangapi huko Darfur? Kwa hesabu hiyo ni wangapi sasa wameshakufa?
Leo hii viongozi wa Afrika wanashindwa kuwajibika na kuwaletea maendeleo wananchi wao na wanabaki kuutaja ukimwi kuwa kikkwazo na kushindwa kuelezaz ukweli kwamba hawawezi kuongoza ama rushwa imezidi na mambo machafu yanayofanana na hayo.
Maji yanashindwa kufika mijini, pamoja na kubinafsishwa kwa huduma hizo, sembuse vijijini ambako hata hayo mapambo ya mabomba hayapo? Kisingizio cha yote hayo nii kwamba eti ukimwi umeongezeka. Jamani viongozi wetu wamefika mahali pabaya!
Viongozi wengi wa Afrika wanatumia ugonjwa huo kuwa kigezo cha kuficha ufisadi, kutokuwajibika na utawala bora katika kueleza kwao kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi wao.
Kila kiongozi anayelalamika kuhusu kuwepo kwa maendeleo hafifu katika nchi yake anautaja ukimwi kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo na kwamba unazidisha umasikini kwa watu wake.
Ukimwi sasa uneelezwa kuwa chanzo cha njaa, hata kama hakuna mvua mwaka huo! Jamani tumefika pabaya!
Serikal zetu za Afrika kwa kushindwa kuwajibika na kuwaondolea umasikini wa mali na mawzo wananchi wake, na kuwa na visingizo kibao kwamba ni vikwazo ukiwemo ukimwi, zinaonyesha kuwa zimeshindwa kazi na kuwatumikia wananchi.
Kinachofanyika kwa viongozi,a ama wao wenyewe kujinufaisha moja kwa moja au kwa kuwapa nafasi wake zao, mashemeji, wapwa na watoto wa ndugu zao nafasi ya kuchota kile wanachodhani ni halali yao, huku idadi kubwa ya wananchi wakiachwa hoi, wakiwa wanachungulia kaburi kwa njaa.
Inafanya watu kuamini kuwa serikali zetu sasa ni sawa kabisa na vyama visivyokuwa vya kiserikali (NGO) kwa kutoa takwimu za uongo na visingizio ili tu ziweze kupata misaada kutoka kwa Wazungu wanaoabudiwa huku.
Umasikini wa nchi za Afrika unachangiwa kidogo na suala la ukimwi na siyo kweli kwamba takwimu zinazotolewa na baadhi ya viongozi ni za kweli, bali zina lengo la kuficha kutokuwajibika kwao kwa wananchi waliowachagua.
Iweje watu wakose maji, umeme, chakula na kisingizio kikawa ukimwi?

Monday, October 11, 2004

Nyerere Hazina Tanzania

* Hii ni sehemu ya kitabu changu kilichochapwa mara baada ya kifo cha Mwalimu. Ni kitabu cha kwanza kuwa mitaani baada ya kifo hicho, ingawa 'wajanja' walikipoka na kukichapa kwa majina yao. Niliwasamehe kwa kuwa ilikuwa na maana ya kukubaliana na kazi yangu na pia walikuwa wakitoa mchango kwa Mwalimu kwa kupitia kalamu yangu. UNAWEZA KUPATA KITABU HIKI CHOTE KWA MALIPO KIDOGO- WASILIANA NAMI KWA MAIL YANGU
UTANGULIZI

Siku chache baada ya jeneza lililobeba mwili wa muasisi wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwasili Dar es Salaam toka London Uingereza, nilipata fursa ya kuongea na Makamu Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi, Dk. John Samwel
Malecela na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Chama hicho na serikali kuhusu nia yangu kuandika baadhi ya misimamo ya Mwalimu Nyerere.
Malecela alisema itahitaji muda mrefu kuandika mengi mazuri aliyoyafanya Mwalimu Nyerere na isitoshe itahitaji zaidi ya watu sita wenye kumwelewa, kuandika kitabu kuhusu maisha yake. Hata hivyo, Malecela alinitia moyo na kusema yale ninayoyafahamu naweza kufanya hivyo ili iwe kumbukumbu kwa Watanzania na wapenda amani kote duniani.
Viongozi wengine walishauri na kupongeza nia ya kuweka kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika kitabu, ingawa walishauri kuandika masuala yanayoweza kuisaidia jamii yetu na watu wengine waliokuwa wakipenda na kuhusudu misimamo ya Mwalimu.
Katika kipindi chote cha maisha yake, Mwalimu Nyerere amefanya mambo mengi katika taifa letu, bara la Afrika na dunia nzima kwa jumla.
Miongoni mwa kazi hizo alizokuwa akifanya, juhudi za makusudi kabisa aliziweka katika kuonya, kutahadharisha, kuelimisha, kukemea na wakati mwingine kufurahisha kwa kauli na vitendo vyake.
Wosia, maono na maonyo ya Mwalimu Nyerere ni hazina kwa Tanzania kama ilivyo kwa waasisi wa mataifa mengine kama India yupo Mahatma Gandhi, China yupo Mao Tsetung na sasa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Hazina iliyokuwa ndani ya kichwa chake ndio hasa inabeba jina la kitabu hiki: MWALIMU NYERERE HAZINA TANZANIA.
Hii ndio kazi niliyoifanya.

NYERERE: HAZINA TANZANIA

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni hazina. Hazina isiyokauka wala kumalizika. Ni hazina inayodumu hadi mwisho wa dahari.
Hazina inayotegemewa na kila Mtanzania, mpenda haki, amani, maendeleo na uhuru. Hazina inayowalinda na kuwatukuza wapenda haki wote na kuwalaani mafisadi na makaburu popote walipo, bila kujali rangi ama tofauti za maumbo yao na sehemu wanakotoka.
Hazina inayowaponda na kuwalainisha wanafiki kwa ulafi na ufitini wao; wanaopenda kuneemesha matumbo yao na yale ya vitegemezi vyao; wasiojali maslahi ya umma kwa kutumia dhamana za uongozi kuiba na kufuja mali za nchi
Hazina inayoogopwa na wote wenye tabia mbovu na chafu. Hawa hawawezi kuiharibu wala kuwarubuni wengine wenye busara kuibomoa hazina hiyo kwa kebehi wala kejeli.
Hazina ilijengwa na kusanifiwa na yeye mwenyewe aliyekuwa mwenye busara, mwona mbali na mwenye kupenda haki.
Mwalimu Nyerere hakutaka kuonea, lakini alikaripia pale palipojitokeza udhaifu.
Hazina ya Mwalimu Nyerere ilionya na kuadabisha; pia ilikuwa na wakati wa kupongeza palipostahili kusifiwa kwa jitihada na uwazi. Na hata leo inaendelea kufanya kazi hiyo.
Hazina hii ndani yake kuna busara, maono, maonyo na pongezi nyingi.
Ama kweli hazina yake katu, haiwezi kugegedwa na siafu wala mchwa, isipokuwa kulinda pasi na rupia.
Hivi sasa hayupo Mwalimu Nyerere anayepumua, ambaye Watanzania walimzoea, ambaye walipata muda wa kuchota busara toka kwenye kichwa chake, ambacho miaka michache tu baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961, kilianza taratibu kujaa mvi.
Mwalimu Nyerere amekufa na ametangulia huko ambako kila nafsi itafika, Inshallah.
Hazina ya Mwalimu, ambayo imesheheni hekima, itaendelea kudumu miongoni mwa jamii yetu Watanzania na kwingineko duniani.
Nani anajutia msiba wake kwa kusema Nyerere amekwenda na hazina yake? Ni wanafiki pekee.
Yote mazuri ambayo alitakiwa kuyafanya yamefanyika, tena yapo mengi, yamehifadhiwa.
Hazina ni sahemu ambamo kunahifadhiwa vitu vya thamani kubwa; ni sehemu ambayo mara nyingi ni yenye ulinzi wa kutosha ili kuwabana wezi na wote wenye malengo mabaya nayo.
Hotuba, taarifa na maandiko ya Mwalimu Nyerere, ambavyo alikuwa akivitoa kwa nyakati tofauti wakati wa uhai wake, vimehifadhiwa kwenye kanda ama kwenye kurasa kwa ajili ya manufaaa ya Watanzania na watu wa nchi nyingine duniani wenye kuthamini mambo aliyoyaamini na kuyapigania.
Hifadhi ya busara ya Mwalimu Nyerere ndio hazina. Hazina kwa maendeleo ya nchi, hazina kwa kiongozi bora, hazina kwa mwananchi wa kawaida na hazina kwa Taifa.
Mwalimu Nyerere alikuwa baba, babu na mlezi wa kila mmoja. Wapo wanaokejeli ubaba, ubabu na ulezi wake ambao ameutoa kwa Tanganyika, na baadaye Tanzania, kwa zaidi ya nusu ya maisha yake yote.
Mwasisi huyo wa taifa la Tanzania atabaki kuwa baba, babu na mlezi bila kujali nani anasema ama kuwaza nini, kutokana tu na hisia za kutokubaliana naye kwa kile alichokiamini.
Busara zake zimemjengea sifa na heshima kubwa kuanzia kwa watu waliotukuka sana duniani hadi kwa wananchi wa kawaida dunia nzima. Ni kwa kutambua ukweli huu, ndiyo maana watu wachache wanaomkejeli waziwazi, hata akiwa kaburini, wanaonekana vichaa; na wanaofanya hivyo kwa kificho husutwa na nafsi zao kwa kuona mazuri mengi aliyoifanyia nchi yake na bara zima la Afrika.
Mwalimu Nyerere siku chache baada ya uhuru, Desemba 1961, aliwaasa Watanganyika kufanya kazi kwa bidii ili kuliwezesha taifa kupata maendeleo ya haraka, badala ya kuwategemea watawala wa kikoloni ambao walikuwa wamefungasha virago.
Alisema si vyema kujifanya wanyonge katika kutenda kazi za maendeleo yetu wenyewe, kwani kwa kulea udhaifu huo, itafika mahali ambapo wananchi watashindwa kutatua matatizo yao wenyewe kwa unyonge huo huo, hivyo kuwa rahisi kwa wakoloni ambao wameondoka, kurejea na kutawala tena.
Mwalimu aliwahimiza wanaume kujituma katika kuchapa kazi kama ilivyo kwa wanawake, kwa kutambua kuwa Tanganyika isingeweza kujengwa na kina mama peke yao.
Aliamini kuwa wanaume wengi wakati huo, kutokana na imani za kimila, walipendelea kuagiza tu wanawake na watoto kufanya kazi za shamba na kuchunga mifugo, kama ilivyokuwa katika koo nyingi, huku wao wakirandaranda na kunywa pombe.
Ilimchukua muda mrefu kuzunguka nchi nzima, karibu kila kijiji kueleza maana ya kujitawala ili kila mwananchi popote alipo, aweze kuchangia maendeleo ya taifa changa la Tanganyika kwa kufanya kazi kwa juhudi na kusisitiza maarifa.
Nyerere aliwakemea viongozi walioko madarakani kwa hulka ya kujikusanyia mali kwa njia zisizo halali, hasa za kificho. Aliwaona viongozi wa aina hiyo kuwa hatari kwa uhai wa taifa kwani wanaweza kufika mahali wakatamani kuuza hata nchi kwa ajili ya kupata mali kwa manufaa yao binafsi; mali iliyokusanywa kwa jasho la wananchi.
Nyerere alisikika mara kwa mara akiwakemea viongozi wa namna hiyo na kusema kwamba ni wepesi kuuza uhuru wao. Alisema, hao ni viongozi ambao husahau matatizo yote ya wananchi na kukumbuka tu ya 'mabwana' wao.
Aliamini katika umoja na alisisitiza: Penye umoja, utengano haipo na kufanya adui yoyote kuogopa kuchezea jamii ya aina hiyo yenye mshikamano thabiti.
Mwalimu alisema hata adui yeyote, iwapo ataamua kuendelea na mpango wa kuvuruga palipo na umoja, itamchukua muda na fedha nyingi kutimiza lengo hilo na wakati huo huo wenye umoja nao watakuwa na mbinu mpya za kujibu mashambulizi.
Alishauri na akatoa maamuzi kwa Watanganyika kuishi kwa mshikamano, hatma yake ikiwa ni kuanzishwa kwa Operesheni Vijiji, ili kuwawezesha wananchi kuishi pamoja vijijini.
Nia hasa ya operesheni vijiji ilikuwa ni kuiwezesha serikali kutoa huduma kwa wananchi wake jwa urahisi zaidi. Huduma muhimu zinazozungumzwa hapa ni pamoja na elimu, afya, maji safi na nyingine za maendeleo.
Aliamini kuwa watu wanapoishi pamoja inakuwa rahisi kuwahudumia kuliko wanapokuwa wametawanyika. Alipenda kutoa mfano wa watu wanaoishi mijini na kusema kwamba wanapata huduma nyingi kwa sababu ni rahisi kuwafikishia mahitaji hayo, tofauti na kama wangekuwa wanaishi mbalimbali kama ilivyo vijijini kwa wakati huo.
Alithamini haki za binadamu na kusema ni kigezo cha msingi katika kudumisha amani na mshikamano, katika nchi moja kwa upande mmoja na katika dunia kwa upande mwingine.
Mwalimu alikemea utumiaji wa mitutu ya bunduki ama nguvu za dola katika kuzima ama kuzuia haki za watu, akieleza kuwa matumizi ya maguvu ya aina hiyo hayawezi kudumu milele kukandamiza na kuzuia haki kutendeka.
Mwalimu Nyerere alisisitiza; kwa kusema, iwapo kuna ukiukwaji wa haki za binadamu na serikali kujivunia uwezo wake wa dola katika kutenda uonevu, itafika siku ambayo wanaonyanyaswa na kugandamizwa wataamua, kwa mikono yao kuvunja vunja mitutu (ya bunduki) ya dola na kupata wanachokitaka; Haki.

MAONO YAKE

Maono ya Mwalimu Nyerere, baadhi yakiwa yameelezwa ndani ya kitabu hiki, yanaweza kuelezeka kama kioo muhimu kwa jamii tuliyonayo na pengine jamii itakayokuja ya watoto, wajukuu na hata vilembwe wetu.
Kauli alizozitoa zaidi ya miaka 30 iliyopita ndiyo mambo yanayojitokeza hivi sasa.
Nchi za Ulaya na Marekani zinaendelea na kila jitihada kurejesha umoja wao ili pengine kuweza kurejea katika nchi maskini kwa sura nyingine: Ya kuja kutawala, si moja kwa moja, bali kwa kukamata njia muhimu za uchumi, ikiwemo huo ubinafsishaji unaolazimishwa kufanywa na hao wanaojiita wakubwa wa dunia hii ili kuweza kutoa misaada na mikopo kwa maskini.
Muungano wa nchi nyingi za Ulaya, umewezesha hata kuwa na uchumi mmoja na sarafu moja ambayo itakuwa na nguvu zaidi. Hii ni dalili iliyopaswa kuigwa na bara la Afrika.
Lakini kwa upande wao, nchi za Afrika zinagombana zenyewe kwa zenyewe na kuvunja umoja wao, ama wananchi wenyewe ndani ya nchi moja moja ama kati ya nchi moja na jirani zake. Kwa kufanya hivyo, umoja katika nchi hizo unatoweka na kufanya ujenzi wa nchi zao kuwa ndoto. (INAENDELEA KITABUNI)

NYERERE: MAISHA, KUUGUA, KIFO

Hakuwa mnene wala mwembamba, alikuwa mwenye umbo la wastani. Alipendelea kudhibiti uzito wake, hakupenda kuzidi kilo 70.
Alipenda kuvaa nguo za kawaida na mara nyingi zisizo na ukosi. Miguuni alipendelea kuvaa viatu vya wazi. Uso wake ulikuwa umbo la yai, si wa mviringo: macho madogo na makali yaliupamba uso wake na kuonekana mtu anayejali, lakini asiyependa upuuzi.
Kinywa chake kilikuwa kimesheheni meno yasiyokuwa na mpangilio wa kuvutia: Ya mbele yalikuwa na ncha kali, yalikuwa yameachana toka jino moja hadi jingine.
Kutokana na kuwa na meno ya aina hiyo, alipachikwa jina la "Mchonga" na baadhi ya Watanznaia ambao walifurahia utani.
Masikio yake yalikuwa mapana, na bila shaka yaliyomwezesha kunasa mawimbi ya sauti kwa ubora zaidi, hayakuwa mazito katika kusikia.
Siku za uzee wake, kichwa chake kilibeba nywele zenye rangi nyeupe, zinazoelekeza kwa Kiswahili kuwa ni mvi.
Pamoja na uzee wake, ngozi ya mwili wake ilionekana nyororo, wororo uliotokana, bila shaka, na tabia yake ya kula vyakula ambavyo inaaminika hutunza ngozi na kuonekana 'changa' muda mrefu.
Alipendelea vyakula vya asili, visivyokuwa na mafuta mengi: Ugali wa mahindi na wakati mwingine mtama na uwele kwa mboga za majani na nyama, kikiwa ni kitoweo cha asili cha Wazanaki na makabila mengine ya wafugaji ya mkoa wa Mara.
Hili ndilo umbo la mtu maarufu duniani, Mtanzania msomi, Rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Burito Nyerere, aliyefariki dunia Alhamisi, Oktoba 14, 1999, katika hospitali ya Mtakatifu Thomas mjini London, Uingereza.
Maisha yake yalikoma siku hiyo baada ya mwili, msaada wa madaktari na dawa kushindwa kukabiliana na ugonjwa wa sarakani ya damu.
Anaondoka mjini Dar es Salaam kwa ndege Agosti 31, 1999 kwenda London, Uingereza kwa ajili ya matibabu ya kawaida ya ugonjwa huo ambao uligundulika mwilini mwake Aprili, 1998.
Katika safari yake, anaandamana na mkewe, Mama Maria daktari wake, David Mwakyusa na wasaidizi wake.
Baada ya kufika London, anakwenda hospitalini, St Thomas, siku inayofuata na kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na kuruhusiwa kuwa mgonjwa wa nje. Kwa siku 22 anaendelea kuwa mgonjwa anayekwenda kutibiwa hospitalini hapo na baadaye kurejea alikofikia.
Baada ya siku hizo 22, hali yake inabadilika ghafla a kupelekwa hospitalini hapo ambako analazwa na kupata matibabu yenye uangalizi wa karibu zaidi toka kwa madaktari bingwa.
Siku inayofuata hali yake inaendelea kuwa mbaya kuliko siku iliyotangulia. Madaktari wanaamua kumpeleka katika chumba cha uangalizi zaidi wa wagonjwa mahututi (Internsive Care Unit) ambamo anaendelea kupata huduma za karibu na uangalizi wa muda wote.
Kuanzia Oktoba Mosi, hali yake inakuwa ya mashaka zaidi kwani anashindwa kuongea, kutambua na hata kufumbua macho. Anashindwa hata kupumua na madaktari wanaamua kumwekea mashine inayomsaidia kupumua ili aweze kuendelea na tiba.
Juhudi za madaktari kidogo zinaanza kuleta matumaini baada ya kutoa taarifa kwamba ugonjwa unaanza kukubali dawa na anaaza kufumbua macho na kujigeuza.
Madaktari wanakuwa na matumaini ya kuendelea kuimarika kwa afya yake, hali inayowafanya kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua kwa muda ili aweze kuvuta na kutoa pumzi mwenyewe.
Kuondolewa kwa mashine hiyo kunaonekana ni hatua nzuri ya mafanikio katika tiba yake. Hata hivyo, kutokana na kutokuwa na nguvu za kutosha kuvuta hewa ya kutosha yeye mwenyewe anarejeshwa mashine hiyo.
Akiwa bado ndani ya chumba hicho, Oktoba 7 hali yake kwa mara nyingine inabadilika na kuwa ya wasiwasi zaidi na madaktari wanagundua ana homa kali.
Anaanzishwa tiba ya ugonjwa huo na wakati huo huo madaktari wanaeleza kuwa karibu viungo vyake vyote vinashindwa kufanya kazi.
Hali hiyo inawaongezea wasi wasi madaktari, familia yake na Watanzania kwa ujumla ambao wamekuwa wakipata taarifa sahihi za tiba yake kupitia magazeti, redio na televisheni za hapa nchini na nje. Madaktari wanaamua kuufanyia uchunguzi ubongo wake kuona kama bado unaendelea kufanya kazi.
Uchunguzi wa ubongo ndio hasa unaondoa matumaini ya kupona. Matokeo yanaonyesha ubongo umepata kiharusi kikali na hivyo umekwisha kufa.
Oktoba 14, 1999 saa 4.30 (saa za Afrika Mashariki) Mwalimu Nyerere anakata roho. Tanzania, Afrika na dunia nzima inampoteza kiongozi mwenye msimamo thabiti, busara na maono.
Watanzania kwa ujumla wao walitarajia kauli yoyote ya mwisho toka kwa kiongozi wao mpendwa, lakini haikuwa hivyo kwani hakuweza kurejea akiwa hai. Alirejea akiwa mfu, ndani ya jeneza.
Jeneza ulimokuwa mwili wake lilipokelewa na umati mkubwa wa Watanzania waishio Dar Es Salaam na miji mingine jirani na baadaye kupitishwa katika mitaa mbali mbali ya Jiji. Siku hiyo mwili wake unalazwa nyumbani kwake Msasani, Dar Es salaam na siku inayofuata unapelekwa kuwekwa Uwanja wa Taifa kwa wananchi na viongozi wa mataifa ya nje kutoa heshima za mwisho.
Mwili wa Mwalimu baadaye unasafirishwa hadi kijijini kwao, Butiama, mkoani Mara, ambako alizikwa sehemu ya Mwitongo, Oktoba 23, 1999 kwa heshima zote za Kitaifa.
Hiyo ikawa safari ya mwisho ya maisha ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Burito duniani.
Mwalimu Nyerere alizaliwa katika majira ya mvua nyingi na kuanza kwa kilimo katika kojiji cha Butiama. Kijiji kilichopo kilomita 40 mashariki mwa mji wa Musoma, mkoa wa Mara.
Majira hayo katika kijiji hicho inakisiwa kuwa huwa ni kati ya miezi ya Machi na Aprili. Hivyo basi kwa kuwa enzi hizo hakukuwa na wasomi kijijini hapo, Mwalimu Nyerere na familia yake walikubaliana kuitambua tarehe 13 Aprili ,1922 kama siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Baba yake, Nyerere Burito, alikuwa chifu wa kabila dogo la Wazanaki ambaye alifariki mwaka 1942 akiwa na umri wa miaka 82. Nyerere ni jina ambalo alipewa mzee huyo na baba yake Burito likiwa na maana ya wadudu wanaoharibu mazao wenye umbo la 'washawasha'. Hivyo nyerere kwa Kizanaki ni wadudu hao.
Mama yake Mwalimu, Mugaya alikuwa mke wa tano miongoni mwa wake 18 wa Chifu Nyerere Burito. Mama huyu baadaye aliitwa Christina baada ya kubatizwa kufuatia imani yake katika dini ya kikristo, dhehebu la Kikatoliki.
Christina Mugaya wa Nyang'ombe alifariki mwaka 1997, akiwa anakadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 100.
Maisha ya Mwalimu wakati wa utoto wake hayakuwa tofauti na watoto wengine wa kijijini alioishi nao wakati huo. Alichunga ndama, mbuzi na kondoo akisaidiana na wenzake.
Kwa kawaida hakuvaa nguo wakati akifanya kazi hiyo, na jamii ya wakati huo, hasa vijijini, haikujisumbua kuficha 'utupu' wa mtoto anapokuwa mdogo, hasa wa kiume.
Alipotimu umri wa miaka 12, Kambarage alipelekwa katika shule ya Mwisenge, iliyokuwa umbali wa karubu kilomita 30 toka Musoma mjini, kuanza masomo ya awali.
Habari za shule zilimfikia Kambarage kupitia kwa kijana mmoja kijijini hapo aliyeitwa Mwanangwa Marwa, aliyekuwa akisoma shuleni Mwisenge na baadaye kukolezwa na kaka yake, Wambura, aliyekuwa mtoto wa Wanzagi.
Kambarage alivutiwa sana na habari hizo na alikuwa akistaajabu kuona wenzake hao wakiwa wamevaa nguo na kuweza kusoma maandishi toka kwenye madaftari machache waliyokuwa nayo.
Hakujua ni nini kilichokuwa kikisomwa na mwenzake. Lakini inasemekana alivutiwa na 'usanii' wa Mwanangwa wa kupitia mistari iliyokuwa imeandikwa kwa mashine.
Baada ya kuupenda 'usanii' huo wa kusoma, Kambarage alimwendea mama yake na kumweleza jinsi Mwanangwa anavyoweza kufanya 'maajabu' ya kusema maneno toka kwenye kitabu. Akamweleza pia nia yake ya kufuatana na kijana huyo kwenda shuleni kusoma. (INAENDELEA KITABUNI)

NYERERE: RAIS FUKARA
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amefariki akiwa fukara. Hana kitu cha fahari cha kujivunia, mbali na busara na msimamo kwa kile alichokiamini.
Hana lolote la kuweza kunyooshewa kidole na binadamu yeyote kwamba alikuwa na mali nyingi kupindukia ambazo alizipata kwa njia ya udanganyifu.
Alikuwa, amekuwa na ataendelea kuwa mjamaa wa kweli asiye na mfano ndani na nje ya bara la Afrika. Alikuwa na msimamo usiotetereka wala hakuwahi kumpigia magoti mtu kwa mali au utajiri wake.
Aliwakemea wote waliojaribu kumwambia lolote kuhusu kuchota mali za umma kwa ajili yao na ndugu zao. Aliwapa ukweli tena usiokuwa na kificho; Aliwaambia hapana na kweli ikawa hivyo hadi mwisho na wao kukata tamaa.
Kwa wabinafsi na mafisadi, Mwalimu alionekana mjinga kwa kutotumia nafasi aliyokuwa nao kujichotea mali. Hakuweza kamwe kujilimbikizia mali pamoja na kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Nyerere alikuwa ni binadamu tofauti. Kwa kawaida binadamu amezaliwa na tabia ya ubinafsi, lakini yeye hakuweza kuwa na tamaa ya kuiba ama kuchota raslimali zilizokuwapo wakati huo pamoja na umbumbumbu wa idadi kubwa ya wananchi wa Tanganyika, ambao wengi wao kwa wakati huo hawakuwa na elimu wala ufahamu wa kutosha juu ya mambo mengi.
Tabia hii ilifanya Mwalimu ajikusanyie mashabiki na marafiki wengi na alifanikiwa kuipenyeza kwa baadhi ya watumishi waliokuwa madarakani wakati huo.
Ufukara wa viongozi waliokuwa madarakani si dhambi; wala si kosa kwa viongozi walioko madarakani kutumia fedha halali za mishahra yao na masurufu mengine ya lazima kujijengea nyumba na mahitaji mengine muhimu.
Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa kiongozi yeyote Tanzania au nchi nyingine masikini anayeweza kuwa na kasri ama gari la gharama kubwa wakati mishahara si mikubwa, isiyoruhusu kufanya vitu vya kuogofya; na kama anavyo vitu vya fahari kubwa ni wazi kuwa atakuwa akiiba ama mali ya umma au kula rushwa.
Nyerere 'aliwaambukiza' tabia hiyo viongozi wengi waliokuwa chini yake na ambao, hata leo baada ya kustaafu, wamebaki kuwa watu wasiokuwa na msimamo thabiti kwa maisha yao na familia zao kwa kuwa tu hawakuweza kujichotea mali kwa rushwa au wizi. (INAENDELEA KITABUNI)

Sunday, October 10, 2004

Wangari: Mwanamke wa shoka

Wangari: Mwanamke wa kwanza Afrika
kushinda Nishani ya Amani ya Nobel


L Ana msimamo usiotetereka, awabwaga magwiji washiriki 194


ALIKUWA na habari kwamba Ijumaa mshindi atatangazwa kwani ni miongoni mwa watu 194 waliopendekezwa kuibuka washindi wa medali yenye heshima kubwa duniani.
Lakini, tofauti na mapendekezo ya watoto wake na marafiki, hakuwa na mchecheto wa ‘kuganda’ kwenye luninga yake au redio akisubiri kutangazwa kwa mshindi.
Watoto na jamaa zake, asubuhi ya siku ya kutangazwa mshindi walimsihi aache shughuli zake ili asubiri mshindi kupatikana kwani walimwekea asilimia kubwa ya kuwa miongoni mwa washindi.
Hakukubaliana nao, alidamka kama kawaida yake na kuangalia ratiba yake ya siku inamweleza kufanya nini. Ratiba ilimweleza kuwa alitakuwa kuhudhuria hafla ya upandaji miti nje kidogo ya jiji la Nairobi. Shughuli hiyo ilikuwa ifanyike mapema kabla ya kwenda ofisini kwake ambako angeendelea na kazi zake za kawaida.
Hiyo ndiyo ratiba ya Wangari Maathai, mwanamke msomi, mpigania haki na mwanamazingira mahiri wa Kenya ilivyokuwa siku hiyo.
Watoto wake wawili na jamaa wengine hawakuthubutu kuacha kioo cha luninga siku hiyo wakisubiri matokeo ya mshindi wa Nishani ya Amani ya Nobel kwa mwaka huu.
Mtoto wake mwingine, Wanjira alikuwa amekwenda ofisini kwake kuendelea na kazi zake. Anafanya kazi pamoja na mama yake kwenye chama kinachojishughulisha na uhamasishaji wa shughuli za kutunza mazingira cha Green Belt kilichoanzishwa na Wangari mwaka 1977.
Familia ya mama huyo ikiwa inaendelea kukodolea macho luninga, mara mtangazaji wa CNN alitamka kwamba kamati ya kuteua washindi wa Nobel mwaka huu, imemchagua Wangari Maathai kuwa mshindi na kuwabwaga washiriki wengine waliokuwa wakitajwa kuibuka washindi.
Mara baada ya taarifa hizo, simu za nyumba ya mama huyo zilianza kumimika kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kuongea na Mama Wangira, lakini hakuwepo na simu zote zilijibiwa na watoto wake na wanafamilia wengine.
Simu za ofisi ya Green Belt Movement nazo zilipigwa na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, marafiki na jamaa wengine wakitaka kuongea na mshindi Mama Wangari, lakini walijibiwa na Wanjira; ‘Mama hayupo, lakini nashukuru na ninapokea hongera hizo kwa niaba yake na zitamfikia’.
Miongoni mwa waliopiga simu kutaka kuzungumza na Mama Wangari walikuwa ni waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya nje na Kenya.
Katika kuhakikisha kwamba Mama huyo anapatikana, mwandishi wa CNN alipata namba ya simu ya mkononi ya mama huyo na kuongea naye kwa muda mfupi.
“Hallo, huyo ni Wangari Maathai,’ ulisikika upande mmoja wa simu kutoka kwa mwandishi wa CNN ambaye alijitambulisha na baadaye kutoa pongezi kwa kuchaguliwa kuwa mshindi wa Nishani ya Amani ya Nobel.
‘Ndiyo ni mimi na nashukuru sana kwa pongezi zao, haya naweza kukusaidia nini,’ alisema mama huyo akitaka kujua kilichokuwa kikihitajiwa na mwandishi huyo.
Wakati mwandishi huyo akiendelea kuuliza maswali yake, mara simu ilikatika kutokana na kuishiwa nguvu ya betri yake. Mama Wangira alishangaa kukatika huko kwa ghafla.
Lakini alipogundua kuwa simu yake imezimika kutokana na kukosa nguvu ya ‘umeme’, aliamua kuiweka kwenye mkoba wake na kuendelea na kazi yake ya upandaji miti ambako alikuwa akishirikiana na wananchi wa eneo hilo.
Kutobabaika kwa mama huyo kwa zawadi ama ushindi wa nishani hiyo yenye heshima kubwa duniani, na kuendelea na kazi yake ya kupanda miti inaonyesha mama Wangari alivyo na msimamo wa nafsi na vitendo vyake juu ya utunzaji wa mazingira.
Zawadi, nishani na tuzo mbalimbali kwa Mama Wangari siyo vitu vigeni, kwani amepata nyingi mno kutokana na juhudi zake za kutetea haki za wanawake, uhuru, utunzaji wa mazingira na maendeleo.
Kwa kupata nishani ya Amani ya Nobel, anakuwa mwanamke wa kwanza Afrika kutunukiwa nishani hiyo ambayo huenda sambamba na zawadi ya kitita cha zaidi ya dola za Marekani milioni moja. Mama huyo pia ni mwanamke wa kwanza Afrika kupata shahada ya udaktari na kuwa wa kwanza kuongoza kitivo cha tiba kwa wanyama katika Chuo Kikuu cha Naorobi, Kenya.
Jina la mama huyo liliyashinda majina mengine 194 yakiwemo yanayofahamika zaidi duniani; George Bush, Tony Blair na Hans Blix ambaye alikuwa kiongozi wa ukaguzi wa silaha zilizokuwa zikitajwa kuwepo Irak.
Huyo ndiye Profesa Wangari Maathai (64) ambaye siyo tu kwamba anafahamika na kuheshimika zaidi na jamii ya Kenya, bali pia dunia nzima ya wapenda maendeleo, uhuru na utunzaji wa mazingira inamwelewa na kumpa heshima kubwa.
Heshima na kutukuka kwa mama huyo kunatokana na juhudi zake binafsi za kutetea wananchi wanaokandamizwa, kunyanyaswa na maonevu ya kila aina na pia kupigania haki za wanawake kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kwamba, katika jamii ya Afrika, ni kundi ambalo limeachwa nyuma katika maendeleo kutokana na mazingira na historia ya watu wa bara hilo.
Mama huyo alianza harakati za kutetea uhuru na maendeleo ya watu wa Kenya miaka mingi, kabla ya ‘kutunisha misuli’ yake maeneo mengine ya Afrika na dunia.
Historia inaonyesha kuwa mama huyo akiwa kijana mdogo akisoma shule ya msingi na hadi sekondari hakupenda kuonewa na wanafunzi wenzake na hata walimu. Alisimama katika ukweli mara zote na aliweza kuwashawishi wanafunzi wenzake kutokuwa na heshima za woga wanapoonewa.
Alizoea kusema; ‘Simama, tembea katika haki bila woga ili kujenga heshima na uhuru,” – tangu akiwa mdogo na kukua na usemi huo hadi leo anapojiaandaa kwenda kupokea nishani yake na fedha mjini Oslo, Sweden, Desemba 10, mwaka huu.
Mama Wangari, kutokana na kuona umuhimu wa kuwa na ili kupata muda mwingi wa kuelimisha jamii kuhusu mazingira, haki za binadamu na maendeleo kwa ujumla, aliamua kuacha uhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi na kuanzisha chama cha Green Belt mwaka 1977, ingawa vuguvugu la utetezi kwa wanyonge na mazingira lilianza kuonekana wazi zaidi mwaka 1976 na kuwa tishio kwa uliokuwa utawala wa Rais Daniel arap Moi.
Akiwa huru sasa, mama huyo aliamua kuingia moja kwa moja katika utetezi wa suala la wanawake kunyang’anywa ardhi na waliokuwa viongozi wa nchi hiyo kwa ajili ya kujenga na kumiliki majumba makubwa.
Kutokana na vitendo hivyo vya viongozi wa Kenya wakati huo, mama Wangari aliamua kuanzisha kampeni kamambe ya kupinga suala hilo na hata serikali kushituka kwamba huenda kelele hizo zikawashitua zaidi wananchi na kusababisha vurugu kubwa.
Ili kumnyamazisha, serikali ilimkamata na kumfungulia mashtaka kwa kushawishi uchochezi ambao ungesababisha kuvunjika kwa amani na hata kuleta machafuko makubwa nchini hum. Hata hivyo aliachiwa na hiyo haikuwa kufuli kwa kinywa chake, aliendelea kuwashambulia viongozi hao na akawa na maisha yanayoelezwa kuwa ni kukamatwa na kuachiwa mara kwa mara na serikali bila kufunguliwa mashtaka.
Mama Wangari hakupendezwa kamwe na aina ya uongozi uliokuwa ukiendeshwa na serikali ya Rais Moi na alikuwa mpinzani mkubwa wa kiongozi huyo akimshutumu kwa kulea rushwa, uonevu na kila aina ya mabaya kwa wananchi wa Kenya.
Kila alipopata nafasi alimweleza Moi kwamba hapendezwi na uongozi wake na kuwa miongoni mwa wanasiasa machachari wa nchi hiyo.
Baada ya kuingia madarakani kwa serikali ya muungano wa vyama vya siasa, baada ya kukidondosha chama cha KANU katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, Rais Mwai Kibaki alimteua kuwa Naibu Waziri wa Mazingira kutokana na mchango wake kwa maendeleo ya sekta hiyo.
Utetezi wa mama Wangari kwa makundi yanayoonewa haukupendezwa na wanasiasa wengi wenye msimamo wa kati na kujipendekeza kwa watawala na viongozi wa Kenya na alijenga uadui na wengi waliokuwa wakifaidika na kuwepo kwa uonevu kwa makund hayo.
Mama Wangari hakuwa mtetezi wa haki za wengine pekee, pia alikuwa mtetezi mkubwa wa haki zake, kitu ambacho kilimsababishia kuachika kwa mumewe ambaye alikuwa mwanasiasa pia.
Akielezea sababu za kumwacha mama huyo, mumewe, alidai kwamba Mama Wangari ni mwanamke aliyeshindikana kutokana na kuwa na msimamo usiotetereka na ndiyo maana hawezi kuishi na mume wa Kiafrika.
Mumewe huyo ambaye wamezaa watoto watatu na mama Wangari anaendelea kudai kuwa mama huyo ni msomi mno kuzidi wanaume wengi, anaelewa mno na kwa haraka na zaidi ana mafanikio makubwa, vitu ambavyo siyo rahisi kwa mwanaume wa kawaida kuendelea kuvivumilia.
Msimamo wa aliyekuwa mume wa mama Wangari unaonekana kupitwa na wakati na unaitia aibu jamii kubwa ya Kiafrika kwa vile unaweza kuelezwa kuwa ni wa hovyo.
Iweje umuache mkeo kwa kuwa tu ana sifa za ziada na mafanikio makubwa? Kwa mama Wangari labda kuna sababu zingine, lakini kama ni hizo, jamii haipaswi kuiga mwenendo huo.
Mafanikio ya mama Wangari ni makubwa na changamoto kwa wanawake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Hongera mama Wangari Maathai.

Karibu mgeni

Mgeni wangu,

Kwa heshima na taadhima nakukaribisha kwa mikono miwili katika ukurasa huu wa mtandao (website) ambao utakuwa ukieleza mawazo yangu binafsi na kuchapisha makala zangu ambazo, ama zinakuwa zimechapishwa katika magazeti au ambazo hazijachapwa.
Makala hizo zitakuwa zikizungumzia mambo mengi kuhusu Tanzania - nchi yetu, Afrika-bara letu na dunia yetu. Kitakachokuwa kikizungumzwa hapa ni masuala mbalimbali yanayohusu siasa, uchumi, haki za binadamu, sanaa na utamaduni na masuala yanayohusu mazingira na jamii kwa ujumla.
Nitajitahidi kila ninapoweza kuleta masuala yanayogusa zaidi Watanzania na maisha yao. Hata hivyo siyo Watanzania tu, bali hata watu kutoka maeneo mengine ya dunia hii.
Hapa yatazungumzwa masuala ya amani, wakimbizi, vita, umasikini, utunzaji wa mazingira na pia kukuletea mambo ambayo yanayohusu uchaguzi wa nchi mbalimbali kwa mfano katika kipindi cha mwaka huu, Marekani itakuwa ikijiandaa kwa uchaguzi wake mkuu na hali kadhalika, mwaka kesho itakuwa na kazi hiyo hiyo.
Katika kuhamasisha wananchi wa Tanzania walioko nje na hata hapa nchini, kujiandikisha, ukurasa huu hautasita kutoa mchango wake katika hilo ili kuhakikisha kiongozi bora anachaguliwa na wengi waliojiandikisha.
Nakukaribisha sana mgeni wangu na kamwe sitokuacha. Endelea kuwa nami sasa.
Ubarikiwe